Waliocheka, Walionuna na Waliolia baada superpower kubadili muelekeo.

Waliocheka, Walionuna na Waliolia baada superpower kubadili muelekeo.

Sio kuwa matajiri kuwa tajiri sio issue kubwa kwa sisi traders but at least to be successful in life,ukizingatia nchi zetu Dunia ya tatu hizi ajira hakuna na biashara za brick and motor ni ngumu na umangimeza,umwinyi mwingi,Kodi lukuki sio poa.Mimi kama trader nafunga hesabu ya l$20k per month,at least I am successful and it makes sense.
Yaani uingize 20k dola kwa mwezi halafu usiwe tajiri aaah tafadhali mkuu
 
Sio kuwa matajiri kuwa tajiri sio issue kubwa kwa sisi traders but at least to be successful in life,ukizingatia nchi zetu Dunia ya tatu hizi ajira hakuna na biashara za brick and motor ni ngumu na umangimeza,umwinyi mwingi,Kodi lukuki sio poa.Mimi kama trader nafunga hesabu ya l$20k per month,at least I am successful and it makes sense.
Hongera mkuu heri nusu shari kuliko shari kamili
 
Nisimpendi kisa anawafuatilia sana watu ngoja wataona wenyewe maisha yao yakiwa mramba
 
Kuna thread uliweka nadhani ilikua januari mwaka huu ulikua unazungumzia uchaguzi wa marekani wa 2020.

Nilisema binafsi naona kuna uwezekano mkubwa Trump aliibiwa kura 2020 kupitia utaratibu wa zile mail-in ballots.

Ulisema Trump alishindwa fairly ila nataka tufuatilie mpaka kura zote zikisha hesabiwa tukajua jumla ya waliopiga kura ni wangapi, Harris amepata ngapi na Trump amepata ngapi kisha tulinganishe tena na 2020 na 2016, bado naamini kuna kitu tutajifunza.

Bado naamini kuna marehemu walimpigia kura biden 2020!
Mwaka 2020 Kuna uhuni ulifanyika kule Pennsylvania kwenye ballot boxes, ambao ndio ulimpa edge Biden hatimae akashinda na ndio maana mwaka huu Republicans walikuwa makini sana kwenye Hilo Jimbo hili yasije yanajirudia Yale yale
 
Hakuna hata kimoja kati ya vyote sijawahi zihusudu siasa za marekani
Putin mwenyewe hajawahi kuzihusudu siasa za Marekani ila alikuwa na mtu wake moyoni kwenye huu uchaguzi, itakuwa wewe wa huko Buza.
 
Putin mwenyewe hajawahi kuzihusudu siasa za Marekani ila alikuwa na mtu wake moyoni kwenye huu uchaguzi, itakuwa wewe wa huko Buza.
Una ujinga mwingi sana bwana mdogo.
 
Uchaguzi wa Marekani ndio mkubwa zaidi duniani, kila kona ya dunia wanaufuatilia, uwe unaipenda au unaichukia Marekani.
Kwa matokeo haya ya Trump kushinda

1.Democrats wamelia kilio cha maombolezo, ushindi uliokuwa ukitegemewa umeyuyuka, wameshindwa kwa kishindo.

2.NATO na Umoja wa Ulaya wamenuna, Trump huwa hataki pesa za US kutoka sana kwenda nje ya US na Trump ni rafiki wa Putin adui mkubwa wa EU.

3.Ukraine wamelia kilio cha maombolezo, watalazimishwa kukubaliana na mashariti ya Russia kumaliza vita, msaada wa Marekani kupambana na Russia hautegemewi kuendelea.

3. Putin, Orban, Netanyahu na MBS wamecheka sana, wao na Trump ni washikaji sana. Saudi Arabia itaongeza biashara yake na US, Russia wanaweza kuondolewa vikwazo. Viktor Orban hayuko mnyonge tena ndani ya NATO, boss mkubwa wa NATO na yeye ni mapacha.

4. Hamas, Iran na Korea Kaskazini watabaki kuwa nyutro, Trump hatakuwa na msaada au afadhali yoyote kwao.

5.China-kawaida tu,
Wachina wao walishajua tangu zamani ku deal na yeyote wa US huku maslahi yao yakizingatiwa zaidi(Wachina unavyokuja ndivyo wanavyokupokea), pia wana misuli ya uchumi ya kutiliwa maanani na yeyote dunia hii.

6. Africa- Sisi tupo tupo tu, Iwe Kamala au Trump hakuna athari zozote kubwa za maana upande huu wa dunia kutoka kwa yeyote.

7.Wanaharakati wa demokrasia duniani kote- nusu wamecheka, nusu wamelia.

8.Wahamiaji na wazamiaji US-Kilio cha maombolezo.

9.India- Kawaida tu, hawa mambo yao na Marekani ni constant, huwa hayabadiliki awe yeyote pale White House, nafikiri Wahindi ndio Immigrants wanao enjoy sana US.
Nawasikitia Waislam tu wa Ulaya na marekani, maana hili ni pigo kubwa sana kwao na kishindo cha kicheko kwa Israel
 
Back
Top Bottom