Habari za muda huu wadau.
Kuna habari nimeona mitandaoni ikanifikirisha kidogo nikaona niilete jukwaani tupate mitazamo ya wengine.
Ni kwamba Inasemekana ya kwamba watu wote waliokunywa kikombe cha dawa kwa babu wa Loliondo wote kwa sasa wamefariki dunia ikiwa pamoja na babu mwenyewe!
Mimi kwa upande wangu watu ninaokumbuka kuwa walikunywa kikombe hicho na ambao wote wamefariki dunia ni
1️⃣ Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam marehemu Abbaas Kandoro.
2️⃣ Mwanasiasa wa upinzanzani Augustine Mrema na babu mwenyewe
3️⃣ Ambilikile Mwasapila.
4️⃣ Kuna mwanasiasa mwingine kule mkoani Geita wilaya fulani hivi ila naogopa kumtaja na WOTE HAO HATUNAO TENA.
Je wewe unamjua mtu aliyekunywa kikombe cha babu ambaye hajazikwa hadi sasa?