Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi

Dada jasiri kabisa. Jina lake? tuomtoe Rumande.

Polisi Tanzania muwe wazalendo, mwachiane dada na wote mliowakamata. Wanaopigania maslahi yenu na familia zenu kwa miaka 100 inayokuja.
Ni shoga, anamiliki NGO ya LGBQT ni katika list ya Dr. Mwakyembe
 
Jamani tumewasaliti wenzetu wanao fungwa kwaajili yetu shame on us keyboards worries
 
Tukishirikiana vizuri hao polisi hawataweza kutufanya chochote.mimi kwenye maandamano alitaka kunikamata polisi nikamzaba kibao hadi aliona nyota na kuniacha.
[emoji1787][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Habari wana jf wenzangu,sina mengi ya kueleza nazani kichwa cha habari hapo juu kina jieleza.


WANAZUONI natumaini leo walikua miongoni mwa walio andamana.
 

Attachments

  • Fy-sVm7XsAUvNW3.jpeg.jpg
    87.3 KB · Views: 1
Ila virungu nyie mvisikiage tu, achana kabisa na habari ya virungu.

Nashauri maandamano yawe yanafanyika kwenye twitter space na tuendelee kuvurumisha mapost humu jamii forums..

kitaeleweka tuuu!!
 
Namimi naona mijadala ya kumpinga mama kuhusu bandari iachwe sasa tuangalie mambo mengine.
Wenye uchungu zaidi ndio hao hapo waliokamatwa.

Kubwabwaja mitandaoni bila kuchukua hatua kwa vitendo nadhani haina maana.

Hawa watu wametuwakilisha watu wengi ambao ni waoga wa virungu.

Pongezi pia kwa jeshi la polisi hawa watu hawakupigwa hata kofi, hii imenishangaza sana.
 
Wewe ulikuwa unajua wale Wehu CHADEMA wangeandamana? Sahau hiyo, yule Chiba anajifurahisha tu kwa Kulamba asali huku mzee wa bapa mwenye makengeza anatembea na wake za watu tu akina Joyce huku anawahonga ubunge wa viti maalum.
 
P
Mi ndo maana kila siku nasema Bungeni kitu kikipita hakuna maajabu yatakiondoa, zilikuwepo harakati za Tozo ila sasa hazipo tena, ikaja ushoga, sasa ni bandari yataisha
Pambana tu kutafuta ugali wako na wanao. Watawala wa kiafrika hawasikii lugha nyingine isipokuwa mtutu. Harakati za mabango na kulalamika ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.

Ona waarabu wanapoamua lao,njia wanazozitumia kuzungumza na watawala.
 
Unajiandaa kwenda vitani huku umebeba bango halafu mpinzani wako amekushikia bunduki!! Hivi una akili sawasawa??

Muandamanaji wa mabango ni sawa na mfungwa aliyopo gerezani tu.Hata apige kelele vipi ndani ya kizimba chake hawezi kusikilizwa na hakimu wala polisi magereza.

Mwacheni Mama Samia apige kazi!!!
 
Sio useme "nguvu ya umma ijitokeze". Unatakiwa useme wewe utaongoza nguvu ya umma kupinga. Kama huwezi wewe kujitokeza Kaa kimya!
 
SWAT! SWAT kama inavyoonekana mgongoni kwenye kizibau alichovaa polisi pichani ni vikosi vya Polisi wa Marekani wenye utaalamu wa kijeshi wa kuweza kutumia silaha za kuangamiza, Tanzania ya leo imefikia huko!
 
Uonevu tu huu, kuandamana ni haki ya kikatiba.....nyie mnaoivunja hii haki mnakiuka katiba.
 
Uonevu tu huu, kuandamana ni haki ya kikatiba.....nyie mnaoivunja hii haki mnakiuka katiba.

