Waliojenga mwaka 2021 tunaomba uzoefu wenu

Ndio maana Master bed room nimeiweka mbali sana na vyumba vingine. Hata maongezi ya huko hayatakiwi kabisa yavuke mipaka kwa namna yeyote. Ukitoka vyombani unakutana na sebule na dining kukitafuta chumba chetu.
Yaani ni very simple hata nyumba yangu iko hivi hivi, ina 3 wings, kushoto vyumba viwili na public toilet,katikati living area na kitchen,kulia tena masterbedroom peke yake.
 
ukishajibiwa unasema hiyo hela si bora ukale mbususu 😂😂😂😂
🤣🤣🤣🤣 Hapa kikwazo ilikuwa ramani nilishaipata sasa namtafuta jamaaa na mafundi wake waje wanijenge. Niwe nawakaribisha warembo wa jf tuwe tunapeana utamu mjengoni
 
Mkuu ulitumia msingi wa mawe ?

Hapana kiongozi. Hizo ni za kuinulia tu. Za msingi ziliondoka kama 2000.

IMG_20220111_174304_253.jpg

IMG_20220111_174231_586.jpg

IMG_20220111_174140_713.jpg

IMG_20220111_173805_014.jpg

IMG_20220111_173742_827.jpg

IMG_20220111_173945_462.jpg

IMG_20220111_174117_844.jpg

IMG_20220111_173827_967.jpg

IMG_20220111_174035_086.jpg

IMG_20220111_173711_497.jpg

Kwa uchache, safari ilikua hivyo mkuu.
 
Ndio nmejenga na shimo la choo tena kwa tofali zile za round nmenunua moja 1200 na ni included kwenye hyo hyo 10m.
Hapo umejitahid sana mkuu, Mimi pamoja na kwamba niko stage moja na wewe na kwa kiasi kilekile, nilikuwa na tofali standby 3000 tangu 2019 na nilikuwa na kokoto trip moja, nimeongeza tofali 1500 tu na vingine tuko sawa, hongera ndugu...tuombe Mungu mama atupie jicho na huku hali ni mbaya sana, tunapambana mno ila bei za vifaa haziingiliki.
 
Dah hongera sana mkuu nyumba kubwa sana halafu ina ramani poa sana.

Ahsante mkuu. Lakini kamwe usitishwe na maneno ya watu wala usitake kwenda kwa mwendo wa watu wengine.

Furahia kila hatua unayopiga kwenye maisha, hata ikiwa wengine wanaona hausogei au mwendo wako wa taratibu, hakikisha haukatishwi tamaa.

Nilichojifunza.

1. Fundi anakuvuta kadri awezavyo uingie king, ukishaingia lazima kazi imalizike. Namaanisha atakupa makadirio madogo na kuna baadhi ya vitu hatakwambia awali ili upate moyo wa kuanza. Hapo ndio utakapoanza kupewa bill ndogo ndogo na hauwezi kuishia njiani.

Msisitizo, pitia mara mbili mbili na uliza maswali ya kutosha ukishapewa makadirio. Pia tafuta wengine wawili ili ulinganishe gharama na makadirio.

2. Sio lazima fundi unaeanza nae umalize nae. Wengine akishaona amekamata mradi anajua ndio pa kukupiga na anafikiri unapesa za mchezo. Mie msingi alijenga mwingine. Boma akapandisha mwingine. Finishing wengine, kuezeka wengine. Kuweka dari wengine kabisa. Hata hawahusiani.

3. Simamia manunuzi ya vifaa mwenyewe. Fundi akikupeleka sehem kununua vitu usijekufikiria uwe makini, kuna mmoja alikua anaenda kuongea na jamaa kabla sijaenda ili nipigwe bei kisha cha juu achukue yeye. Uzuri nilikua na mahusiano mazuri na mwenye duka, akanishtua, nilimfukuza kabla hajamaliza msingi na tulimalizia na kibarua wake.
Huyo alinipiga kwenye tofali.

Mwingine akanipiga kwenye mbao. Huyo nae nikafukuzilia mbali. Kwanza alinipa running meter utafikiri naenda kuezeka shule, mie nikipiga hesabu, napata 380, yeye ananiambia 620 kibarua kikaota nyasi.

Hauwezi kukwepa kabisa kupigwa ila unaweza kupunguza maumivu.
 
Shukrani mkuu kwa ushauri wako, mimi pia nina project yangu japo imesimama kidogo, kwa ushauri huu nimepata nguvu na hamasa ya kujivuta taratibu.
 
Back
Top Bottom