Waliokuwa na bidii na elimu lakini wapo mtaani wanadharaulika kwakuwa jamii iliweka matarajio makubwa

Samahani mkuu, unaongelea sayansi hii hii inayofundishwa kwenye shule za hapa Tanzania?
 
Kuna Degree za science hazina issue, Degree zenye issue za science night Udaktari, pharmacy, nursing,lab tech,
What the hell yo talkin about? Aircrafts na automobile eng's unaziachaje sasa? Yo ain't serious
 
ona kilaza huyu za sayansi zipo nyingi ndo maana wapo mtaani na hao sayansi wanapangiwa mpaka mishahara na arts
 
kaangalie ellon musk je kasoma engineering hunaunalojua. ni kwamba miaka fulani utakuja soma formular za umeme ambazo kagundua yeye na hajawai kusoma yaani sayansi unasoma maono ya watu na wanasayansi wengi ndo wanaongoza kukariri kama wasomi wa history tu

maisha ni kuendeleza vipaji ndo nchi kubwa zinafanya na uvumbuzi

hesabu unazosoma na physics hazikuletei uvumbuzi sababu ni uvumbuzi ulishafanyika na most of it is technology already existed

unasoma hesabu unakuja fundisha hesabu zile zile labda shule za tech
 
Mleta mada unachotakiwa kufahamu hapa bongo elimu tunayoipata wote wa science na arts haina ukombozi kwetu ,tunakarirshwa na tusipo pata ofisi ndoo imetoka hiyo.Mm ni mwlm najua tunavyowafundisha wanafunzi Mungu ndie anaejua.
 
Bravoo. Big up broo. Tukirudi mitaani hakuna degree ambayo ni better than nyingine kwenye swala la utafutaji, Ila akili yako ya maisha tu ndo itakuweka mtaani na itafanya uendelee kuishi.
M nimemaliza degree yangu hapo UDSM, bachelor of arts with education (history and geography). Nikaingia kitaa kuanza kupiga mishe. Lkn Sasa Mambo sio mabaya Sanaa.
Chamuhimu tukomae tu, m namshangaa mtu alie comment humu, cjui degree ya sayansi ni Bora kuliiko ya art, au Sheria, au uhasibu.
Muhimu piga mishe mtaani tengeneza life lako maisha yasonge.
Mungu kasaidia Nina ka-kampuni kadogo wafanyakazi 4, kausafiri na machine kubwa ya kazi. Naishi kwa mishe za drilling and blasting. Na supply mawe ya kujengea na kokoto napiga udalali tu kwa hao mainjinia.
Tuje Sasa. Kwa huyo wa kutukuza degree za sayansi halafu anadai za art zifutwe.
Nilienda kublast jiwe sehemu injinia kanipa hyo kazi.
Cha ajabu mm nimechukua ujuzi mtaani Nina experience kubwa ya kuhimili, kusuka na kutambua milipuko kuliko yeye wa darasani, nikatambua kua Vitu vinabadilika kila siku yeye kakariri alivyosomea darasani. Kumbe mm nakutana na milipuko mipya kila siku.
Injinia wa ujenzi mmoja alikadiria mawe ya kujengea bwawa kwa hizo cubic metre zake. Nikawambia hazitoshi coz mawe ni shapeless, na Yana tofautiana Sana ukubwa, tofauti na kokoto au mchanga. Akabisha kuja kusapply mahesabu yake yakayumba ikabidi niongeze mawe mengi zaidi ili yatoshe.
Nilijua tu yeye kaingia na hesabu za darasani Yuko sahihi lkn mm ndo mishe zangu hizo na supply mawe kwa mainjinia wengi ko hata kwa macho tu najua hapa atahitaji cubic metre nga za mawe. So experience ninayo kubwa kuliko yeye kwa sababu mm ni supplier na naenda site nyingi zaidi kuliko yeye.

Chamuhimu tuishi tu nothing is perfect na tunaishi kwa kutegemeana.
 
