Waliogundua hesabu ngumu walikuwa wanatafuta nini na walizigunduaje?

Waliogundua hesabu ngumu walikuwa wanatafuta nini na walizigunduaje?

wenyewe wa PCB na PCM wanakwambia hesabu ndio ya kupumzikia[emoji28][emoji28][emoji28]

kweli duniani tuko tofauti sana.
yaani aliyefaulu masomo yote alama za juu anaonelea bora akapumzike kwenye hesabu PCM kuliko kukumbana BIOLOGY ya PCB.
Mi History na biology nilikua nafeli ila sio Maths..masomo ya kukariri nacho kipaji!
 
Hesabu ni somo linalochukiza sana.
Tangu napata ufahamu nikiwa primary nilikua nafeli tu hesabu. Darasa la 4 mpaka la 7 nilikua napata 10% mpaka 20%, yaani 5/50 mpaka 10/50. Inshort primary nilikua mbumbumbu na mwonekano wa kimbumbumbu, mpaka nikawa nafananishwa na kilaza wa darasa, nikawa naitwa kwa jina la huyo kilaza.
Nilivyoanza sekondari nikaanza kujifunza mwenyewe kwenye kitabu bila kufundishwa. Nikawa najifunza mwenyewe kwa muda mrefu, kidato cha pili NECTA nikapata C (49%). Kutoka 10% - 20% mpaka 49% nikaona kumbe inawezekana!, likizo ya form 2 kwenda form 3 nikakazana nikawa najifunza mwenyewe kitabu cha form 3. Midterm ya form 3 nikapata 78% kumzidi aliyeongoza shule nzima kidato cha pili, yeye midterm alipata 77%, nikapata moyo zaidi. Nikamaliza book 3 na book 4 harakaharaka nikiwa form 3, nikiwa form 3 nikaanza kufanya mitihani ya form 4 na wanafunzi wa form 4, nikawa nawakimbiza form 4, grade As zikawa za kumwaga. Form 4 NECTA usiulize, nimetoka na banda la number.
Ndo siri ya hesabu haitaki uvivu soma daily na ukiijua unajuijua hakuna longolongo dunia nzima!straight if A=B=C baasi jibu ndo hilo hilo!
 
Hyperbolic functions

Hyperbolic hii Ni jamii ya watu wazimana waliokuwa wanaishi Urusi walikuwa wanajulikana kwa Jina ilo
 
Na hesabu za Trigs zinatumika katika ujenzi wa miundo mbinu hasa madaraja na barabara..

Leo hii ukimuuliza mtu kwanini kwenye kona kali ya barabara imejengwa ikiwa na slope uelekeo wa kona (sijui nmeeleweka hapa [emoji23]) na kwanini isiwe katika uwiano kama sehemu zingine, bila shaka wengi watakwambia hawajui.
Super elevation hiyo inaitwa mkuu
 
Sioni matumizi ya hesabu kama trigono ratio au logarithim ktk maisha ya kawaida. Yaan zinatumika wapi?

Mkuu, kila kitu kina matumizi yake. Mfano mdogo tu kwenye maisha ya mtaani, unapotaka kuwzeka nyumba lile paa unaloliona ni matumizi ya Trig Ratios ambapo utapata urefu wa Wima, Mlalo na Kitako pamoja na nyuzi mlalo wa paa ili liweze kumwaga maji( slopes na inclination angle).
Hesabu za juu zaidi kama finite element hutumika kukokotoa mambo magumu ya structures kama minara ya simu na minara ya kusafirisha umeme ( nadharia za kiuhandisi za juu yaani advance structural analysis katika kukokotoa forces, deformations, displacements, internal and external stresses and strains, nk. Minara ile ya grid hesabu zake ni hizo ngumu ngumu, na minara hii imo kwenye kundi gumu liitwalo Space trusses, tofauti na plane trusses kama zile za paa la nyumba)
Pia, kwa upande wa mambo ya simu na mawasiliano zipo hesabu fulani hivi huitwa Fourier Series, ni Advanced Integral, mawimbi yote haya tuyatumiayo yamepitia nadharia ya hizo hesabu za Fourier. Imeniwia vigumu kupata terminology rahisi ili kuweza kueleweka, lakini kila hesabu zina kazi zake.
Mfano Probability na Statistics, unaweza kujengea Hoja ya Kinadharia( Testing Hypothesis) katika mambo ya confidence intervals nk kutabiri uwezekano wa jambo kutokea katika sampuli za utafiti( bado sijaweza kuifafanua kiurahisi), itoshe tu kusema kila hesabu ina kaz zake.
 
