Walioingia JKT kwa njia za panya kutimuliwa

Status
Not open for further replies.

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Jeshi la Wananchi (JWTZ) limetangaza kuwachukulia hatua viongozi wa ndani na nje ya jeshi hilo na vijana waliohusika katika vitendo vya udanganyifu katika uandikishaji wa majina ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Udanganyifu huo ulihusisha ukiukaji wa taratibu na kughushi nyaraka na vyeti vilivyotumika katika uandikishaji huo.

Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda, akizungumza jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Venance Mabeyo, alisema licha ya taratibu za uombaji kuwa wazi, baadhi ya viongozi wamebainika kutumia nafasi walizonazo kupenyeza majina ya ndugu, jamaa na rafiki ili wasajiliwe.

“Napenda kuwataarifu kuwa baada ya kubaini kuwako kwa udanganyifu huu, JWTZ/ JKT tutafanya uhakiki wa vyeti na nyaraka zote husika kwa vijana walioandikishwa tutashirikiana na ofisi ya Nida (Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa), Baraza la Taifa la Mitihani, Takukuru na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuwabaini waliofanya udanganyifu,” alisema Kanali Ilonda.

Ilonda bila kutaja uhakiki huo utafanyika lini na wakati gani, alisema utahusisha kuhakiki wa vyeti, nyaraka mbalimbali zilizokuwa zikihitajika kwenye uandikishaji huo pamoja na vyeti vya kuzaliwa na vipimo vya afya.

"Kwa kuweka usawa tutafanya uhakiki huu kwa kushirikiana na JKT, Nida, Wizara ya Elimu, taasisi zinazohusika na masuala ya rushwa, vyombo vya ulinzi na usalama, ili tuweze kuwachuja, tunataka kujiridhisha je, ni Watanzania kweli, wana afya njema, wana akili timamu, ametoka eneo husika na ana sifa stahiki, wale wenye sifa watachukuliwa, hata kama idadi yao itakuwa ndogo tofauti na matarajio yetu," alisema.

Ilonda alisema wale ambao watabainika kughushi watakamatwa na kufunguliwa mashtaka.

“Hakuna atakayesalimika labda wahame nchi, aliyeghushi vyeti na nyaraka mbalimbali kiwe cha kuzaliwa au daktari aliyetoa majibu ya uongo atakamatwa, waliowashawishi kughushi watakamatwa, waliotengeneza vyeti bandia, waliohusika kuwaandikisha vijana hao bila kuwa na vigezo, viongozi wote waliohusika kupenyeza majina wa ndani na nje ya jeshi nao watachukuliwa hatua kupitia mamlaka zao husika,” alisema.

Alisema hatua zitakazochukuliwa hazitaangalia wadhifa au cheo cha mtu kwa sababu lengo ni kusafisha nchi iwe na viongozi waadilifu na wanaofuata sheria na taratibu.

Your browser is not able to display this video.
 
Kama kuna mahali kuna double standard kwenye recruitment katima nchi hii. Inaanza jeshi alaf inafuata TRA. Trust me kama hakuna mtu unayemjua huwez kupata nafasi za JWTZ hata uwe na sifa zipi hupati....


Hata uhakiki huu bado nina wasiwasi nao kuna mgongano wa kimaslahi baada ya kila mtu kutaka jina lake liingizwe, ndo wakaamua kuumbuana lkn nalo litapita na mambo yatarudi katika uozo uleule
 
Kama wanahitaji usawa wanaoudai na kutoa mikwara wanayoisemea warudie UPYA ZOEZI ZIMA la USAILI.
Hakuna hiko kitu... HAPO WANATISHA ILI WAINGIZE WATU WAO...
BABA KANITUMA HAZIKOSEKANI..
 
Hapa ni uzushi tu. Kuna watu wanataftwa JKT kufukuzwa. Naimani tena ni wale wanaoonesha kutokuwa na imani na serikali ya Msgufuli.
 
wanawafundisha watu kutumia silaha alafu wanaturudishia mtaani
 
Wakitumbuliwa wanajeshi mtaani hapatakalika na uhalifu unaweza kuongezeka kwa kiasi kikubwa sana
 
Malengo ya jkt ni kutoa elimu ya kujitegemea na uzalishaji wa mali,sasa vyeti vya kazi gan wakati mwisho wa siku wanarudishwa majumbani.Hata ninyi nao mmeingia kwenye mtego wa siasa.
 
Kama vijana watarudishwa mitaani wasifundishwe kutumia mabunduki.

Kuhusu wakubwa kuingiza watu wait Hilo liko kwenye mitandao ya wahasibu na HR.
 
hapo nilipo bold umedanganya mkuu
 
kuna member humu alilalamika kuwa morogoro katimuliwa na mkuu wa wilaya kwa yeye ana 26yrs ,walimweleza wanachukua below 26 na wa morogoro tu yeye akaombe Dar es salaam ,nimeshangaa sana kumbe wana watu wao wa la saba na failure waingie, na siku hizi jeshini lazima jkt ,jeshi litakuwa na MAZUZU wengi, siku hizi vita ni TECHNOLOJIA siyo VIFARU
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…