Walioingia JKT kwa njia za panya kutimuliwa

Status
Not open for further replies.
kuna member humu alilalamika kuwa morogoro katimuliwa na mkuu wa wilaya kwa yeye ana 26yrs ,walimweleza wanachukua below 26 na wa morogoro tu yeye akaombe Dar es salaam ,nimeshangaa sana kumbe wana watu wao wa la saba na failure waingie, na siku hizi jeshini lazima jkt ,jeshi litakuwa na MAZUZU wengi, siku hizi vita ni TECHNOLOJIA siyo VIFARU
Hata ukizaliwa tofauti na wilaya uliyoomba wanakuondoa..
 
Wakitumbuliwa wanajeshi mtaani hapatakalika na uhalifu unaweza kuongezeka kwa kiasi kikubwa sana
Wengine wakitumbuliwa ni haki? Hakuna aliyeoko juu ya sheria ila wapo watu walio juu ya sheria. Kumtumbua Mwalimu au Daktari mwenye vyeti feki ni sawa ila siyo sawa kwa mwanajeshi. Hii inapatikana Afrika tu
Sheria ikitungwa kwa watu wote na sheria hiyo ikianza kubagua watu hiyo inakuwa siyo sheria ni uonevu. Kama sheria inawapendelea baadhi ya watu kwanini uitunge? Ngozi nyeusi ni shida sana
 
Jeshi la Wananchi (JWTZ) limetangaza kuwachukulia hatua viongozi wa ndani na nje ya jeshi hilo na vijana waliohusika katika vitendo vya udanganyifu katika uandikishaji wa majina ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Udanganyifu huo ulihusisha ukiukaji wa taratibu na kughushi nyaraka na vyeti vilivyotumika katika uandikishaji huo.

Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda, akizungumza jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Venance Mabeyo, alisema licha ya taratibu za uombaji kuwa wazi, baadhi ya viongozi wamebainika kutumia nafasi walizonazo kupenyeza majina ya ndugu, jamaa na rafiki ili wasajiliwe.

“Napenda kuwataarifu kuwa baada ya kubaini kuwako kwa udanganyifu huu, JWTZ/ JKT tutafanya uhakiki wa vyeti na nyaraka zote husika kwa vijana walioandikishwa tutashirikiana na ofisi ya Nida (Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa), Baraza la Taifa la Mitihani, Takukuru na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuwabaini waliofanya udanganyifu,” alisema Kanali Ilonda.

Ilonda bila kutaja uhakiki huo utafanyika lini na wakati gani, alisema utahusisha kuhakiki wa vyeti, nyaraka mbalimbali zilizokuwa zikihitajika kwenye uandikishaji huo pamoja na vyeti vya kuzaliwa na vipimo vya afya.

"Kwa kuweka usawa tutafanya uhakiki huu kwa kushirikiana na JKT, Nida, Wizara ya Elimu, taasisi zinazohusika na masuala ya rushwa, vyombo vya ulinzi na usalama, ili tuweze kuwachuja, tunataka kujiridhisha je, ni Watanzania kweli, wana afya njema, wana akili timamu, ametoka eneo husika na ana sifa stahiki, wale wenye sifa watachukuliwa, hata kama idadi yao itakuwa ndogo tofauti na matarajio yetu," alisema.

Ilonda alisema wale ambao watabainika kughushi watakamatwa na kufunguliwa mashtaka.

“Hakuna atakayesalimika labda wahame nchi, aliyeghushi vyeti na nyaraka mbalimbali kiwe cha kuzaliwa au daktari aliyetoa majibu ya uongo atakamatwa, waliowashawishi kughushi watakamatwa, waliotengeneza vyeti bandia, waliohusika kuwaandikisha vijana hao bila kuwa na vigezo, viongozi wote waliohusika kupenyeza majina wa ndani na nje ya jeshi nao watachukuliwa hatua kupitia mamlaka zao husika,” alisema.

Alisema hatua zitakazochukuliwa hazitaangalia wadhifa au cheo cha mtu kwa sababu lengo ni kusafisha nchi iwe na viongozi waadilifu na wanaofuata sheria na taratibu.
nimeipenda
 
Kwa dhima tunayoelezwa kuhusu jkt hasa katika mission na vision yake ilibidi iwe wazi kwa kila mtanzania kuhudhuria hayo mafunzo.
Labda leo tungekuwa na wajasilia mali wengi na wazalendo wa kutosha.
 
Mimi naona wasifundishwe kutumia silaha hao vijana wa jkt. Wabadilishe mfumo wa mafunzo,wafundishwe ujariamali na kazi za mikono. Kama
1.Kilimo na ufugaji wa kisasa
2.Ufundi wa aina zote
3.Michezo na Sanaa
4.Mengineyo
Nadhani hili litasaidia sio waje kukaa mtaani.
 