Tanzania ipo katika right track kama maandamano haya hayatafifia yatakuwa endelevu bila kukoma na vijana wote kujitokeza kwa wingi kuwa chachu ya kushawishi jamii yote kubwa kuwa nyuma yao idai mabadiliko na haki za kisiasa pamoja na vile za kijamii

KUTOKA MAKTABA:

VIJANA NA MABADILIKO

Duniani ni vijana wa vyuo vikuu ndiyo wanaoongoza kuchagiza mageuzi

Historia inaonesha mara baada ya uhuru wa kwanza kupatikana ktk mtaifa mbalimbalii iwe kwa mtutu wa bunduki au maandamano ya kuondoa wakoloni, baadaye kulifuatia msuguano wa wananchi wenyewe kwa wenyewe kwa kutoridhishwa na wale waliochukua utawala toka kwa wakoloni.

Sababu mbalimbali zilizua msuguano ktk nchi huru kama udiktekta, tawala kamdamizi ya chama kimoja, utawala mbovu, ubaguzi wa kielimu mfano mtoto aliyesoma shule za kata / st. Kayumba anadanganywa kuwa akihitimu chuo kikuu atakuwa na nafasi sawa na mwenzake aliyesoma St. Mary's akamaliza elimu ya chuo kikuu pia anayekimanya kiingereza vizuri zaidi na wajomba wake wapo ktk nafasi za kiutawala n.k

Hapo ndipo Wanafunzi waliopo ktk nchi kama Sudan, Chile, Cuba, Afrika ya Kusini, Kenya walishiriki kudai mageuzi ili kuondokana na tawala zilizomgoa mkoloni.

Tanzania vijana hawajishughulishi kuhoji mambo yasiyowaridhisha wananchi kama bandari kuchukuliwa kuwa vituo vya nchi ngeni, matumizi mabaya ya kodi za wananchi, tozo ziluzokifu wananchi, demokrasia kubinywa, katiba kandamizi n.k

Huko Chile marekani ya kusini nchi iliyo viongozi wa vyama vya wanafunzi wenye kushiriki kikamilifu katika siasa pia maandamano imewezesha kiongozi kijana wa wanafunzi Gabriel Boric ambaye ndiye rais kijana kabisa wa kuchaguliwa amezaliwa 11 February 1986 ambaye alichukua madaraka ya urais tarehe 11 March 2022 baada ya kushinda uchaguzi mkuu nchini Chile tarehe 19 December 2021 kwa kupata asilimia 60% ktk uchaguzi wa urais.

Gabriel Boric on the Chilean student movement 14 June 2017
Mwanafunzi wa chuo kikuu toka familia masikini anazama ktk mkondo wa madeni ya fedha za mkopo wa elimu ya juu huku akiwa na matumaini potofu ya kupata ajira au kuwepo mazingira hewa ya kujiajiri.


Vijana vyuo vikuu na mijini pia vijijini badala ya kumezwa na ukiritimba wa UVCCM na ahadi kuwa ni viongozi wa kesho huku watoto wa vigogo wa CCM wanapewa nafasi sasa na siyo kesho wanatakiwa kuunda chombo chao kipya cha kutambulika kama mdau muhimu anayehitaji kuonekana katika majukwaa ya siasa pia ktk vituo vya redio, televisheni na mitandao ya kijamii kuchagiza mabadiliko na mageuzi ikiwemo pia kupewa nafasi nje ya mfumo wa vyama ili wagombee nafasi za kuchaguliwa na wananchi.


Gabriel Boric - The 100 Most Influential People of 2022 - TIME

time.com › collection › gabriel-boric


23 May 2022 · He is making Chile the social, economic, and political laboratory of the world once again. Stiglitz is a Nobel Prize–winning economist
 
Wanaosema hivi ni SOCIAL MEDIA MANIPULATORS, sio wananchi wa kawaida, ni MAKACHERO HAO.

Wanajaribu kutengeneza MASS DESPERATION na HOPELESSNESS.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…