Imetulia hii
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Imetulia hii
Hii mpaka kupaua ni tofali ngapi?Imetulia hii
Yaani ni very simple hata nyumba yangu iko hivi hivi, ina 3 wings, kushoto vyumba viwili na public toilet,katikati living area na kitchen,kulia tena masterbedroom peke yake.Ndio maana Master bed room nimeiweka mbali sana na vyumba vingine. Hata maongezi ya huko hayatakiwi kabisa yavuke mipaka kwa namna yeyote. Ukitoka vyombani unakutana na sebule na dining kukitafuta chumba chetu.
Katika ubora wakoHii mpaka kupaua ni tofali ngapi?
Mwaka huu najenga bwana hapa nilishapata ramani. Hii ukikaribisha mrembo ndani mbona lazima akupe mbususu kama sio kuhamia kabisaKatika ubora wako
Ndio uliyumia million ngapi mpaka kupaua?Yaani ni very simple hata nyumba yangu iko hivi hivi, ina 3 wings, kushoto vyumba viwili na public toilet,katikati living area na kitchen,kulia tena masterbedroom peke yake.
Hii mzee tofali 5000 sii tayari boma kwwisha?Yaani ni very simple hata nyumba yangu iko hivi hivi, ina 3 wings, kushoto vyumba viwili na public toilet,katikati living area na kitchen,kulia tena masterbedroom peke yake.
Soma polepole
Upande wa master bedroom nimeweka private room.
ukishajibiwa unasema hiyo hela si bora ukale mbususu 😂😂😂😂Hii mpaka kupaua ni tofali ngapi?
🤣🤣🤣🤣 Hapa kikwazo ilikuwa ramani nilishaipata sasa namtafuta jamaaa na mafundi wake waje wanijenge. Niwe nawakaribisha warembo wa jf tuwe tunapeana utamu mjengoniukishajibiwa unasema hiyo hela si bora ukale mbususu 😂😂😂😂
Hiyo nyumba kwa hizo kuta nyingi namna hii si ilikula Tofali laki hii ??
Hiyo nyumba kwa hizo kuta nyingi namna hii si ilikula Tofali laki hii ??
Mkuu ulitumia msingi wa mawe ?Hazikwenda nyingi, ni ndefu kwenda juu na fundi alinikomalia nijengee inchi 6 badala ya 5. Ziliteketea kama 3000.
Mkuu ulitumia msingi wa mawe ?
Dah hongera sana mkuu nyumba kubwa sana halafu ina ramani poa sana.Hapana kiongozi. Hizo ni za kuinulia tu. Za msingi ziliondoka kama 2000.
View attachment 2077217
View attachment 2077219
View attachment 2077220
View attachment 2077223
View attachment 2077225
View attachment 2077226
View attachment 2077227
View attachment 2077228
View attachment 2077229
View attachment 2077230
Kwa uchache, safari ilikua hivyo mkuu.
Likewise1 master room, 2 bed rooms, Kitchen, dining, sebule, public toilet! Location mbezi dsm nmeanza oktoba 2021 hadi hapo 10m imekata. View attachment 2037971
Hapo umejitahid sana mkuu, Mimi pamoja na kwamba niko stage moja na wewe na kwa kiasi kilekile, nilikuwa na tofali standby 3000 tangu 2019 na nilikuwa na kokoto trip moja, nimeongeza tofali 1500 tu na vingine tuko sawa, hongera ndugu...tuombe Mungu mama atupie jicho na huku hali ni mbaya sana, tunapambana mno ila bei za vifaa haziingiliki.Ndio nmejenga na shimo la choo tena kwa tofali zile za round nmenunua moja 1200 na ni included kwenye hyo hyo 10m.
Dah hongera sana mkuu nyumba kubwa sana halafu ina ramani poa sana.
Hongera sana ndugu.
Shukrani mkuu kwa ushauri wako, mimi pia nina project yangu japo imesimama kidogo, kwa ushauri huu nimepata nguvu na hamasa ya kujivuta taratibu.Ahsante mkuu. Lakini kamwe usitishwe na maneno ya watu wala usitake kwenda kwa mwendo wa watu wengine.
Furahia kila hatua unayopiga kwenye maisha, hata ikiwa wengine wanaona hausogei au mwendo wako wa taratibu, hakikisha haukatishwi tamaa.
Nilichojifunza.
1. Fundi anakuvuta kadri awezavyo uingie king, ukishaingia lazima kazi imalizike. Namaanisha atakupa makadirio madogo na kuna baadhi ya vitu hatakwambia awali ili upate moyo wa kuanza. Hapo ndio utakapoanza kupewa bill ndogo ndogo na hauwezi kuishia njiani.
Msisitizo, pitia mara mbili mbili na uliza maswali ya kutosha ukishapewa makadirio. Pia tafuta wengine wawili ili ulinganishe gharama na makadirio.
2. Sio lazima fundi unaeanza nae umalize nae. Wengine akishaona amekamata mradi anajua ndio pa kukupiga na anafikiri unapesa za mchezo. Mie msingi alijenga mwingine. Boma akapandisha mwingine. Finishing wengine, kuezeka wengine. Kuweka dari wengine kabisa. Hata hawahusiani.
3. Simamia manunuzi ya vifaa mwenyewe. Fundi akikupeleka sehem kununua vitu usijekufikiria uwe makini, kuna mmoja alikua anaenda kuongea na jamaa kabla sijaenda ili nipigwe bei kisha cha juu achukue yeye. Uzuri nilikua na mahusiano mazuri na mwenye duka, akanishtua, nilimfukuza kabla hajamaliza msingi na tulimalizia na kibarua wake.
Huyo alinipiga kwenye tofali.
Mwingine akanipiga kwenye mbao. Huyo nae nikafukuzilia mbali. Kwanza alinipa running meter utafikiri naenda kuezeka shule, mie nikipiga hesabu, napata 380, yeye ananiambia 620 kibarua kikaota nyasi.
Hauwezi kukwepa kabisa kupigwa ila unaweza kupunguza maumivu.