Labda hujanielewa mkuu, sina wivu, m wivu wa Nini Sasa hapo darasani nimepiata. Kila mtu anasomea kitu anachokipenda. Ndio maana Kuna taaluma nyingi za kusomea.
Nimemjibu huyo aliesema kua masomo ya art c kitu. Kwamba sisi tuliosomea art degree hakuna tulichofanya Tena ukiangalia na Sasa soko la ajira haituoi favor.
Wala cjazungumzia uwezo wangu wa kifedha Wala madaraka, Wala cjasema nimemzidi Nini. Ila nilikua natoa tu ukweli kua iwe umesoma art au science bado hakukufanyi uonekane uko better zaidi ya wenzio.
Hiyo nimemjibu mtu fuatilia toka mwanzo mtiririko wa message.

Cha kwanza nimempongeza brother engineer ambae alianzisha mradi wa kuku, yaan tofauti Ana alichosomea na maisha yanaenda. Then nimejilinganisha na mm ambae nimesomea ualimu wa masomo ya arts. Lkn nafanya kazi za mainjinia.
Yaan nikimaanisha maisha hayana formula Ila yanatuhitaji tupambane ili tuendelee kuishi.
Cjajitukuza kau nimemzidi hela Wala kupasua mawe nimeonesha experience za maisha na elimu ya darasani, mda mwengine experience ya kazi maishani inazidi kile ulichokioitia darasani. Kuna mda experience inahitajika zaidi.
Nilichomaanisha ni kua ninaujuzi wa kutumia milipuko vzr, ambao tulipoenda field na engineer mm nilitegemea yeye ndio ataniongiza coz ni kazi yake na kaisome lkn lilipokuja suala la kazi yenyewe mm ndo nikawa tegemeo na yeye mwenyewe alikiri. Sikumdharau Ila nikatambua kua Nina experience kubwa kuliko yeye.
Huyo mwingine alinibishia nilipomwambia ulichokadiria hakiatatosha lkn tulipokuja kuvifanya kazi mm nikawa sahihi kuliko yeye Sasa yeye kasomea, mm sijasomea civil engineering lkn Nina experience ya kile kidogo ninacho kifanya.
Na nimetoa hitimisho kua tukiachana na elimu ya darasani ambayo watu wanajitukuza nayo , tunatakiwa kuishi na maisha yaendelee. Usimdharau mtu kisa we umesoma art au science Misha ni zaidi ya elimu ya kawaida.
Nb: alienifundisha kuhusu milipuko alikua ni jmaa tu darasa lasaba lkn kaajiriwa kwenye kampuni kubwa ya mchina Ila baadae nilipata shirt course ya darasani. Nikapewa leseni.
Tunaishi kwa kutegemeana, hakuna aliye zaidi ya mwenzie kila mtu anaishi kwa maono na matakwa yake.
 
Kipanga anakuwaje na maisha mabovu, labda kama kuna bahati mbaya kama kuugua ilimtokea huko njiani......vipanga mara nyingi ndo wanabaki kuelimisha vyuo vikuu hadi wanakuwa madaktari na maprofessa, zaidi wanakuwa kwenye academics au kazi nyingine za kuajiriwa........fursa zao zipo wazi sana ukilinganisha na vilaza ambao mara nyingi wanategemea connection, wakati kipanga uwezo wake unamuuza......
 
Sasa c unakuta sio wote wanaobahatika kuajiriwa
 
Kukariri ndiyo msingi wa kuelewa. Nina maana huewezi kuelewa bila kukaririii
 
Percent ya kukariri ni ndogo huwezi linganisha na mtu aliyesoma digriii ya history au sheria au administration au uhasibu nk
Sehemu kubwa lazima uelewe kwenye digriii ya udaktari
Uhasibu nao kuna kukariri?
 
Mkuu mtu ambaye ni kichwa hawezi kukosa fursa, labda kama kuna mambo ya miziziology.......
Yes hawezi kukosa fursa hapo nakubali, issue ni kwamba tunategemea kwenye kuajiriwa tu.
 
