Wewe ulitaka mimi niandike historia ya Mzee John nikakwambia huna haja ya kusubiri kwani imeishaandikwa bila bias yeyote ya udini na nikakupa reference sasa unataka nini zaidi sheikh!!!
Hukuweka reference wala hukunukuu kilichoandikwa.
Ona ulichoandika...
"...ukienda kwenye Journal of history and Anthropology..."
Hiyo ndiyo "reference" au kututoa njiani?
Nikakuuliza kuna kipi katika hizo "references" zako kilichopingana na alichoandika
Mohamed Said?
Ukawa huna la kujibu, mpaka dakika hii unapiga piga chenga tu. Njoo na historia "solid" si kubabaisha babaisha useme ndiyo historia.
Kwani Allama
Mohamed Said hujamsoma anachokisema siku zote? Kuwa kaisoma historia iliyopo akakuta mapungufu au kwa lugha yako akakuta "bias" na yeye akaona aandike anayoyajuwa, aliyoyaishi, anaowajuwa kuweka sawa historia iliyopotosha ikapindisha ukweli au iliyowaacha wazalendo waliokuwa mstari wa mbele kuutafuta uhuru kabla hata ya Nyerere kuja Dar.
Na naam, historia aliyotuletea ni adhyim na adim na ndiyo kila akiingia humu mijadala yake hujaza watu wenye shauku za kila namna.
Huelewi hayo?
Wewe badala ya kuja na historia inayomuweka sawa alipopindisha au alipopaacha unakuja na porojo unatuambia kasomeni huko.
Tukasome badala ya kuonesha hii hapa umeandika kuhusu John Rupia ipo "biased" ukaweka "citation" ya ulichokisoma kuwa hakipo sawa. Huna. Nini huko ulichokiona ambacho kipya hata utupe kazi ya kupatafuta?
Kama wewe huna ulijualo si weka "citation" za huko ulipopaita "reference" yako ambayo siyo "bias", japo ya sentensi mbili tatu ili utukinaishe?
Tunasubiri. Nnauhakika tutasubiri sana kama njlivyokueleza juu huko. Wenzako miaka inakatika bado tunawasubiri sijuwi "wameingia mitini"? Bado wewe.
Tunasubiri.