Waliochaguliwa kuandaa mpango wa maendeleo 2050 wote wanaishi Mbezi Beach au Masaki, wanalishwa kwa kodi za umma miaka yote, wana umri zaidi ya 50 yrs

Acha hizo wewe!
Ulitaka dira ya Taifa iandaliwe na kina VUNJABEI,MAJIZO,MWIJAKU,BABA LEVO MISOMISONDO (A.K.A DJ TRAVELLA)MWAMPOSA SHILOLE GIGY MONEY ...kisa wanaweza kwenda china?

hebu shika adabu bana
 
Huyo Mduma ana uzoefu gani?Lecture wa chuo kikuu huyo Mduma

Mleta uzi analalamika uwepo wa hao lectures kama Neema Mduma

Wewe unamtetea huyo Neema Mduma,Una undugu nae huyo mwalimu ?

Badala ya kujibu hoja za kujaza akademician au walimu wa vyuo vikuu wewe unamtetea mwalimu mmoja wa chuo kikuu cha Nelson Mandela Arusha aitwae Neema

Profesa kabudi na Ossoro wa madini si ndio walimuingiza chaka JPM kwenye madini na sasa tunalipa?
 
Nchi hii nafasi ziko kwa connections, huna connection hata uwe na uwezo kiasi gani utapata tabu sana kufikia nafasi za hivyo. Hiyo mipango wanayopanga mingi ni nadharia ndio maana wanachaguana wa huko huko ushefani.
 
Hizo Dira ni za Serikali na CCM Kuombea Mkopo IMF na WB….Maendeleo yataletwa na wewe na familia yako.
Lakini pia maendeleo husababisha kuwanyanyua wale walo nyuma kimaendeleo.
 
Waziri wa Mipango Kitila Mkumbo hiyo inatosha kukueleza kitakachotokea.
 
Niwarudishe nyuma kidogo, hivi ule mpango wa maendeleo wa miaka 20 wa Dr. Mpango enzi za JK ukiishiaga wapi?

Tumeshaupima kabla ya kuja na huu?
 
Ulitaka wachukuliwe wasio na maendeleo wakatupangie dira ya maendeleo?
 
Ningepewa kazi ya kuandaa mpango wa taifa, ningetumia 'nusu saa' kukamilisha hiyo kazi.
No wonder hiyo team ya wataalaam watavutana hapoo kila mmoja akijaribu kuonesha usomi wake mpaka 2025 itapita.
 
"Ndio hawa badala ya kuripoti uhalisia wao wanaripoti uongo na uzandiki ".
 
Upo sahihi Mkuu.

SIJUI NI LINI TUTAKUWA SERIOUS KWENYE MAMBO YA NCHI YETU, YANI KILAKITU TUNACHOFANYA NI LAZIMA KIWE NA KASORO.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Sio kila kitu, kasoro wanazilazimisha wao ziwepo. Unakumbuka rasimu ya tume ya Warioba? Watu wote huku mtaani waliiridhia kuanzia kwa Wajumbe jinsi walivyoteuliwa mpaka kwa rasimu yenyewe ilivyochakatwa hadi ikapatikana yakiwa ndiyo maoni halisi ya wananchi. Lakini ona sasa CCM walivyoifanya, wakaanza kuikosoa kwa vifungu hadi kikaja kitu kingine kabisa eti katiba pendekezwa ambayo waliondoa baadhi ya maoni ya wananchi na kuweka ya kwao waliyoona wana maslahi nayo. Kwa staili kama hiyo ya kulazimisha kasoro, kelele zitaacha kuwepo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…