Waliomsindikiza Mwalimu Nyerere safari ya kwanza UNO 1955

Waliomsindikiza Mwalimu Nyerere safari ya kwanza UNO 1955

Umetaja jina ukaandika bila ushahidi wowote. Una uhakika mohamed Saidi hajaandikia kuhusu John Rupia?

Kwanini wewe usimpe "kipaumbele" kwa kutuletea ya ziasa kuhusu John Rupia.

Hivi alipataje jina la pesa za kihindi "Rupia" na ilhali nijuavyo ni msukuma?

Leta vitu.

Soma vizuri katikati ya mistari na uelewe; sijasema kuwa historia ya Mzee Rupia haijaandikwa la hasha!!! Nimewaambia kuwa hajapewa prominence kama wanavyopewa wakina Abdulwahid na Ally!!!
 
Kimya hujakaa nakubaliana na wewe 100% kwa hilo. Lakini hujaleta historia yoyote ile iwe ya wazee wako au ya wazee wa wenzako.

Ndiyo maana nikakueleza kuwa labda walikuwa upande wa wapinga uhuru. Ndivyo? Ndiyo maana unapata kigugumizi cha mikono kuwaandika?

Upingaji wako unaelekea unataka kujuwa usilolijuwa lakini unaona haya kuuliza. Sababu tu, ulikuwepo wakati huo tena una akili sana lakini inaonesha kwa bahati mbaya kabisa hukuwa upande wa "winners". Huna wa karibu yako aliyekuwa kwenye upande wa kudai uhuru? Kama yupo muelezee. Hii ni challenge. Leta hata kama walikuwa upande wa pili wa shillingi, yote ni historia.

Sheikh nashukuru kwa kunivika kilemba cha ukoka ; mimi sio mwana historia ila nimejaliwa fani nyingine lakini hata hivyo I accept your challenge vuta subira. Ningependa kuandika historia juu ya WAMANYEMA hapa nchini ; nadhani kwavile ulisema babu yako alitokea huko Belgian Congo unaweza kuwa na msaada fulani!!
 
Soma vizuri katikati ya mistari na uelewe; sijasema kuwa historia ya Mzee Rupia haijaandikwa la hasha!!! Nimewaambia kuwa hajapewa prominence kama wanavyopewa wakina Abdulwahid na Ally!!!
Ulitumia neno "kipaumbele" hujatumia neno "prominence" usobadili maneno.

Na mimi nikakujibu nikaandika leta wewe basi hicho "kipaumbele". Maana huwezi kupinga kitu ambacho hukielewi. Tunangoja.

Kuhusu "prominence" ya John Rupia ni nani ambae mtu wa kuzaliwa na kukulia Dar miaka hiyo asiielewe?

Tuelezee wewe hiyo "prominence" yake ambayo haijaelezewa na Allama Mohamed Said. Kinakushinda nini?
 
Sheikh nashukuru kwa kunivika kilemba cha ukoka ; mimi sio mwana historia ila nimejaliwa fani nyingine lakini hata hivyo I accept your challenge vuta subira.
Inna Allah maa swabiri. Tunasubiri.

Kwa kukujuza tu, mpaka leo tunasubiri kutoka kwa pascal mayala aliahidi kama wewe atatafuta kitabu asome aje na mrejesho.

Zamani kidogo aliahidi anaejiita Yericko Nyerere kuwa atakuja na kanda ya hotuba ya Mwalimu Nyerere ya kuaga pale diamond. Tena alisema ataifata Msasani. Mpaka leo tunasubiri, bado tu.

Akaahidi tena atakuja na habari za uhakika kutoka kwa akina Mkwawa. Mpaka leo tunasubiri.

Wakaja kina Mzee Mwanakijiji na wenzake wakaahidi watakuja na kitabu cha kukosoa anayoyaandika Mohamed Said ili waweke historia sawa. Miaka sasa inakwenda bado tunasubiri tu.

Ikiwa tumeweza kusubiri wote hao tutashindwa kusubiri hili lako kuhusu John Rupia?
 
