Waliojenga mwaka 2021 tunaomba uzoefu wenu

Reasonable lakini, Hongera sana Mkuu

Ahsante mkuu. Hapo sijaweka top za milango. Yaani mafundi inatakiwa wakikwambia hakuna vitu flani wasubirishe kwanza akili itulie. Ukiwa unatoa tu utapelekeshwa sana.

Msingi uliondoka na pesa ndefu kutokana na ule udongo kuwa wa mfinyanzi. Unakata nyumba sana usipoweka imara.

Ndiomaana baada ya mchanga, nilitandaza nondo tatu chini ndio tofali zikaanza. Hizo zote hazikua na ulazima ukizingatia mkanda wa baada ya tofali za kulala na wenyewe ulikua wa nondo nne tena una umeshiba.

Sasa unaweza kuona jinsi gani ufujaji ulifanyika. Kitu sijilaumu ni bati za Alaf, hazijapauka rangi.
 
Nakuelewa mkuu,
Niliboreha kidogo hii ramani nikaitumia, around 100m zimekatika
 
Ha ha HA Kazi unayo
Hapa naamini nikiingia mwenyewe site nipo benet na mafundi m60 nahamia japo chumba cha master jiko na sebule vitakuwa kamili. Vyengine taratibu mkuu sina haraka yoyote muhimu nilishapata sehemu ya kuwagegeda warembo.
 
Asante Mkuu kwa Ufafanuzi
 
Me nimeanza Sept. Nipo msingi napambana January niinue Boma kama hivyo inafanana requirements kama yako
Pambana msingi kwa ramani hiyo bila shaka ulikula milioni nne na gharama za ufundi boma andaa milioni sita unasimamisha…

Kimbembe kinaanza kwenye bati na finishing za ndani wacha kabisa..
 
Hii m100 kweli nakubali ...ila vyumba vingi mzeya vipi babu na bibi wanachumba chao pia?

Swali moja mkuu hizo corridor mbona kama zitakuwa na giza sana
Ni kweli mwanga sio mkubwa sana ikabidi rangi ya ndani iwe light, so sio giza sana!
 
Pambana msingi kwa ramani hiyo bila shaka ulikula milioni nne na gharama za ufundi boma andaa milioni sita unasimamisha…

Kimbembe kinaanza kwenye bati na finishing za ndani wacha kabisa..
Mkuu hii comment sikuisoma but ume hit kwenye uhalisia nimeanza ujenzi wa boma jumatatu hii ina approach hiyo 6 msingi ulitwanga 4

Kama una uzoefu nipe approximate mpaka namaliza itanigharimu ngapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…