Kuna mambo mengi yanotokea duniani kwa sasa khasa vita vya kijiografia, ukuaji Artificial Intelligence, kuibuka kwa silaha mpya, mabadiliko ya sayansi na teknolojia, mabadiliko ya tabia nchi, viashiria hatarishi vya hali ya usalama duniani, usalama wa chakula (food security), usalama na afya za wananchi, kuangalia sera ya elimu Kama yakidhi hali ya sasa ya kidunia na mambo mengine lukuki.
HAKIKA
'Usalama wa Chakula' ni jambo ufunguo kwa msingi thabiti wa maendeleo ya watu na vitu.
'Usalama wa Jamii' ni suala mtambuka.
Akili Bandia inaweza kusaidia katika mapinduzi ya kweli ya maisha ya watu duniani -- na tutaenda kutoboa kupitia ujuzi na ufundi wa kuratibu maendeleo kupitia mapinduzi ya nyenzo hii -- Ni 'mpango wa kando' kwa hata wataalam hawa walioteuliwa kwa dhamira hii ya kusanifu dira ya maendeleo.
Sasa suala la 'Akili Bandia' na 'Usalama wa Jamii' lina 'mafundi wake'; hawawezi kuwa watu wa kutokea kwenye akademia pekee yake ama wazoefu wa tawala na mipango; japo humo wanaweza kuwepo wawili watatu wenye kufanania na ujuzi wa haya kutoka kwenye hizo kada -- kada za akademia ama nchi-dola.
Haya ni mambo ya Elimu 2.0 na Elimu 3.0; lau kwenye nchi nyingi sehemu ya haya yanahodhiwa na 'kanisa' ama/na 'washirika wa himaya'.
Kuna mengi yanakwenda yanafanania kutokea, na 'yanayozuiwa kutokea' na hali yako '
nje ya uwezo wa wasomi mashudu' -- lau si matusi; ila ni ukweli mchungu unaohitaji baadhi ya wadau 'wawe wapole' ili wapatie maoteo sahihi ya watu na maendeleo duniani.
Kuna mawezekano ya 'magomvi ya michongo', 'vita kuu ya dunia', 'Maradhi ya kutengeneza kama yale yaliyoshindwa; na tena hapa Tanzania tulikuwa sehemu ya 'ushindi'; 'Uongo wa Kiufundi sana wa Siasa za Mabadiliko ya Tabia Nchi' na mengine mengi.
Sehemu ya haya ndiyo yamesabisha na yanaendelea kusababisha hata dira ya taifa inayokatikia kuwa 'ndoto nusu nusu' ya 'Watanzania'.
Kuna mambo mawili matatu yanaweza kuzungumzwa kwa kutangulia -- hata kama yatashangaza: Sura ya nchi na tawala inayonasibu ya kubadilika sana ikiwa dira yoyote inayokwenda kutengenezwa itapatia '
ukweli wa mambo' -- kufika 2050.
- Namna ya leo ya siasa za uwakilishi, inakwenda kubadilika sana kutokana na maendeleo ya matumizi ya Akili Bandia.
- Mifumo ya watu na serikali inakwenda kubadilika sana
- Mambo ya 'watawala wanaoabudiwa' labda kwa upambe na uchawa yanakwenda kuthibitisha 'mkosi kamili wa kimifumo', kokote kule hapa duniani -- japo hili linataka sana umma 'ujitambue' kabla kujifunza kupitia na migogoro mikubwa ya kijamii, siasa na maendeleo hapa duniani.
Kuna mambo yamefika ukomo wa matumizi yake lakini kikundi/vikundi vya 'watawala wa dunia' wana vuta nikuvute ya wao kwa wao --
hili ndilo linalochochea uwezekano wa 'vita ya dunia' ili 'kumwaga ugali'; hili tayari linaendelea...
Hili tukilifahamu vizuri tunaweza '
kujipanga' kulingana na ile mithali ya 'Mafahali Wawili Wapambanapo'...
Uchumi wa kifedha, mikopo na masoko globali umefika 'mwisho';
tunahitaji kubuni namna mpya ya uchumi unaweza kuwa himilifu na wakujitegemea kiukweli; labda itashangaza kulisema hili : 'ujamaa na kujitegemea' ilikuwa ni mapelekeo ya maendeleo ya watu na nchi, ambavyo kwa sehemu, 'mafundi wa uono' na 'washirika' walikuwa wakishawishi mawezekano ya '
njia ya tatu'...
SASA, dhamira iliyopelekea ushawishi wa dhamira ya kuanzishwa kwa Chama cha Mapinduzi ndiyo inaufunguo; ikiwa wanamipango wanataka 'kupatia' majukumu yao, ni vema wakatumia '
fremukazi ya uono na ufikirifu mifumo'...
Chama cha Mapinduzi ni 'mtoto' wa 'watu washirika' waliokuwa na 'maono' ya kiroho, maadili na miiko... Haya yote 'yamesahaulika'; lakini ili tutoboe kiza kinachofanania kutukumba, tunalazimika 'kujisahihisha sasa' ama 'hapo mbele'. Tukianza mapema basi tunapunguza mawezekano ya kero na mateso -- kero na mateso ya kujichanganya na kudanganyana...
Hapa Tanzania, 2023, bado hatuna 'Chama Mbadala' hasa; hatima ya nchi bado iko mikononi mwa 'washirika'...
Ufunguo wa 'kumalizana na siasa za nchi', kutengeneza serikali ya watu huru kweli inayonafasi kupitia wadau wa Chama cha Mapinduzi wenye upeo, uwezo na ufundi wa kurejea katika misingi--HILI LINAWEZEKANA;
linahitaji tu wadau kujiongeza kwa Elimu 2.0 na Elimu 3.0....