"Prominence" sio kipaumbele bali ni " umuhimu"!!!
Kajisome, uliandika "kipaumbele" uliporudi kunijibu ukachomekea "prominence" na nikakujibu kwa yote hayo. Kanisome vizuri.

Huwa sikisii.
 
Sheikh nashukuru kwa kunivika kilemba cha ukoka ; mimi sio mwana historia ila nimejaliwa fani nyingine lakini hata hivyo I accept your challenge vuta subira. Ningependa kuandika historia juu ya WAMANYEMA hapa nchini ; nadhani kwavile ulisema babu yako alitokea huko Belgian Congo unaweza kuwa na msaada fulani!!
Hapa naona unamjibu "Sheikh" mimi labda uandike "Sheikhat".

Mimi siyo Mmanyema na sijawahi kusema babu yangu katoka "Belgian Congo". Unakurupuka.

Lakini.ukiiansika hisyoria ya Wanyema ukaileya humu tutaisoma. Wengine ni wapenzi sana wa historia ndiyo maana utaona hatubanduki kwenye hii mijadala ya kihistoria. Leta vitu, tunasubiri.
 
Umetaja jina ukaandika bila ushahidi wowote. Una uhakika mohamed Saidi hajaandikia kuhusu John Rupia?

Kwanini wewe usimpe "kipaumbele" kwa kutuletea ya ziasa kuhusu John Rupia.

Hivi alipataje jina la pesa za kihindi "Rupia" na ilhali nijuavyo ni msukuma?

Leta vitu.
Hisitoria yetu imepotoshwa mno lakini ukiwa mvivu wa kujifunza huwezi kugundua hilo.
Anacho andika. Mohamed Said. Kina ukweli kwa 100% tatizo ni jamii yetu ambayo wamepotoshwa na hisitoria ya mashuleni ambayo imewafanya baadhi ya watu kama miungu watu (J.K Nyerere).
Hisitoria yetu imeficha wote na kumuacha Nyerere peke yake kama mpigania uhuru wa Tanganyika.
Hisitoria inaelekea kumfanya Nyerere kuwa ni mtakatifu.
Mpaka sasa sijui lengo mahususi la upotoshaji wa makusudi wa hisitoria yetu?

Mungu ibariki Tanganyika
Mungu ibariki Afrika
 
Inna Allah maa swabiri. Tunasubiri.

Kwa kukujuza tu, mpaka leo tunasubiri kutoka kwa pascal mayala aliahidi kama wewe atatafuta kitabu asome aje na mrejesho.

Zamani kidogo aliahidi anaejiita Yericko Nyerere kuwa atakuja na kanda ya hotuba ya Mwalimu Nyerere ya kuaga pale diamond. Tena alisema ataifata Msasani. Mpaka leo tunasubiri, bado tu.

Akaahidi tena atakuja na habari za uhakika kutoka kwa akina Mkwawa. Mpaka leo tunasubiri.

Wakaja kina Mzee Mwanakijiji na wenzake wakaahidi watakuja na kitabu cha kukosoa anayoyaandika Mohamed Said ili waweke historia sawa. Miaka sasa inakwenda bado tunasubiri tu.

Ikiwa tumeweza kusubiri wote hao tutashindwa kusubiri hili lako kuhusu John Rupia?

Sheikh hili la John Rupia huna haja hata ya kusubili kwani ameishaandikwa sana hata ukienda kwenye Journal of history and Anthropology taarifa zake zimejaa!! Kitu kimoja tu ni huo mtindo mnaotumia mara mnapopata CRITIQUE kujitetea kuwa hao wanaokosoa kazi zenu basi waandike zao!!! Huko kunaonesha kukosa uvumilivu wa kukosolewa.
 
Hapa naona unamjibu "Sheikh" mimi labda uandike "Sheikhat".

Mimi siyo Mmanyema na sijawahi kusema babu yangu katoka "Belgian Congo". Unakurupuka

Hapa umejistukia sio kuwa wewe ni "Sheikhat" na sio mmanyema!!!!
 
Sheikh hili la John Rupia huna haja hata ya kusubili kwani ameishaandikwa sana hata ukienda kwenye Journal of history and Anthropology taarifa zake zimejaa!! Kitu kimoja tu ni huo mtindo mnaotumia mara mnapopata CRITIQUE kujitetea kuwa hao wanaokosoa kazi zenu basi waandike zao!!! Huko kunaonesha kukosa uvumilivu wa kukosolewa.
Siyo "Sheikh" ni Sheikhat.