Hahaha unakuta yeye anaongea kwa ukali, kumbe naye aliingizwa kwa njia hizohizo anazozikataa. Waswahili wanasema mwizi akiibiwa husikitika utadhani kafiwa.
Vyeti havina maana yoyote huko JKT, who cares kama umefoji au la?! Vijana wote JKT ni walinzi/security guard sasa uhakiki vyeti ili iweje?! Chuku unaowapenda usiowahitaji waache wataendelea kuwa security guard tu.
 
Mimi naona wasifundishwe kutumia silaha hao vijana wa jkt. Wabadilishe mfumo wa mafunzo,wafundishwe ujariamali na kazi za mikono. Kama
1.Kilimo na ufugaji wa kisasa
2.Ufundi wa aina zote
3.Michezo na Sanaa
4.Mengineyo
Nadhani hili litasaidia sio waje kukaa mtaani.
Hahaha hivi vyote havihitaji kufundishwa, wawaache watoto wakae majumbani mwao.Mnawapa hope msiyoweza kuitekeleza.
Mi nililima sana, lakini sikuhitaji jkt kufahamu kulima.
 
Sizungumzii hao wanafunzi mayai. Nazungumzia wale wanaomba kwa ajili ya kuajiriwa.
 
Kama wanasifa ila wamepitishwa kwa upendeleo je?
 
Leo NIMEUMIA sana sana sana sana

Maumivu yangu yamechagizwa na kauli ya Mzee Mmoja mstaafu wa Jeshi yeye alistafu miaka 3 nyuma Leo tukiwa kijiweni aliamua kufumguka dhidi ya Ile habari ya viongozi wakubwa serikali kutengeneza makundi mbali mbali ya vijana wao walio waingiza kwenye Majeshi yetu mbalimbali nchini

Mstaafu anasema Jeshi LILIRO salama ni Jeshi la MAGEREZA kidogo kwa sababu haliwavutii wakubwa wengi ila Majeshi mengine mengi yameisha athilika kikubwa mnooo

Ameenda mbali zaidi akadai haya mambo yalishamili kwenye UTAWALA wa awamu ya NNE hata wanajeshi wanao hishi kwenye Kambi ya karibu na mstaafu wengi ni wanae.
Amedai ukienda usalama wa taifa uko ndo pameoza yaani Jeshi la wakuu wastaafu TU

Yaani yawezekana usinielewe hivi wewe uliwai FIKA kwa Tibaigana kijijini kwao? Unajua yule kazungukwa na askari watupu? Nenda kwa Ma IGP wastaafu, nenda kwa viongozi wakubwa huko jeshini ni balaaaaa!

Majeshi yetu yajitafakari upya kinyume chake uko mbele Kuna hatari kubwa ya wakubwa kuwa na Majeshi Yao ndani ya Jeshi la mchi
 
Limechelewa kutoka wapi na wapi linakwenda ili tujustfy ujumbe wako
 
Sawasawa. Katiba mpya muhimu
 
akili za kuambiwa changanya na zako gentleman, otherwise utabebwa ufala kifikra na kupotoshwa kilofa sana aise kuhusu mambo haya 🐒
 
Leo NIMEUMIA sana sana sana sana

Maumivu yangu yamechagizwa na kauli ya Mzee Mmoja mstaafu wa Jeshi yeye alistafu miaka 3 nyuma Leo tukiwa kijiweni aliamua kufumguka dhidi ya Ile habari ya viongozi wakubwa serikali kutengeneza makundi mbali mbali ya vijana wao walio waingiza kwenye Majeshi yetu mbalimbali nchini

Mstaafu anasema Jeshi LILIRO salama ni Jeshi la MAGEREZA kidogo kwa sababu haliwavutii wakubwa wengi ila Majeshi mengine mengi yameisha athilika kikubwa mnooo

Ameenda mbali zaidi akadai haya mambo yalishamili kwenye UTAWALA wa awamu ya NNE hata wanajeshi wanao hishi kwenye Kambi ya karibu na mstaafu wengi ni wanae.
Amedai ukienda usalama wa taifa uko ndo pameoza yaani Jeshi la wakuu wastaafu TU

Yaani yawezekana usinielewe hivi wewe uliwai FIKA kwa Tibaigana kijijini kwao? Unajua yule kazungukwa na askari watupu? Nenda kwa Ma IGP wastaafu, nenda kwa viongozi wakubwa huko jeshini ni balaaaaa!

Majeshi yetu yajitafakari upya kinyume chake uko mbele Kuna hatari kubwa ya wakubwa kuwa na Majeshi Yao ndani ya Jeshi la mchi

View: https://www.facebook.com/share/v/1CAB7u9QYe/
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom