Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi

Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi

Kuwakamata hao waandamanaji ndio wanaharibu kabisa, polisi wanathibitisha Tanganyika tunatawaliwa na mkoloni.

Samia ni msaliti. Tunaitaka Tanganyika yetu.
mbona hukwenda umewacha wengine waandamane?

Uhodari wa kuandika kwenye mitandao tu
 
Kwa ni unawaita binadamu wenzio mbwa waoga?

Ikiwa wewe ulienda kwa maandamano umebadilisha mkataba?

Na kama hukuenda kwa maandamano je na wewe ni mbwa muoga?

Majibu ya maswali hayo yapeleke kwa m/kiti wa mtaa wako.
ni mbwa waoga na wanafiki wakubwa.
 
Maskini dada wawatu kiherehere kimemponza
 
Huyu dada hakuandamana ni mpita njia lakini Polisi wamemkamata kinyume na sheria.
 
Kwa ni unawaita binadamu wenzio mbwa waoga?

Ikiwa wewe ulienda kwa maandamano umebadilisha mkataba?

Na kama hukuenda kwa maandamano je na wewe ni mbwa muoga?

Majibu ya maswali hayo yapeleke kwa m/kiti wa mtaa wako.
Kwa hiyo mnapo shinda humu mnabwabwaja humu mkataba umebadirika?
Kama hamuwezi kusimamia kile mnacho kitetea kaeni kimia acheni kutupigia makelele.
 
Yaa

Polisi wa Tanzania wao wafuata amri na wamejiandaa kuvunja goko za watanganyika wenzao.

Na kufanya hali iwe ya kuogofya zaidi wamejipa jina la SWAT.

Yaani ile FFU haipo tena.

Tanganyika ina safari ndefu sana.
Polisi ni chombo Cha Dola,Dola ni kitu Cha mwisho kufa katika taifa,ni kheri raia wafe Dola ibaki,tia Hilo kwenye fuvu lako
 
Vijana waandamana jijini Dar es Salaam Tanzania kupinga mkataba wa bandari kati ya serikali na Dubai Ports World pamoja na muswada wa marekebisho ya sheria ya Usalama wa Taifa.

Vijana walioandamana jijini Dar es Salaam kupinga mkataba wa Bandari wamekamatwa eneo la Mnazi Moja.


========

WALIOANDAMANA WAISHIA MIKONONI MWA POLISI

Taarifa za awali zinaeleza kuwa vijana waliokuwa wameandamana kupinga Mkataba wa Bandari eneo la Mnazi Mmoja kuelekea Ikulu ya Magogoni Dar es salaam wamekamatwa na Jeshi la PolisiTaarifa zaidi zitawajia endelea kutufatilia.


MRATIBU WA MAANDAMANO AINGIA MITINI

Jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya vijana waliojitokeza kuandamana kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo, a mratibu wa maandamano hayo, Deus Sokkatika hali ya kutofahamika, hajatokea kwenye maandamano hayo yaliyopangwa kuanzia Temeke na kuishia Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Mwananchi Digital ilipomtafuta kwa simu zake zote za kiganjani, hakupatikana na katika majina ya waliokamatwa na polisi pia jina lake halikuwepo.

Juni 15 mwaka huu Deus Soka ambaye aligombea udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, alitangaza kuitisha maandamano kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo Juni 17 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam likipiga marufuku maandamano hayo na kueleza kuwa, mtu aliyeandaa maaandamano hayo ameshajibiwa kwa barua akielezwa ni marufuku kufanyika maandamano yoyote.

Juni 10, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha azimio kuhusu pendekezo la kuridhiwa kwa mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha ushirikiano katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.

Pendekezo hilo liliwasilishwa bungeni Juni 10, na kupitishwa na Bunge baada ya wabunge kupata fursa ya kuchangia na kuishauri Serikali kuhusu mkataba huo.


Mwananchi

PIA, SOMA:
- Vijana kufanya Maandamano kupinga Mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Dubai
- Polisi yapiga marufuku maandamano ya kwenda Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam, Jumatatu Juni 19, 2023
Katika kuonyesha mshikamano kwa hili jambo la bandari, itapendeza wale wote wanaupinga wajitojeze mahakamani kwa wingi, 🙏🙏
 
Kwa hiyo mnapo shinda humu mnabwabwaja humu mkataba umebadirika?
Kama hamuwezi kusimamia kile mnacho kitetea kaeni kimia acheni kutupigia makelele.
Nina mashaka kama upo central police, wewe nawe ni "mbwa muoga"

Endelea kuperuzi social media kupata umbea zaidi 😂
 
Kuwakamata hao waandamanaji ndio wanaharibu kabisa, polisi wanathibitisha Tanganyika tunatawaliwa na mkoloni.

Samia ni msaliti. Tunaitaka Tanganyika yetu.
Na tunataka Samia na Mbarawa warudi kwao watuache nchi yetu
 
Ivi ili yaitwe maandamano waandamani wanatakiwa wawe kuanzia wangapi
 
Wewe usimwangalie profesa bana. Kwani ungali under 18? Simama wewe kama wewe. What if profesa ameshalambishwa asali?

Usiitelekeze nchi yako. Ipiganie kufa na kupona. Ipambanie hadi tone la mwisho la damu yake! Isimamie imara, bila kuyumba. Ipatie kipaumbele. Nchi yako iwe moyoni mwako daima.

KauliMbiu: Bandari Haitoki!
Sidanganyikiii, Yani nikaumie kisa tumbo la mtu mwingine? Hao tuliowapa dhamana wakitaka watoe, wakitaka waache....as long hawatoi bure nitasubiri nione matokeo.....Ila Mimi NIANDAMANE never
 
Back
Top Bottom