Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Uchaguzi wa Marekani ndio mkubwa zaidi duniani, kila kona ya dunia wanaufuatilia, uwe unaipenda au unaichukia Marekani.
Kwa matokeo haya ya Trump kushinda
1.Democrats wamelia kilio cha maombolezo, ushindi uliokuwa ukitegemewa umeyuyuka, wameshindwa kwa kishindo.
2.NATO na Umoja wa Ulaya wamenuna, Trump huwa hataki pesa za US kutoka sana kwenda nje ya US na Trump ni rafiki wa Putin adui mkubwa wa EU.
3.Ukraine wamelia kilio cha maombolezo, watalazimishwa kukubaliana na mashariti ya Russia kumaliza vita, msaada wa Marekani kupambana na Russia hautegemewi kuendelea.
3. Putin, Orban, Netanyahu na MBS wamecheka sana, wao na Trump ni washikaji sana. Saudi Arabia itaongeza biashara yake na US, Russia wanaweza kuondolewa vikwazo. Viktor Orban hayuko mnyonge tena ndani ya NATO, boss mkubwa wa NATO na yeye ni mapacha.
4. Hamas, Iran na Korea Kaskazini watabaki kuwa nyutro, Trump hatakuwa na msaada au afadhali yoyote kwao.
5.China-kawaida tu,
Wachina wao walishajua tangu zamani ku deal na yeyote wa US huku maslahi yao yakizingatiwa zaidi(Wachina unavyokuja ndivyo wanavyokupokea), pia wana misuli ya uchumi ya kutiliwa maanani na yeyote dunia hii.
6. Africa- Sisi tupo tupo tu, Iwe Kamala au Trump hakuna athari zozote kubwa za maana upande huu wa dunia kutoka kwa yeyote.
7.Wanaharakati wa demokrasia duniani kote- nusu wamecheka, nusu wamelia.
8.Wahamiaji na wazamiaji US-Kilio cha maombolezo.
9.India- Kawaida tu, hawa mambo yao na Marekani ni constant, huwa hayabadiliki awe yeyote pale White House, nafikiri Wahindi ndio Immigrants wanao enjoy sana US.