The Genius
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 822
- 2,095
Taarifa kutoka mkoani Songwe zinaeleza kuwa Mwenyekiti wa UVCCM kata ya Maporomoko, na kiongozi wa Green guard wilaya ya Momba wamefariki kwa ajali baada ya kugongwa na gari wakiwa kwenye pikipiki, ikiwa ni miezi miwili tu tangu waliposhiriki igizo la kuizika Chadema kwenye jeneza na kuweka msalaba wakimshirikisha Dr.Tukia Akson lililofanyika mjini Mbeya.
Vijana hawa pia wanatuhumiwa kumpiga Mwenyekiti wa Chadema kata ya Maporomoko mzee Nsinge Nsinge (70) na kumjeruhi maeneo mbalimbali ya mwili hali iliyosababisha mzee huyo kulazwa hospitalini Tunduma kwa siku tatu. Tukio hilo liliripotiwa kituo cha Polisi Tunduma lakini vijana hao hawakuchukuliwa hatua zozote.
September 19 mwaka huu watu wengine wawili akiwemo Mwenyekiti wa CCM Ilala walifariki kwa ajali mkoani Morogoro wakitokea Mbeya kwenye shughuli za kisiasa ambapo pamoja na mambo mengine walishiriki kwenye igizo hilo la kuizika Chadema kwa mazishi rasmi ya kikristo na kufanya maombolezo.