Kama ni hivyo mbona hata Mohamed Said kisha muandika?

Nilifikiri una kipya au cha ziyada ambacho hatukifahamu.

Hizo sources zako kuna ambacho kinapingana na alichoandika Mohamed Said?

Sasa hapo hujaleta historia wala "citation" wala kimeandikwa nini. Umeandika tu "history journal" na "anthropology", ndiyo nini sasa hiyo? Reference hiyo au ni kujitoa kimasomaso?

History Journal ipi? Maana zipo nyingi tu. Au nikutajie chache ninazozifahamu mimi utuambie ni ipi, labda umesahau?

Anthropoly ni somo. Sasa.kudema "anthropology" ndiyo umefanya nini?

Acha mzaha katika haya mambo ya historia. Siyo unaleta vitu vya kutoa watu njiani. Weka vitu vyenye rejea za uhakika, nani kaandika? reference ipi? citation?

Ingawa mnadhani sisi wa Kariakoo hatujasoma lakini nakukumbusha tu, tuna uelewa wa kutosha kuwa huwezi kututoa njiani kwa namna hiyo.
 
Soma vizuri katikati ya mistari na uelewe; sijasema kuwa historia ya Mzee Rupia haijaandikwa la hasha!!! Nimewaambia kuwa hajapewa prominence kama wanavyopewa wakina Abdulwahid na Ally!!!
Ndinani,
Unaweza kuanza kusoma hapo chini:
  1. Ally Sykes ana barua ya mwaka 1954 iliyoandikwa kwa penseli toka kwa Zuberi Mtemvu kwenda kwake akimtaarifu juu ya mazungumzo aliyokuwanayo (Mtemvu) na Nyerere kuhusu yeye na TANU; stakabadhi ya hundi ya posta toka kwa Ally Sykes kwenda kwa Japhet Kirilo wakati wa Mgogoro wa Ardhi ya Wameru; nakala ya barua isiyokuwa na tarehe kutoka TAA kwenda kwa Malkia Elizabeth iliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA: Rais Julius Nyerere, Makamu wa Rais Abdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi, Naibu Katibu Dossa Aziz, Mweka Hazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwa kutawazwa; barua ya mwaka 1952 toka kwa Rashid Mfaume Kawawa kutoka Bukoba kwenda kwa Ally Sykes ikimfahamisha juu ya hali ya siasa katika Kanda ya Ziwa; barua ya mwaka 1963 toka kwa Lady Judith Listowel, Kenneth Kaunda, Julius Nyerere, Kasela Bantu, Chifu Thomas Marealle ...orodha haina mwisho.
  2. Hakuna nyaraka zozote zinazoonyesha kama African Association ilikuwa imetayarisha mpango wa kushughulikia hali ya siasa. Kuelewa mwelekeo wa siasa kama wakati ule inabidi mtu atazame mwenendo wa viongozi wa TAA na jinsi walivyokuwa wakiyashughulikia mambo tofauti yaliyokuwa yakiwadhili wananchi. Jambo la kwanza alilofanya Abdulwahid mara tu baada ya kuingia madarakani ni kuunda TAA Political Subcommittee (Kamati Ndogo ya Siasa ya TAA) iliyomjumuisha yeye mwenyewe Abdulwahid, Sheikh Hassan bin Amir kama mufti wa Tanganyika; Dr. Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, Said Chaurembo aliyekuwa liwali wa mahakama ya Kariakoo; John Rupia na Stephen Mhando. Kazi ya kamati hii ilikuwa ni kushughulika na masuala yote ya siasa katika Tanganyika. Kuundwa kwake ndiyo hasa ulikuwa mwanzo wa siasa za dhahiri katika Tanganyika na mwanzo wa harakati za kudai uhuru wa Mtanganyika.
  3. John Rupia kutoka Mission Quarter alikuwa mfanya biashara tajiri na mfadhili wa chama.
  4. Sheikh Hassan bin Amir, Abdulwahid Sykes, Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, John Rupia, Stephen Mhando na Said Chaurembo.
  5. Chama kilikuwa hakijimudu na kilikuwa kikiendesha shughuli zake kwa msaada wa fedha zilizotolewa na Rupia, akina Sykes, Dossa Aziz na wahisani wengine wachache.
  6. Hawa ndio walikuwa wanasiasa maarufu wa African Association: John Rupia, mzee wa umri makamo na mtu mwenye kujiweza.
  7. Baadaye April 1954, Abdulwahid, Nyerere na Rupia walikwenda Bugandika, nyumbani kwa Migeyo.
  8. Uongozi wa ndani wa TAA wa Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz na Rupia ulikuwa tayari umekwishaamua kumpa Nyerere urais wa chama.
  9. Akakihofia kufa kwa chama, Abdulwahid aliwataka shauri viongozi wenzake wa ndani katika TAA - Ally, Dossa, Tewa na Rupia kuwa kipi kifanyike ili kudhibiti hali ile iliyojitokeza.
  10. Waliobakia karibu na Abdulwahid, Nyerere na TAA walikuwa wale wanachama sugu na wachache wasiosikia la muadhini wala la mteka maji, kama Ally Sykes, Dossa Aziz na John Rupia.

