Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi

Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi

Nguvu ya Umma ijitokeze kwa namna zote kupinga maeneo ya Tanganyika kugeuzwa makoloni ya mabeberu

19 June 2023
Dar es Salaam, Tanzania

Vijana walioandamana jijini Dar es Salaam kupinga mkataba wa Bandari eneo la Mnazi Moja wame kamatwa na jeshi la polisi
Sijafungua hiyo video ila huyo askari hapo mashaallah!!
 
Deus Soka kijana ambaye amekubali kutumika na wanaharakati na wanasiasa bila kujua athari zake kwa kuhamasisha maandamano leo jumatatu hajaonekana kwenye maandamano hayo na matokeo yake walioingia mkenge wamenaswa na sasa familia na ndugu wanakaa vikao vya kwenda kuwanasua.

Kibaya zaidi wanaowatuma wamekaa maofisin wanaandika maandiko ya kuomba hela kwa wazungu ili kuendelea kuhamasisha ujinga nchini ilhali wao na familia zao maisha yanaenda.

Watanzania tubadilike, hamtamuona mtoto wa Mbowe wala Tundu lissu wala Maria Sarungi.

Sasa hela ya kula na familia mnakwenda kuitumia kama nauli ya kwenda na kurudi polisi kila siku.

Hiyo ndio concept ya Poverty Circle.
 
.
20230512_225747.jpg
 
Acha utoto wako hapa jf sio facebook
 
Watanzania kwenye unafiki tupewe maua yetu, kipindi naanza Kazi utakuta labda kuna Jambo linawakera mnapanga tumchane bosi kwenye kikao, siku ya kikao wenzako wanakugeuka, unaonekana wewe ndo mbaya....tokea hapo nawaheshimu watanzania.

Aliyeanzisha maandamano ukute saa hizi Yuko na bebi wake wamepumzika wakitafute cha pili, Mie Mwajuma ndala ndefu nikaandamane, thubutuuu.....SITOKAA NIANDAMANE hata serikali ije iniuze Mie mwenyewe....nini Bandari.
 
Tukiondoa uoga, kujipendekeza na unafiki,tunaweza kuionesha serikali kuwa Tanzania hii siyo ile ya Nyerere...
Mkuu vijana wa enzi ya Nyerere na Mwinyi walikuwa jasiri, waliandamana hata watoto wa shule walikuwa wanaandamana;

lakini hawa wa leo wala chips, wengine waoga, wanafiki, chawa hawawezi kuandamana, wengine kazi yao ni kuwachongea wenzao tu.

Hata Bungeni; lile la zamani lilikuwa bora hasa, Mawaziri walikuwa wanajipanga na majibu ya uhakika.

Nadhani mnalikumbuka lile G55 lilimwinua Mwalimu kutoka Msasani hadi IBungeni kusawazisha mambo.
 
Tanzania sio nchi ya kuamini watu, Watanzania ni waoga sana,
Hatujiamini

Tungekuwa twajiamini tungeanza maandamano tokea Magu yupo madarakani.
Ila yalipotangazwa maandamano nilifika posta pako kimya sana kuliko hata Jumapili
Na pale ndo viongozi walizidi kutudharau, hakuna kiongozi anayeheshimu watu waoga na wanafiki.
 
Back
Top Bottom