Kirumberumbe
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 982
- 1,167
Mkuu; Hiyo kuumiza kichwa namna ya kupata mahitaji muhimu.... ndo Hesabu zenyewe! Kila kitu ni Hesabu - hata kulala ni hesabu e.g. Utalala saa ngapi na utaamka saa ngapi ili uweze kutekeleza majukumu yako 1,2,3 n.k. Usipoweka mahesabu yako vizuri utajikuta unakimbia-kimbia tu siku nzima na umri unaenda. Time and Tide waits for no man. Hesabu hutumika mpaka kaburini😲 - huwezi kuacha kutumia Hesabu alimradi upo na unaishi. Hebu fikiria kwa case ya COVID-19 Je, wasingetumia hesabu kwamba mgonjwa apewe oxygen kiasi gani si wangekubugiza hewa hiyo tuu na matokeo yangekuwa mabaya kuliko COVID yenyewe? Hesabu/Mathematics ni somo TAKATIFU na linatawala masomo mengine yote- yooote kabisa( na fani zote hata Uchungaji). Ndo maana kila course yoyote/ combinations zote Arts or Science kunakuwapo na somo la Hesabu(Additional or Applied) - Tuipende tu Hesabu aisee hata kama inasumbua kichwa.Sisi tunaumiza vichwa namna ya kupata mahitaji muhimu kama chakula , mavazi na nyumba hayo mengine ni kazi ya wachache walio jaaliwa