Waliogundua hesabu ngumu walikuwa wanatafuta nini na walizigunduaje?

Waliogundua hesabu ngumu walikuwa wanatafuta nini na walizigunduaje?

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Mihesabu kama ya Trigonometric ratios (Tan, Cos na Sin), Calculus n.k. na mihesabu migumumigumu ya chuo kikuu iligunduliwaje?

AA8F4780-6520-439C-8950-47A9F06E029D.jpeg


Yani mtu unasolve page nne ndio unapata jibu jamani!!! Sasa walifikiajefikiaje muafaka kwamba ukifanya hivi hivi ukaja hivi na hivi mpaka mwisho ndio mjibu huo umetiki?

02BDE474-CBDC-40C6-B876-4D2EFCC4A93F.jpeg


Kwakweli hesabu ni jambo la kushangaza sana. Hebu tupeni historia ya kugunduliwa hesabu mpaka leo. Na je, hakuna hesabu mpya zilizogunduliwa miaka ya karibuni?
 
Kiukweli kuna vitu MUNGU aliweka ndani ya watu na kila mtu anakitu chake cha tofauti.

Hesabu ni baadhi ya hivyo vitu alafu waliotunga vilikuwa vinakuja tu kichwani mwao na kuviandika.

Kinachonifanya niamini vimetoka kwa MUNGU madaraja na miundombinu wanatumia mambo hayo hayo ya trig na yanakuwa kweli.

#Ni mtazamo wala sio sheria
 
Kiukweli kuna vitu MUNGU aliweka ndani ya watu na kila mtu anakitu chake cha tofauti.

Hesabu ni baadhi ya hivyo vitu alafu waliotunga vilikuwa vinakuja tu kichwani mwao na kuviandika.

Kinachonifanya niamini vimetoka kwa MUNGU madaraja na miundombinu wanatumia mambo hayo hayo ya trig na yanakuwa kweli.

#Ni mtazamo wala sio sheria
Mi pia nina mtazamo kama wako! Kwa sababu kuna mambo mengine unaona kabisa kuwa kwa akili ya kawsida ya binadamu ni vigumu sana.

Juzi hapa na rafiki yangu tulikuwa tunaangalia ufanyaji kazi wa kitu kidogo tu, photocopy machine. Tukaangalia wingi wa vidudedude vilivyopo mle na jinsi inavyofanya kazi na kujiuliza hivi binadamu huyu alitumia miaka mingapi hadi kukamilisha hili? Mwishowe tukasema kama ulivyosema wewe mkuu, kwamba Mungu kuna alivyoamua kuvishusha kupitia tu binadamu
 
Hizo hesabu zilianza kugunduliwa kwa kufanya assumptions nyepesi tuu. Mfano calculus aliyezigundua alikuwa anajaribu kutafuta Gradient(slope) ya mstari ambao haujanyooka (curve) maana hapo mwanzo gradient(slope) ilikuwa inatafutwa kwa mstari ulionyooka( straight line).

So far nadharia nyingi za kimahesabu zimeonekana kuwa ni mwendelezo au marekebisho au ugunduzi mpya wa wanafunzi fulani kutoka awali walipoishia waalimu wao au wakubwa wao katika kazi.

Mfano THOMSON alikosolewa na mwanafunzi wake Ernest Rutherfod. So far Rutherford nae alikosolewa na mwanafunzi wake James Chadwik.


Isaack Newton alipata kufundishwa na mwalimu wake ambaye nae alikuwa mtaalamu wa mahesabu Isaac Barrow. Tafiti nyingi za Newton zilitokana na kukosoa tafiti za waalimu wake.
 
Back
Top Bottom