Hesabu ni modeling ya physical phenomenon. Ukishajua hilo hakuna hesabu utasema ni ngumu. Hizo alama zinazotumika zisikutishe hata wewe una jina linalokutofautisha na binadamu wengine😂😂😂
 
Na hesabu za Trigs zinatumika katika ujenzi wa miundo mbinu hasa madaraja na barabara..

Leo hii ukimuuliza mtu kwanini kwenye kona kali ya barabara imejengwa ikiwa na slope uelekeo wa kona (sijui nmeeleweka hapa [emoji23]) na kwanini isiwe katika uwiano kama sehemu zingine, bila shaka wengi watakwambia hawajui.
Hii ni kweli hata kwenye autobhan ndio iko hivi
 
Hesabu ni somo linalochukiza sana.
Tangu napata ufahamu nikiwa primary nilikua nafeli tu hesabu. Darasa la 4 mpaka la 7 nilikua napata 10% mpaka 20%, yaani 5/50 mpaka 10/50. Inshort primary nilikua mbumbumbu na mwonekano wa kimbumbumbu, mpaka nikawa nafananishwa na kilaza wa darasa, nikawa naitwa kwa jina la huyo kilaza.
Nilivyoanza sekondari nikaanza kujifunza mwenyewe kwenye kitabu bila kufundishwa. Nikawa najifunza mwenyewe kwa muda mrefu, kidato cha pili NECTA nikapata C (49%). Kutoka 10% - 20% mpaka 49% nikaona kumbe inawezekana!, likizo ya form 2 kwenda form 3 nikakazana nikawa najifunza mwenyewe kitabu cha form 3. Midterm ya form 3 nikapata 78% kumzidi aliyeongoza shule nzima kidato cha pili, yeye midterm alipata 77%, nikapata moyo zaidi. Nikamaliza book 3 na book 4 harakaharaka nikiwa form 3, nikiwa form 3 nikaanza kufanya mitihani ya form 4 na wanafunzi wa form 4, nikawa nawakimbiza form 4, grade As zikawa za kumwaga. Form 4 NECTA usiulize, nimetoka na banda la number.
From Zero to Hero
 
Usinikumbushe machungu nilitakiwa Ku graduate ila kuna kimama kimenishika kwenye """linear algebras ""
 
Stori yako kama yangu. Hesabu zilikuwa zinanitesa sana. Nilipoingia form four tukapewa vitabu. Nikaanza kusoma Earth as a sphere, nikaona ha!, inaenda. Nikasoma na linear programming na probability. NECTA napata B hata mwenyewe sikuamini.

Hesabu zina matumizi mengi sana, kama hujui hesabu hata kukadiria gharama za kujenga nyumba utashindwa. Lazima ujue urefu na upana wa ukuta. Urefu na upana wa tofali nk
Mie hesabu za maisha ya kawaida hazinishindi ila zikishawekwa kwenye makaratasi tu ni kipengele
 
Na hesabu za Trigs zinatumika katika ujenzi wa miundo mbinu hasa madaraja na barabara..

Leo hii ukimuuliza mtu kwanini kwenye kona kali ya barabara imejengwa ikiwa na slope uelekeo wa kona (sijui nmeeleweka hapa [emoji23]) na kwanini isiwe katika uwiano kama sehemu zingine, bila shaka wengi watakwambia hawajui.
Kwenye kona Atasema anaongeza centripetal force [emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom