Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #201
Maalim Faiza,Allama Mohamed Said usimshangae huyo Ndinani. Hapo kishaishiwa anatapatapa.
Kuna jambo mimi linanistaajabisha sana kwa hawa ndugu zangu.
Hivi hawaiamini hii historia niliyoandika au kitu gani?
Hivi kweli wao wanaona sawa kuwa hii historia yote hii iliyofutwa hivi wangependa kama isingekuwapo?
Kwa nini wana chuki na historia hii?
Hili mosi,
Pili kinachowaghadhabisha ni kitu gani?
Ni kwa kuwa historia hii ni historia ambayo inaeleza kuwepo kwa Waislam Tanganyika na kuwa walipigania uhuru wa Tanganyika au ni nini khasa kinawakereketa nafsi zao na ndiyo maana wakailia njama kuifuta?
Tatu tofauti na wasomi Ulaya na Marekani hawa historia hii imegutua fikra zao na kushangazwa kuwa iweje historia kama hii iwe watafiti wote na wasomi katika Idara ya Historia ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam iwapite wasiifahamu kwa miaka yote?
Sasa wao kwangu mimi wamekuwa ni kuniuliza maswali na kutaka kujua zaidi na kuomba ushahidi kwa baadhi ya mambo ambayo wao hawakuyaelewa.
Hawa sasa hivi wamekuwa msaada mkubwa sana hawa ndiyo walioniletea taarifa za ziri za Special Branch kutoka Uingereza kuhusu Abdul Sykes na harakati zake za siasa wakati wa anahanga kuunda TANU.
Baadhi ya nyaraza hizi nimeziweka hapa barzani na kila wakipata taarifa mpya basi watanitumia.
Ni hawa rafiki zangu walionitia hima nitafute picha ya Denis Phombeah (TANU Card No. 5) hadi nikaitia mkononi.
Nimeweka picha mbili za Denis Phombeah hapa Majlis na nimeandika historia yake naamini wengi mmemsoma.
Historia hizi zinawachoma nini?
Hakuna hata mmoja katika wasomi hawa wa Ulaya na Marekani kanikabili kwa vitisho, kejeli au matusi.
Zaidi wamenipa mialiko kuzungumza kwenye vyuo vyao.
Ni hapa nyumbani tu ndipo historia hii inapandisha ghadhabu kupelekea matusi na kejeli.
Ajabu ya Rahman.
Kisa cha Ally Sykes, Denis Phombeah na Kenneth Kaunda Tanganyika na mkutano wa wapigania uhuru Kusini ya Sahara 1953 - Sehemu ya pili
KISA CHA ALLY SYKES, DENIS PHOMBEAH NA KENNETH KAUNDA TANGANYIKA NA MKUTANO WA WAPIGANIA UHURU KUSINI YA SAHARA 1953 SEHEMU YA PILI Trevor Huddleston Ally Sykes na Denis Phombeah walipoingia ndani ya jengo la uwanja wa ndege mjini Salisbury waliambiwa wasimame mwisho wa foleni nyuma ya...