Waliomfitini Dr Mwele kwa Magufuli, wanajisikiaje?

Waliomfitini Dr Mwele kwa Magufuli, wanajisikiaje?

Pale Dr. Mwele hakutangaza outbreak ya Zika. Alikuwa anaelezea matokeo ya tafiti zilizofanyika. Moja ikihusisha watoto wenye mwonekano kama wale wa wazazi waliopata Zika kule Brazil.

Na matokeo yalikuwa chanya, yakiwa yamefanywa kwa PCR machine. Hii ilionyesha kuwa nasi hatujajitenga na haya matatizo kwani karibu nasi kuna nchi ambazo zilikwishapata Zika (mipaka yetu haina makomeo ya ugonjwa).

Uongozi wa juu ukapaniki, kwani haya ni mambo ya science, Zika ni lifelong/matatizo na uwepo wake unaweza kutambuliwa hata ndani ya miaka yote ya maisha yako. Hivyo, mtu akipata unaweza kupata ushahidi wakati wowote.

Hakumaanisha tulikuwa na outbreak, katafute kwenye kile kikao kama kuna neno outbreak au tuna janga la Zika.
Ila kupaniki kwa uongozi kulisukumwa na kilichokuwa kinaendelea Brazil na nchi za karibu na huko.
Ni uzuzu wa magu

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Mwele alitumwa na akajibiwa vizuri ukipanda upupu huvuni kuku
 
Magufuli alikuwa CCM establishment alivyochaguliwa tu akawafukuza watoto wote wa mafisadi kazi .
Mafisadi gani hakuna fisadi kama huyo huyo magufuli alitaka Uhuru wa kuchota pesa akawa anawatoa toa wanoko wote anawaweka anaowaweza yeye
 
Mwele alitumwa na akajibiwa vizuri ukipanda upupu huvuni kuku
Utafiti ni kutumwa?
Ninyi mnao amini ushirikina mnashida sana.
Na kama alitumwa lete ushahidi, mwendazake alikuwa na tabia ya kuwarekodi wabaya wake kupitia TCRA, mnazo rekodi akitumwa?
Wafitini ole wenu.
 
Hebu acha uongo Dr Mwele hakufitiniwa na mtu yeyote yule alijifitini yeye mwenyewe! Jiulize ile Zika ilikwenda wapi? Dr Mwele hakufata utaratibu wowote wa kufanya aliyoyafanya maana hata waziri wake hakuwa na taarifa! Uwezi tangaza janga kwenye nchi halafu bila kuzishirikisha mamlaka! Dr Mwele aliwajibika kwa makosa yake mwenyewe tuache kusingizia watu na kuwabebesha watu lawama wasizostahili!
Nyie ndiyo waleee mliozoea kuficha matatizo yaliyopo kwenye jamii kwa sababu za kipuuzi... Huyo waziri alijulishwa vizuri tuu but wakamgomea kwamba hakuna kutangaza, yeye akaona huu ni ujinga and it's unethical kutoijulisha jamii ili watu wachukue tahadhari... Upuuzi nchi hii umeanza leo? Can you imagine mtu kuaminishwa kwamba kipimo cha covid kimepima papai na mbuzi na kuwa positive? Hivi hii inaingia akilini?? Yaani kipimo mfano cha malaria ukapime tikiti maji halafu useme majibu ni compatible really??
 
Btw, tuliambiwa humu kuwa Magufuli alikufa mapema kwa sababu ya madhambi yake; sasa huyu binti amekufa kwa sababu ya madhambi ya nani?
Conclusion za makamanda wakati mwingine ni za kijinga sana!
Kuna wanaokufa kwa kuadhibiwa na Kuna wanaokufa kwa mipango ya Mungu, kwa kuwa wewe ni pimbi huwezi kujua..
 
Pale Dr. Mwele hakutangaza outbreak ya Zika. Alikuwa anaelezea matokeo ya tafiti zilizofanyika. Moja ikihusisha watoto wenye mwonekano kama wale wa wazazi waliopata Zika kule Brazil.

Na matokeo yalikuwa chanya, yakiwa yamefanywa kwa PCR machine. Hii ilionyesha kuwa nasi hatujajitenga na haya matatizo kwani karibu nasi kuna nchi ambazo zilikwishapata Zika (mipaka yetu haina makomeo ya ugonjwa).

Uongozi wa juu ukapaniki, kwani haya ni mambo ya science, Zika ni lifelong/matatizo na uwepo wake unaweza kutambuliwa hata ndani ya miaka yote ya maisha yako. Hivyo, mtu akipata unaweza kupata ushahidi wakati wowote.

Hakumaanisha tulikuwa na outbreak, katafute kwenye kile kikao kama kuna neno outbreak au tuna janga la Zika.
Ila kupaniki kwa uongozi kulisukumwa na kilichokuwa kinaendelea Brazil na nchi za karibu na huko.
Well said [emoji1666][emoji1666][emoji106][emoji106]
 
Umeeleza vizuri sana. Kuna watu wajinga wasioheshimu sayansi kwahiyo ukifanya utafiti kwa mambo wasioyaoyapenda hawataki kusikia matokeo yake. Iwapo angefanya utafiti kuwa watu wangapi na wa marika gani wanampenda Magufuli na akatoa matokeo yake angepandishwa na cheo
Na hii ndiyo moja ya sababu ya Africa kutopiga hatua kisayansi na kiuchumi coz ina viongozi wa hovyo Sana ambao wanachopenda kusikia ni wao kusifiwa. Hawataki hata mara moja kusikia wengine wakisifiwa kwa akili kubwa au uvumbuzi mkubwa. Imagine hata fedha za mikopo hawapendi kabisa kusikia neno fedha hii ni msaada toka nchi fulani, wao wanataka jamii iamini pesa hiyo ni wao wameitoa as if wameitoa from their pockets.
 
Msifanye watu humu wajinga si kila tafiti zikifanyika basi unakurupuka kutangaza hasa tafiti za magonjwa makubwa...usifananesha utafiti wamagonjwa makubwa na utafiti wa vikoba!

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Pumba tupu.. Ndiyo maana hata tafiti za TWAWEZA mlizipiga marufuku kisa kuogopa ukweli...
 
Dr Mwele alikuwa kipenzi cha watu.
Hakuwahi kufanya siasa kwa muda mrefu, lakini uthubutu wake, hasa akiwa mwanamke msomi na mwanasayansi uliwagusa wengi.

Kuna ambao hawakumpenda kwa sababu hizo.
Lakini huu msiba wake umeonyesha alivo moyoni mwa watu.

Magufuli alimfukuza kazi Dr Mwele, saa sita za usiku.
Magufuli lazima alipelekewa umbeya wa kufitinisha, naye kwa vile kulikuwa na kitu rohoni mwake akasema hapahapa, wala hakukuchi!

Lakini dunia ni mviringo, sijui wafitini, na wanajulikana, wanajisikiaje sasa.
Sifkirii kama alifitiniwa tutambue na michango binafsi katika kufanya kosa....
 
Tulisema tukiweka takwimu za uviko 19 hadharani watu watapanic....... Sijui watu wamesha panic au vip?
Watu wanataka kusifiwa wao tu.
Takwimu za covid sasa ziko hadharani na hakuna matatizo yoyote.
Zika ipo hata leo, watu wanajiharishia kutangaza tafiti zao.
 
Back
Top Bottom