Kidagaa kimemwozea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 3,680
- 6,554
Mtandao uliotoa takwimu na kusema Tanzania inashika nafasi katika ligi tano Bora Afrika bila kujali Kigezo walichotumia huenda takwimu hizo zilisukumwa na aidha kutokuwa na taarifa sahihi kuhusu ligi za Afrika, au mitazamo na mihemko binafsi au labda alitumia Kigezo cha kuwa na mashabiki na followers wengi katika mitandao ya kijamii. Unapozungumzia ligi hauongelei timu moja au mbili Bali vilabu vyote vinavyoshiriki ligi kuu pengine na ligi nyinginezo za chini.
Nalubaliana na hoja kuwa tanzania inaweza kuwa na vilabu Bora kimoja au viwili lakini hatuna ligi Bora. Ligi yetu haijawahi kutoa wachezaji Bora Afrika Wala wachezaji wakutumainiwa Sana katika timu zao za Taifa (wanaoweza kufanya makubwa kwenye mashindano katika timu zao za Taifa)
Ligi yetu bado inahitaji uwekezaji mkubwa ili timu zote zimudu kuwa na wachezaji Bora kutoka kila pembe ya Dunia.
Tukiwa na ligi Bora hata timu yetu ya Taifa utapata ahueni. Hauwezi kuwa na ligi Bora then ukose timu ya Taifa Bora. Aidha linapokuja suala la ushindani ligi yetu bado Sana. Ushindani upo baina ya vilabu vikubwa viwili kwa miaka mingi huo ubora uko wapi? Je, manufaa ya ubora huo yako wapi?
Ikiwa hata timu yetu ya Taifa ambayo inawachezaji wengi wanaocheza ligi ya tano Bora Afrika wanashindwa kufuzu Chan?
Chanzo masshele.com