Hivi ni ipi maana halisi ya mafanikio au kufanikiwa maishani..?
Nafikiri mafanikio au kufanikiwa maishani kupo katika maana nyingi. Na hutofautiana na malengo au maono ya mtu, Hali ya kitamaduni na kijamii, kidini, kisiasa kiuchumi n.k. hivyo inategemea ww au mtu anatafsiri katika nyanja ipi.
Mfano. Kidini au kiimani tunaamini mafanikikio ni kumfuata Imani au kishika dini kikamilifu, kumfuata yesu, au kuokoka kwa wakristo, Kufuata matendo ya mtume na Kufuata nguzo za uisilamu kwa waisilamu( Sina uhakika kwasababu mm sio muislamu) vivyo hivo na kwa Imani zingine Kama Taoism, Buddhism,n.k.
"Hakuna mafanikio maishani zaidi ya kishika dini na Sheria zake. Huyo ndio mtu aliyefanikiwa zaidi" ndivyo viongozi wetu wa dini hutuambia Hawa hawaangilii Sana kiuchumi na kijamii na kisiasa.

Mafanikio ya kiuchumi, sasa hapa ndio wengi tume base, (hata mm pia) na hii ni kwasababu tunaishi katika ulimwengu wa nguvu ya fedha hasa. (Capitalist system). Wengi tunaamini mafanikio no kua na pesa nyingi zaidi. Au kua na vyanzo vya mapato vya kiuchumi vingi.
Kijamii, ni vile jamii husuka inatafsiri mafanikio ni Nini. Mfano jamii za wafugaji mafanikio kwao ni kua mifugo mingi zaidi. Aliyekua na mifugo mingi ndie aliyefanikiwa zaidi. Jamii za wakulima Alie na mashamba au ardhi kubwa ya kulima na kutoa mavuno mengi ndie aliyefanikiwa zaidi ya wengine. Vivyo na jamii zingine zinatofautisha mafanikio kwa vile wao huona labda kua na nyumba au mahala pa kuishi, kua na kazi fulani pia. Kuoa au kuolewa. Hawa hawangalii dini au pesa huangalia zaidi Mambo ya kijamii. Mfano ukiwa mamilioni ya pesa halafu hujaoa wanakuona muhuni tu Wala hujafanikiwa. Au una pesa nyingi lkn huna nyumba wanakuona hujafanikiwa, au unapenda nyingi lkn wanaona huba furaha wataona huna mafanikio. Au umeshika dini lkn huna nyumba ya kuishi bado watakuona ww huna mafanikio.

Kwa maoni yangu mafanikio ni vile wewe utakavyo yatafsiri katika maisha yako mwenyewe.
 
Duuuhh Nafikiri ww ndo unamatatizo mkuu kwa kutoa assumption kwenye maisha ya watu wengine. Sijawahi kua bulled kwa kusoma arts. Na Wala sijawahi kuipenda science tokea nasoma secondary.
Na Wala sijawahi kua na inferiority kma unavyodai na sitakua nayo kwa sababu nakuamini katika maisha yangu ya utafutaji. Ualimu ni taaluma niliyoipenda tokea moyoni.

Ninacho kieleza mm na ww vitu viwili tofauti. Hicho inabidi uelewe. Nimeeleza kua huwezi kudharau taaluma ya mtu. Sasa sijajua ww unaeleza Nini.
 
Ila bwana inategemea unasoma kitu gani? Kuna dogo kasoma marine huko kamaliza novemba, februari kala shavu huko umangani. Pesa aliyokusanya miye nikichukua mkopo nalipa miaka mitatu au mitano.
Mkuu sio kwa ubaya, naomba nije PM. Namimi nimesoma mambo ya Marine, na natafuta michongo majuu, kama utaniunganisha na "mwana" ili anipe ABC's
 
Mkuu Sky Eclat naomba leo nikupige msasa kidogo.... (sio kwa ubaya)

Neno uzamili usilitumie pale unapotaka kuwa specific kumaanisha masters.

Masters ni umahiri.
PhD ni uzamivu
"Postgraduate", collective term ya masters, PhD n.k ndio kwa kiswahili inaitwa uzamili.

Bila shaka hautachukia.
 
Watu wanajua sayansi hakuna kukariri hahahahah. Kuanzia Engineering hadi u daktari ni kukariri mwanzo mwisho.......sema tu ni kukariri wenye nafuu
Wanaobishana ni wale waliokariri wakahisi wameelewa.

Mfumo wa elimu ya kibongo ni kukaririshwa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…