Waliosema Tanzania ni miongoni mwa ligi tano bora Afrika wajitafakari

View attachment 2506865

Mtandao uliotoa takwimu na kusema Tanzania inashika nafasi katika ligi tano Bora Afrika bila kujali Kigezo walichotumia huenda takwimu hizo zilisukumwa na eidha kutokuwa na taarifa sahihi kuhusu ligi za Africa, au mitazamo na mihemko binafsi au labda alitumia Kigezo Cha kuwa na mashabiki ma na follower wengi katika mitandao ya kijamii. Unapozungumzia ligi hauongelei timu moja au mbili Bali vilabu vyote vinavyoshiriki ligi kuu pengine na ligi nyinginezo za chini

Nalubaliana na hoja kuwa tanzania inaweza kuwa na vilabu Bora kimoja au viwili lakini hatuna ligi Bora. Ligi yetu haijawahi kutoa wachezaji Bora Afrika Wala wachezaji wakutumainiwa Sana katika timu zao za Taifa (wanaoweza kufanya makubwa kwenye mashindano katika timu zao za Taifa)

Ligi yetu bado inahitaji uwekezaji mkubwa ili timu zote zimudu kuwa na wachezaji Bora kutoka kila pembe ya Dunia.

Tukiwa na ligi Bora hata timu yetu ya Taifa utapata ahueni. Hauwezi kuwa na ligi Bora then ukose timu ya Taifa Bora. Aidha linapokuja suala la ushindani ligi yetu bado Sana. Ushindani upo baina ya vilabu vikubwa viwili kwa miaka mingi huo ubora uko wapi? Je manufaa ya ubora huo yako wapi?

Ikiwa hata timu yetu ya Taifa ambayo inawachezaji wengi wanaocheza ligi ya tano Bora Afrika wanashindwa kufuzu Chan?

Chanzo masshele.com
Weka list yako...acha maneno mingi chalii.

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Taasisi iliyotoa hizo Takwimu ni ya mchongo iko Saudi Arabia
 
Pinga takwimu kwa takwimu,sio unakurupuka na kupinga bila kufahamu vigezo vilivyotumika[emoji144]
 
Ligi bora inaundwa na clubs bora, chukulia mfano hapa kwetu kuna club inaweza challenge clubs za South Africa ki uchumi, miundombimu na quality ya wachezaji?
 
View attachment 2506865

Mtandao uliotoa takwimu na kusema Tanzania inashika nafasi katika ligi tano Bora Afrika bila kujali Kigezo walichotumia huenda takwimu hizo zilisukumwa na eidha kutokuwa na taarifa sahihi kuhusu ligi za Africa, au mitazamo na mihemko binafsi au labda alitumia Kigezo Cha kuwa na mashabiki ma na follower wengi katika mitandao ya kijamii. Unapozungumzia ligi hauongelei timu moja au mbili Bali vilabu vyote vinavyoshiriki ligi kuu pengine na ligi nyinginezo za chini

Nalubaliana na hoja kuwa tanzania inaweza kuwa na vilabu Bora kimoja au viwili lakini hatuna ligi Bora. Ligi yetu haijawahi kutoa wachezaji Bora Afrika Wala wachezaji wakutumainiwa Sana katika timu zao za Taifa (wanaoweza kufanya makubwa kwenye mashindano katika timu zao za Taifa)

Ligi yetu bado inahitaji uwekezaji mkubwa ili timu zote zimudu kuwa na wachezaji Bora kutoka kila pembe ya Dunia.

Tukiwa na ligi Bora hata timu yetu ya Taifa utapata ahueni. Hauwezi kuwa na ligi Bora then ukose timu ya Taifa Bora. Aidha linapokuja suala la ushindani ligi yetu bado Sana. Ushindani upo baina ya vilabu vikubwa viwili kwa miaka mingi huo ubora uko wapi? Je manufaa ya ubora huo yako wapi?

Ikiwa hata timu yetu ya Taifa ambayo inawachezaji wengi wanaocheza ligi ya tano Bora Afrika wanashindwa kufuzu Chan?

Chanzo masshele.com
Acha kukariri mbona premier league ni bora ila timu ya taifa sio bora kihivyo.
 
Ww kweli hujui hata takwimu zinapatikana vipi takwimu ni overall performance na sio seasonal performance ndio maana team namba moja duniani kwa ubora ni Brazil licha ya Argentina kuchukua world cup na Brazil ndio team pekee duniani ambayo haijawahi kukosa kushiriki world cup toka ianzishwe kwa hyo Senegal kwasababu kawa bingwa basi ndio awe namba moja sio

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
Acha kukariri mbona premier league ni bora ila timu ya taifa sio bora kihivyo.
Mwaka gani umesikia timu ya Taifa ya England Ipo nje ya Top 10 Duniani!! Mwaka gani umesikia Ligi ya uingereza inashika nafasi ya tatu Kwa ubora barani Ulaya maana wao kama si wa kwanza basi wa pili. Ligi yetu ni mbovu haistahili ata kuwa ya 10 Kwa Afrika.
 
Timu ya Taifa ni kujaza Usimba na Uyanga humo waifumue kikosi cha kwanza watoke wale wachezaji wa timu zingine wenye damu changa na wapambanaji
 
Waingereza walituachia umbea na ligi timu la taifa bovu.. 😂 😂

Kwanza napinga kuwa namba 5',
Ligi za misri, morroco, algeria, tunisia, South Africa, angola, sudan zinapaswa kuwa juu yetu.

Pili ligi yetu inang'arishwa na wachezaji wa kigeni, hilo ndilo tatizo.
Wazawa hatuna jambo.. Na hata hao wazawa wanaofanya vizuri, ukiwaweka pamoja wanavyocheza utacheka. 😂
Kwani si tulishakubaliana kwenye kikao cha taifa kwamba sisi hatuna tunachoweza zaidi ya kuzagamuana?
 
Ligi bora inaundwa na clubs bora, chukulia mfano hapa kwetu kuna club inaweza challenge clubs za South Africa ki uchumi, miundombimu na quality ya wachezaji?
South ni story za kale.....
Kwa Sasa wana team moja tu, mamelod zingine hakuna kitu.
Simba proved that.
 
Timu ya Taifa ni kujaza Usimba na Uyanga humo waifumue kikosi cha kwanza watoke wale wachezaji wa timu zingine wenye damu changa na wapambanaji
Timu zipi mkuu ? hata kufanya vizuri kwa Simba na yanga nikwasababu Kuna wachezaji wa kigeni. Nitajie timu inayofanya vizuri Tanzania yenye wachezaji wazawa tu utagundua wachezaji wetu Kuna shida na hawawezi kulisaidia taifa
 
Kwan wanatumia vigezo gan kuandaa hizo rank, anayevijua aweke hapa tuongee kwa facts. Tatizo jingine kwa waandish wa habari bongo sio wafatiliaji, nilitegemea wangekuja na historia na kazi ya shirika lililotoa takwimu pia vigezo wanavyotumia na mambo mengine kama hayo
 
Back
Top Bottom