Ndinani

Nilikuuliza juu huko, vipi John RUPIA ana jina la pesa za Kihindi "rupia" na yeye tujuavyo ni Msukuma, hujanijibu.

Kama hujuwi sema tu, maana sitegemei kuwa unaweza kujuwa kilakitu kuhusu John Rupia.
 
Nikweli wahusika wengi hawatajwi na inawezekana walikuwa na mchango mkubwa kuliko hata Nyerere
Historia pana ya uhuru wa tanganyika na mambo yake ipo mtaani kwa wazee wa kitambo,
Ya shuleni imechujwa chujwa wee utamu wote ukachwa,
 
Hapa umejistukia sio kuwa wewe ni "Sheikhat" na sio mmanyema!!!!
Sheikh linatumika kwa wanaume. Sheikhat kwa wanawake.

Ningekuwa Mmanyema ningejisifu na kujisikia sana sana kwani sijawahi kukutana na Mmanyem asiye Muislam.

Wapo Masheikh na Masheikhat wengi sana wa Kimanyema.
 
Ndinani

Nilikuuliza juu huko, vipi John RUPIA ana jina la pesa za Kihindi "rupia" na yeye tujuavyo ni Msukuma, hujanijibu.

Kama hujuwi sema tu, maana sitegemei kuwa unaweza kujuwa kilakitu kuhusu John Rupia.

Hili neon RUPIA linatokana na RUPEE ambayo ni fedha za India. Sasa Mzee John cuita kwa jina hilo bila shaka ilitokana na yeye kuwa tajiri!!
 
Nime
Sasa kama nimeandika wewe unauliza nini?
Nimeuliza wewe wapi? Maana umewataja "wa Msikitini" kama viile ni kitu kigeni sana kwako au cha ajabu. Kwa kejeli.

Hivi kukejeli mtu ambae hana imani kama yako kunakusaidia nini? Ndiyo imani yako ilikifunza hivyo au ni kibri tu?
 
Hili neon RUPIA linatokana na RUPEE ambayo ni fedha za India. Sasa Mzee John cuita kwa jina hilo bila shaka ilitokana na yeye kuwa tajiri!!
Ooh kwa kujuwa mambo wewe ni hodari sana. Hiyo ni historia iliyotukuka ya John Rupia.

Sasa nijibu na yale ya "history journal" na "anthropology" uliyoyaleta, si unakumbuka?
 
Sheikh hili la John Rupia huna haja hata ya kusubili kwani ameishaandikwa sana hata ukienda kwenye Journal of history and Anthropology taarifa zake zimejaa!! Kitu kimoja tu ni huo mtindo mnaotumia mara mnapopata CRITIQUE kujitetea kuwa hao wanaokosoa kazi zenu basi waandike zao!!! Huko kunaonesha kukosa uvumilivu wa kukosolewa.

= kusubiri.
 
Back
Top Bottom