Walioingia JKT kwa njia za panya kutimuliwa

Walioingia JKT kwa njia za panya kutimuliwa

Status
Not open for further replies.
Leo NIMEUMIA sana sana sana sana

Maumivu yangu yamechagizwa na kauli ya Mzee Mmoja mstaafu wa Jeshi yeye alistafu miaka 3 nyuma Leo tukiwa kijiweni aliamua kufumguka dhidi ya Ile habari ya viongozi wakubwa serikali kutengeneza makundi mbali mbali ya vijana wao walio waingiza kwenye Majeshi yetu mbalimbali nchini

Mstaafu anasema Jeshi LILIRO salama ni Jeshi la MAGEREZA kidogo kwa sababu haliwavutii wakubwa wengi ila Majeshi mengine mengi yameisha athilika kikubwa mnooo

Ameenda mbali zaidi akadai haya mambo yalishamili kwenye UTAWALA wa awamu ya NNE hata wanajeshi wanao hishi kwenye Kambi ya karibu na mstaafu wengi ni wanae.
Amedai ukienda usalama wa taifa uko ndo pameoza yaani Jeshi la wakuu wastaafu TU

Yaani yawezekana usinielewe hivi wewe uliwai FIKA kwa Tibaigana kijijini kwao? Unajua yule kazungukwa na askari watupu? Nenda kwa Ma IGP wastaafu, nenda kwa viongozi wakubwa huko jeshini ni balaaaaa!

Majeshi yetu yajitafakari upya kinyume chake uko mbele Kuna hatari kubwa ya wakubwa kuwa na Majeshi Yao ndani ya Jeshi la mchi
Sababu hasa ni Nini?!
 
 


Hii ni hatari kubwa sana.

Wanasiasa Waovu wanataka kujitengenezea mitandao yao ya Uhalifu kwa kuwapachika Mawakala wao wa uhalifu ndani ya Majeshi ya Ulinzi na Usalama.
Hii ni hatari kubwa sana, JWTZ/TPDF isikubali kabisa kuingia kwenye mtego huu hatari.

Mpaka Sasa, waTanzania wema karibia wote kabisa tayari wamepoteza kabisa Imani dhidi ya Jeshi la Polisi na TISS, kwa sababu hayo Majeshi Wananchi wanayona kama yanatumika vibaya sana kisiasa katika kuendesha Operesheni za kuwateka Watu na kuwapoteza. Siyo Siri hata kidogo, JWTZ/TPDF ndio Jeshi pekee ambalo Wananchi wengi sana wanaonekana kuwa bado Wana imani nalo kubwa ukilinganisha na Majeshi mengine. Hilo ndilo limebaki kuwa ndio Jeshi ambalo limebeba tumaini la mwisho kabisa la waTanzania walio wengi zaidi, wasiwavunje moyo waTanzania kwa kukubali kuvurugwa na Watawala/Wanasiasa Waovu wasiolitakia mema Taifa hili
Jeshi likatae kabisa kutumika kisiasa, badala yake Jeshi hilo lijikite kwenye UADILIFU, UZALENDO WA KWELI, HAKI, MASDILI NA NIDHAMU YA HALI YA JUU KABISA KWENYE MISINGI YA JESHI.
 
Hiyo message ya ilonda umeiona Leo? Kipindi asema jambo hili alikuwa lieutenant colonel na sasa ni colonel.
Nb.
Huko kunaitwa kujikosha. Ni unafiki mkubwa. Kama kweli Hilo ni la kweli mbona hiyo tabia haijakomeshwa mipaka Leo huko Jkt , jei Wii na hata Pi tii?
 
Kule Haiti kila kitongoji kina mmiliki wake, nawe tafuta kitongoji umiliki.

Kikinuka unakuwa humilikiwi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom