Si ndio maana nikakwambia historia uliyotuletea wewe ni "bab kubwa" na haipo "biased" kabisa.
Halafu tupe kile kipande cha wazee wako walishiriki vipi katika kudai uhuru, na "roles" walizo "play" kabla ya Uhuru, maana ulibahatika na ulipendelea na Mwenyeezi Mungu (kama ulivyotujulisha juu hapo) kuwa wakati huo tayari ulikuwa una akili (bahati mbaya bwana umesahau kutueleza wakati upi) lakini huyu
mohamed said analeta ya wazee wake toka kabla ya 1920s na wewe unayo ya wakati huo au upi? Funguka bwana. Tupe bwana. Na hiyo ya kuwa na akili bwana kisayansi ni "heredity" achana na huyo na u "bias" wake kakazania "wazee wangu wazee wangu". Tupe kidogo. Hata kama wazee wako walikua upande wa pili wa shillingi wewe lete tu usione haya.
Nasema upande wa pili, kwani lazima kama kuna "waliodai uhuru" basi kuna "waliodaiwa uhuru" na kuna waliokuwa upande wa wadai uhuru na kuna waliokuwa upande wa wadaiwa uhuru.
Sisi wazaliwa na wakulia Kariakoo bwana tunafahamu upande mmoja tu wa wadai uhuru na kule mission quarter tunafahamu kuwa ulikuwa upande wa wadaiwa uhuru bwana. Tunafahamu kuwa wote ya wasio Waislam walikuwa wasomi na wenye akili sana kwa hiyo walipewa kazi na wadaiwa uhuru na wengi wao wakawa upande wa wadaiwa uhuru wakiogopa maslahi yao.
Hata kama wewe ni wa upande huo wa walioogopa, tupe tu bwana/bibi
Ndinani kwani lazima kuna pande mbili (heads na tails).
Wewe ni vitu adimu kabisa bwana, maana utakuwa unayajua ya "tails" siyo huyu anatuketea "heads" tu. Lete elimu bwana isiyokuwa "biased" isipotee bure ukazikwa nayo. Si unaona kina Sykes wamewaachia watoto nyaraka sasa ni kumbukumbu nzuri sana, hata wewe umeshauri arudi kwa Abbas Sykes akaulize! Au siyo bwana? Hivi wewe hauna wakumuuliza upande huo wa.pili ukatuletea hayi mamb9 bwana ili tumuweke sawa huyu
Mohamed Said? Lazima na wewe utakuwa na mengi yako na ya wazee wa upande wako waliyoyaacha bwana. Haiwezekani wazee wa kariakoo na gerezani wasio wasomi kama hawa wa
Mohamed Said wawe na nyaraka na mapicha na kumbukumbu. Na wasomi kama wewe na wazee wako msiwe na chochote cha kulipa taifa la leo kama kumbukumbu njema bwana.
Au umeleta bwana na sisi hatujaviona bwana?