Waliofahamika kupitia migongo ya mastaa..

Waliofahamika kupitia migongo ya mastaa..

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
1. Petit man wakuache
Huyu jamaa amefahamika kupitia Wema Sepetu, jina lake limevuma na kutajwa tajwa sana baada ya kuwa karibu na madame. Sio muigizaji wala mwanamuziki.

2. Romy Jones
Huyu jamaa ni ndugu wa Diamond. Amefahamika sana baada ya kuwa karibu na mwanamuziki Huyo, japokuwa ana maringo na nyodo kuzidi Diamond. Na yeye huyu sio mwanamuziki wala mcheza filamu.

3.Penny
Huyu bidada ni mtangazaji wa Dtv. Alikuwa hafahamiki apo awali, Jina lake lilivuma sana na kujikuta akiingia kwenye ulimwengu wa mastaa baada ya kujihusisha kimapenzi na msanii Diamond, ni miongoni mwa watu wanaofuatiliwa sana na kuzungumzwa.

4.Mange kimambi
Huyu alipata umaarufu kupitia mastaa kadhaa wa Tasnia mbali mbali apa bongo, alianza kuzinguana kwenye blogs na msanii wa maigizo Sintah, Ray( kuhusu kifo cha Kanumba), Shigongo na wengine kadhaa, wengi walitaka kumjua ni mtu wa aina gani baada ya kuanzisha bifu na mastaa wa bongo, hatimaye akajikuta akiogelea umaarufu.

5.Chaga Barbie
Huyu alijipatia umaarufu baada ya kujihusisha kimapenzi na msanii wa Kenya Prezzo, jina lake lilivuma zaidi pale walipozinguana na Prezoo hadi kufikia hatua ya kutoleana maneno mbofu mbofu mitandaoni. Ni kati ya watu wanaofuatiliwa sana mitandaoni.

6.Agnes Masogange
Huyu alijipatia bahati ya kufahamika kwa kasi baada ya msanii belle 9 kumtumia kwenye nyimbo yake ya masogange ambayo Agnes alicheza kama Masogange, hadi Leo anafahamika kwa jina la masogange, ni kati ya watu wanaozungumzwa sana mitandaoni. Kesi yake ya madawa ya kulevya ilimuweka kwenye ulimwengu wa mastaa.

7.Najma
Huyu ni ex wa Mr blue, nae alianza kufahamika baada ya kujiingiza kwenye mahusiano na msanii huyo. Scandal yake ya kutoka na Diamond ilimuongezea credit kwa kiasi flan na kumfanya aongelew sana mitandaon, alishawah kujarib mziki pia na filamu.

8.Clement
huyu alifahamika baada ya kujiingiza kwenye mahusiano na super star Wema Sepetu, ni kati ya watu wanaozungumzwa sana mitandaoni hadi kesho, japokuwa sura yake haifahamiki kihivyo, bado watu wanapenda kujua kuhusu yeye na maisha yake.

9.Ostadh Juma
Watu mjini wanatafuta umaarufu kwa kasi, baada ya kuzipata pesa kwa wingi , aliamua Ku manage wasanii kama PNC, dogo Janja na wengine japokuwa hana management skills nzuri. Kumrudisha dogo Janja dar es salaam na kumweka kwenye kundi lake la watanashati entertainment pamoja na kumpiga picha PNC alipokuwa akijaribu kumuomba msamaha kumemfanya aongelewe zaidi na kufuatiliwa maisha yake mbaya zaidi hadi ya wazazi wake kitu ambacho kimem cost kwa kiasi Fulani.

10. Kajala Masanja
Kwenye mtandao wa instagram ana followers karibia elfu thelathini na kitu, wote wametokana na promo ya maana kwa shoga yake Wema Sepetu, kutolewa rumande na Wema Sepetu kumemuongezea umaarufu zaidi na kuwa miongoni mwa watu wanaozungumzwa sana, jina la kajala limekaa sana mdomoni mwa Wema Sepetu, hivyo kumfanya apate mashabiki wengi zaidi kupitia Wema. Ni mcheza filamu za kibongo.
 
Hureeeeee wapiii Kifasiiiii celebrity wetu wakuwaaacheee kesho ututundikie mapicha hapa
 
Hivi Vencha sijui anaitwa (Venture),kwenye verse kibao katajwa sana na wasanii wa hip hop,anahusika na nn hasa?
 
Hivi Vencha sijui anaitwa (Venture),kwenye verse kibao katajwa sana na wasanii wa hip hop,anahusika na nn hasa?

alikuwa ni produza wa mawingu rekods(sijui kama bd ipo) , pia alikuwa dj wa clouds tv(sijui km bd ni dj clouds)
 
huyu kifes bado hajawa maarufu kihivyo anajulikana lbd humu jukwaa la celebriti au na kwa wapambe wa dayamondi, hakustahl kuwemo kwny list hyo.
 
Kuna mmoja namuona insta anajiita martinkadinda jamaa wa misifa sana kupiga mapicha kama watotot wa kike kila sehem picha,simjui ni nani huyu?
 
Jamani Kifesi ni maarufu au unaleta utani?Au maarufu humu JF?
 
Umewasahau Mapedeshee 😉
 
Kuna mmoja namuona insta anajiita martinkadinda jamaa wa misifa sana kupiga mapicha kama watotot wa kike kila sehem picha,simjui ni nani huyu?

martin kadinda nahs alistahl kuwepo kwa list hyo. ni mpambe au meneja wa wema sepetu. amejulikana sana baada ya kuwa meneja wa wema. vlevle anajifanya ni designer wa singobatan, wakat hzo nguo ni za 60s kwa usa.
 
Kuna mmoja namuona insta anajiita martinkadinda jamaa wa misifa sana kupiga mapicha kama watotot wa kike kila sehem picha,simjui ni nani huyu?

Ni mwanamitindo na manager wa wema sepetu, pia ni big boss wa clothing line kama single button na kwachukwachu
 
martin kadinda nahs alistahl kuwepo kwa list hyo. ni mpambe au meneja wa wema sepetu. amejulikana sana baada ya kuwa meneja wa wema. vlevle anajifanya ni designer wa singobatan, wakat hzo nguo ni za 60s kwa usa.

Single button ilimpa umaarufu zaidi.
 
huyu kifes bado hajawa maarufu kihivyo anajulikana lbd humu jukwaa la celebriti au na kwa wapambe wa dayamondi, hakustahl kuwemo kwny list hyo.

Nime mdelete kaka
 
Back
Top Bottom