Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi

Ni raha sana kutawala Taifa ambalo wengi wa wananchi hawana uelewa( wajinga wengi_, mtu atakwambia kwani hiyo Bandari ntaila? inanihusu nn ? mie napigania ugali wa wanangu bwana, nikaandamane afu wanivunje miguu nani atanitibia na kuwalisha wanangu nikiwa rumbande ama jela 😀 😀

Sasa hata mimi nginekuwa Rais hapo nachekelea tu, siku zinasonga mbele.
 
Umenena kweli sn mkuu
 
Halafu wananchi wenyewe wanashangaa hata hawaelewi kinachoendelea, ukute wengine walijua movie inaigizwa🤣🤣🤣

Sema nini, wabongo tunavimba sana nyuma ya keyboard, location mambo tofauti sana🤣🤣🤣
Mimi Leo kila nnae muuliza kuhusu maandamano ananiuliza Mimi .. maandamano kuhusu nini??

Watu hawataki kabisa kusumbuana na serikali.....kila mtu anawaza kuiba upande wake .🤣🤣🤣🤣
 
Dada jasiri kabisa. Jina lake? tuomtoe Rumande.

Polisi Tanzania muwe wazalendo, mwachiane dada na wote mliowakamata. Wanaopigania maslahi yenu na familia zenu kwa miaka 100 inayokuja.
 
Acha upotoshaji wa kijinga, amekamatwa nikiona kwa macho yangu.
Yuko Masaki bwana, ni jirani yangu Chole Road. Wana duka la hardware mtaa wa Narung'ombe, ni mdogo wa binamu yake mbowe anaishi Washington DC Marekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…