Waliosema Tanzania ni miongoni mwa ligi tano bora Afrika wajitafakari

Weka list yako...acha maneno mingi chalii.

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Labda wametumia media coverage
 
Taasisi iliyotoa hizo Takwimu ni ya mchongo iko Saudi Arabia
 
Pinga takwimu kwa takwimu,sio unakurupuka na kupinga bila kufahamu vigezo vilivyotumika[emoji144]
 
Pinga takwimu kwa takwimu,sio unakurupuka na kupinga bila kufahamu vigezo vilivyotumika[emoji144]
Ligi bora inaundwa na clubs bora, chukulia mfano hapa kwetu kuna club inaweza challenge clubs za South Africa ki uchumi, miundombimu na quality ya wachezaji?
 
Acha kukariri mbona premier league ni bora ila timu ya taifa sio bora kihivyo.
 
Ww kweli hujui hata takwimu zinapatikana vipi takwimu ni overall performance na sio seasonal performance ndio maana team namba moja duniani kwa ubora ni Brazil licha ya Argentina kuchukua world cup na Brazil ndio team pekee duniani ambayo haijawahi kukosa kushiriki world cup toka ianzishwe kwa hyo Senegal kwasababu kawa bingwa basi ndio awe namba moja sio

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
Acha kukariri mbona premier league ni bora ila timu ya taifa sio bora kihivyo.
Mwaka gani umesikia timu ya Taifa ya England Ipo nje ya Top 10 Duniani!! Mwaka gani umesikia Ligi ya uingereza inashika nafasi ya tatu Kwa ubora barani Ulaya maana wao kama si wa kwanza basi wa pili. Ligi yetu ni mbovu haistahili ata kuwa ya 10 Kwa Afrika.
 
Timu ya Taifa ni kujaza Usimba na Uyanga humo waifumue kikosi cha kwanza watoke wale wachezaji wa timu zingine wenye damu changa na wapambanaji
 
Kwani si tulishakubaliana kwenye kikao cha taifa kwamba sisi hatuna tunachoweza zaidi ya kuzagamuana?
 
Ligi bora inaundwa na clubs bora, chukulia mfano hapa kwetu kuna club inaweza challenge clubs za South Africa ki uchumi, miundombimu na quality ya wachezaji?
South ni story za kale.....
Kwa Sasa wana team moja tu, mamelod zingine hakuna kitu.
Simba proved that.
 
Timu ya Taifa ni kujaza Usimba na Uyanga humo waifumue kikosi cha kwanza watoke wale wachezaji wa timu zingine wenye damu changa na wapambanaji
Timu zipi mkuu ? hata kufanya vizuri kwa Simba na yanga nikwasababu Kuna wachezaji wa kigeni. Nitajie timu inayofanya vizuri Tanzania yenye wachezaji wazawa tu utagundua wachezaji wetu Kuna shida na hawawezi kulisaidia taifa
 
Kwan wanatumia vigezo gan kuandaa hizo rank, anayevijua aweke hapa tuongee kwa facts. Tatizo jingine kwa waandish wa habari bongo sio wafatiliaji, nilitegemea wangekuja na historia na kazi ya shirika lililotoa takwimu pia vigezo wanavyotumia na mambo mengine kama hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…