The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,242
- 45,930
Shukrani mkuu kwa ushauri wako, mimi pia nina project yangu japo imesimama kidogo, kwa ushauri huu nimepata nguvu na hamasa ya kujivuta taratibu.
Narudia tena, usikate tamaa wala kuona unachelewa.
Hizo picha zisikutishe, mambo hayakwenda haraka kama zinavyoonekana.
Baada ya kufunga mkanda wa chini, nilikaa mda mrefu tu inakaribia miezi nane.
Nilipoinua boma kufunga linter na ile mistari mitatu ya juu napo nikapitea hapo ni miaka 2. Nikaja kurudi kwa kasi hadi kuhamia sasa.
Usivunjike moyo kabisa.