Waliojenga nyumba hupenda kuwaogopesha wengine kuwa ujenzi ni gharama!

Hiyo ni gharama ya msingi na ukuta tu mkuu
Mbona mnatisha sana watu? Suala la ujenzi kama baadhi ya wadau walivyoeleza huko juu inategemea na wewe mwenyewe. Haiwezekani wewe mwendesha bodaboda unataka ujenge nyumba sawa na ya muuza ganda! Milioni ishirini inatosha kabisa kama unataka kujenga nyumba ya thamani hiyo. Ukitaka ukusanye milioni 200 ndipo ujenge nyumba utaumia bure na si ajabu usijenge nyumba kabisa maishani mwako! Kwa mfano, ukiwa na kiwanja unaweza kujenga nyumba kwa staili hii: Kila weekend ikikukuta una laki moja mfukoni usiende bar wala kokote kwenye starehe; badala yake nenda na hiyo laki site ikafanye kazi...
 
Wapi huko kiongozi kiwanja Laki 9?
 

Sawa mkuu ,ila 16 mil bado ni ndogo at least 25 mil kama ni nyumba ndogo .
 
Sawa mkuu ,ila 16 mil bado ni ndogo at least 25 mil kama ni nyumba ndogo .
Nyumba ndogo kwa maana gani, maana hata mtu mwenye nyumba ya sebule katikati, upande mmoja chumba na upande mwingine chumba,yuko kwenye nyumba yake na ana enjoy! Tunachojadili hapa ni kwamba hakuna kiasi cha fedha ambacho ni maalum kwa watu wote kwamba ndicho kinatosha kujenga nyumba. Kuna mtu amwomba Mungu apate milioni tano tu aondoke kwenye nyumba ya kupanga. Anajua atapata kiwanja cha milioni moja, tena huko huko kwenu Dar, na atashusha slope yake yenye chumba chake na mkewe pamoja na chumba kimoja cha watoto na choo cha nje!
 
Mkuu ni kweli kbs .
 
Ukiomba gharama za makadirio ya ujenzi eleza vizuri unachokitaka. Wengi wanasema nataka kujenga nyumba ya "kawaida" labda ya vyumba vitatu. Hilo neno kawaida linatofautiana kwa mtu na mtu. We sema nataka kujenga kwa kutumia vifaa vya bei ya chini kabisa, na finishing nitafanya hadi kufikia kiwango flani. Usitumie neno kawaida. kila kifaa unachokijua cha ujenzi kina grade tofauti. Hata tofali lipo la inchi tano na sita na zinatofautiana bei. Cement pia zipo grade mbili, nondo saizi tofauti tofauti. Mtu akikutajia gharama zake amini tu, ila si lazima na wewe ujenge kwa gharama hizo ukitumia vifaa vya quality ya chini. Hata kwa nyumba zinazolingana ukubwa na ramani, moja inaweza ikawa bei mara mbili ya mwenzake. Ukipandisha sana msingi, unakula material nyingi ikiwemo na vifusi...yaani mambo ni mengi kweli kwenye ujenzi wala siwezi kueleza yote hapa. Choo tu cha kukaa vipo kuanzia 150,000 hadi milioni, ila kwa jicho la asiejua hawezi kutofautisha. Kwa hiyo usione umetishwa, makadirio ya ujenzi hauna wastani kwa nyumba zote....we kaza buti mdogo mdogo na wewe ujenge kwa nafasi yako
 
Unachosema kweli kaka....Ujenzi sio lele mama. Watu wanataka kupewa moyo kwamba ujenzi ni rahisi. Sio rahisi hata kidogo. Itabidi mtu ujibane haswa. Kila mtu naamini anaweza kujenga nyumba kulingana na nafasi yake...hata vyumba viwili ni nyumba pia. Tofauti ni kwenye ubora tu, hapo lazima tofauti ionekane. Lakini hakuna mtu anapaswa kuogopa kujenga ila hakikisha unajenga nyumba inayoendana na uwezo wako...usitake kulinganisha kabisa.
 
80% ya waliochangia hawajawahi kujenga wala kusimamia ujenzi.
 
Nimemaliza kupaua last week, ila hadi sasa imeshanicost 22M, NAVUTA PUMZI NIANZE MCHAKATO WA FINISHING, NADHANI MPAKA NAMALIZA ITAKUWA IMENICOST NOT LESS THAN 35M
 
Nimemaliza kupaua last week, ila hadi sasa imeshanicost 22M, NAVUTA PUMZI NIANZE MCHAKATO WA FINISHING, NADHANI MPAKA NAMALIZA ITAKUWA IMENICOST NOT LESS THAN 35M

Asante mkuu lkn sijui ni aina gn ya nyumba,materials ulizotumia,umewalipa mafundi kiasi gani,decorations ulizofanya na utakazofanya..,thats all..gharama za nyumba yako zitadepend upon hivyo vitu na vingine vingi.
 
Asante mkuu lkn sijui ni aina gn ya nyumba,materials ulizotumia,umewalipa mafundi kiasi gani,decorations ulizofanya na utakazofanya..,thats all..gharama za nyumba yako zitadepend upon hivyo vitu na vingine vingi.
Naweza kushare na watu excell template ya cost and expenditure maana kila kitu nimekuwa narekodi, atakayetaka just pm me
 
Kweli aise
 
Hakika mkuu watu nuksi
 
Kwa iyo tusio na nyumba tusijenge sabab ni gharama kubwa mkuu?
Mim najenga nyumba ya vyumba viwil sebule sitting room dining pamoja na jiko nimefikia hatua ya KUEZEKA ila bado sijazidi milioni kumi na tano na Mbao nshanunua pamoja na bati sitegemei nyumba izid m25 sasa izo gharama kubwa zipo wapi wasiwatishe bana wewe anza kujenga sema usiwe na haraka sana maana nyumba unakua unazika pesa waweza jikuta unadownfall bila hata kumaliza ujenzi unabaki kuona pagale tu bila kujua hatima ya hilo pagale
 
Bora mkuu dah maana naisigi wanataka wawe na nyumba wenyewe tu[emoji2]
 
Endelea kujifariji kwa vimahesabu vyako vya kwenye computer,
Kwann usianze kujenga kisha ukawa unatupa update ya hali ya ujenzi inavyoendekea kulko kutuandikia mambo ya kufikirika..

Mimi nina nyumba na siezi kukufariji kuwa ujenzi, ni, bei chee wakati kiukweli ni mziki..
Mi, nnavyoona we lengo lako ni kujenga kibanda na sio nyumba, kama unajenga ili mradi uambiwe unajenga basi sawa ila tambua kuwa nyumba standard ni gharama hasa hapa mjini, Bongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…