Waliofundishwa na Magufuli katika Sekondari ya Sengerema mje tuwachukue maelezo hapa

Waliofundishwa na Magufuli katika Sekondari ya Sengerema mje tuwachukue maelezo hapa

Alikuwa Mwalimu bora na akifundisha kemia lazima uelewe kweli kweli.. maana alikuwa ni msema kweli na akikuambia utafeli lazima ufeli...
nadhani pia mlimuombea hadi amekua rais huwa anasisitiza "muniombee"
 
Kabla hatujaanza kuchangia tujuzane kwanza ya Sengerema kipindi hicho HM Matu, kwa waliofikia mabweni ya Milambo au Kibasila na wapenzi wa kujifichà Chaka ambako ukionana na Mwalimu CHILIMILA utasafisha seawage wiki nzima. Kama huyajui haya wewe siyo wa SESESCO usichangie.
 
Kabla hatujaanza kuchangia tujuzane kwanza ya Sengerema kipindi hicho HM Matu, kwa waliofikia mabweni ya Milambo au Kibasila na wapenzi wa kujifichà Chaka ambako ukionana na Mwalimu CHILIMILA utasafisha seawage wiki nzima. Kama huyajui haya wewe siyo wa SESESCO usichangie.
Bosi Mimi nilikuwaga bweni la wajanja Mkwawa karibu na chaka, niliwahi kupigwa suspension baada ya kukutwa nimejificha 'Room7' na wenzangu mida ya class, nakumbuka mwaka 2002 kwenye graduu ya form6 alialikwa Magufuli (kipindi hicho waziri kijana) kama mgeni rasmi akatupiga changa la macho atatuletea TV kubwa, hadi natoka sikuiona. Sesesco bonge la shule sema migomo ilifanya iharibike, mabweni yote hayana vioo madirishani, binafsi nilisoma miaka miwili (2002-2003) wazazi walipohamia Songea kikazi wakanihamisha
 
Swala la ku balance equation kwenye chemistry alikuwasumbua wanafunzi wake kweli??????
 
Mwaka 1982 hadi 1983, Rais Magufuli alikuwa Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati.

Kwa wale mliobahatika kufundishwa na JPM mje hapa mtueleze uwezo wake wa kufundisha ulikuaje?

Na ni kwanini alifundisha kwa mwaka mmoja tu?
Hawa wanaweza kutueleza ukweli wa mambo
 
Mletamada..Kabla hujauliza swali, tuambie kwanza.....ni mrija upi uliobanwa kwako? Wizi, ukwepaji kodi, wafanyakazi hewa, wanafunzi hewa? Tuanzie hapo kwanza
Kusitishwa kwa ajira zaid ya mwaka mzma! Graduate mtaani bachelor ni sawa na std 7, full kudharaulika mtaani!
 
Mods bahna sio watu wazuri. Tangu lini kufundishwa na magufuli kuwe ni bahti?
 
Hakunifundisha,ila nilipata yafuatayo,he had no permanent friend,busy most of the time,alikuwa analalamika mshahara mdogo ndo maana alifanya maamuzi ya kujiendeleza ili apate mshahara mnono zaidi🙁
Wenzie wakidai mshahara mnono anawaambia acha kazi
 
Back
Top Bottom