Waliosoma Jitegemee Secondary School hebu ingieni hapa Tusalimiane

Waliosoma Jitegemee Secondary School hebu ingieni hapa Tusalimiane

Ivi afande Ndiamkama yupo. Yule nae alikuwa mtata sana. Mkisi ndio usiseme ile program yake '''''Mkisi program''''
 
Nakumbuka bwenge alikuwa na sira mbaaya sasa sijui binti yake kama alifata hasara ya sura ile kwa bahat mbaya sikuwah kumwona huyo binti namkumbuku pia mwl Ntibuela alikuwa poa sana, nakumbuka wakati nasoma ilikuwa mwiko mwanafunzi kwenda shule na zaidi ya shilingi elfu tano na tena kuna wakati walimu walikuwa wanatukagua.
Siku moja kuna mwanafunzi tulikuwa tunamwita mdudu nyoka alikamatwa akiwa na shilingi elfu sita akatakiwa amwite mzazi.
Jamaa kufika nyumbani akamwambia mzee wake kuwa ada aliyompa amenyang'anywa na mwalimu mmoja anaaitwa Bwenge, kumbuka wakati huo tulikuwa tunalipa ada shilingi laki moja na elfu ishirini.
Siku ya pili mzazi wa mdudu nyoka yaani mzed nyoka mwenyewe akaja shule akitaka kumwona huyo mwalimu aliyepora ada ya mwanae. Kufika ofisini akakutana na Bwenge basi mzee akaanza kumweleza bwenge kuwa ile hela ilikuwa ni ada hivyo mwanae hana kosa hivyo ampe hiyo hela akalipe hapo ndipo kazi ilianza bwenge katoa elfu sita mzazi akakataa akasema na laki na ishirini wakashindwa kuelewana akaitwa mkuu wa shule afande Massawe.
Kesi ikawa kubwa ikabidi aitwe mdudu nyoka kuulizwa jana bwenge alichukua sbilingi ngapi akasema na laki na ishirini hiyo kauli ilimchanganya mno bwenge na kwa kuwa Massawe hakutaka liende mbali ikaamriwa bwenge arudishe laki na ishirini siku hiyo nilimwona bwenge akitoa machozi unajua wakati huo hiyo hela ilikuwa nyingi sana.
Toka wakati huo ikawa hakuna kupekuana tena na nakumbuka mdudu nyoka alikuwa tajiri kwa mwezi mzima mpaka akamaliza ile ada.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mnanikumbusha mbali kweli
 
Usisikie mihogo na chachandu kwa chinga ukirudi class kusinzia tu.
My time was 1998 to 2001 olevel chini ya kanali masawe. Nilikuwa form 4 A1
 
Daah tupo aisee my Best School
1475512018947.jpg
 
halafu huyu jamaa si alianzia pale pale olevel akapanda alevel
Duh alikuja kuwa headmaster kumbe
Mbonabucha sijui yuko wapi na yule mama wa skauti alikuwa mnoko kama nini
Mbonabucha alishafariki 2003 au 2002 (RIP). Mwalimu wangu wa darasa na physics ya form1&2
 
Namkumbuka afande bruno siku king'ora cha saa sita kimelia ili twende kwenye kwata halafu tukachelewa kidogo kwa sababu ya kukopi homework alivofka na kusimama mlangon tu ilikuwa ni kichurachura hadi uwanja wa damu kilichotokea hakutoa amri ya sisi tusimame acha watu waruke hadi watu wakafka mwisho wa uwanja wa damu kwenye ile mitaro mirefu watu wakabak wakirukaruka tu sehem moja na hawaend mbele niliogopa sana kama angesema turuke ile mitaro lakini akasema tugeuke daaaahhh
 
Nimesoma muda huu kwenye FB kwamba yule mwalimu mtaalam wa adhabu tatanishi (Mr. Ndeha) alishafariki dunia.

Mwenye kumfahamu huyu mwalimu, unamkumbukaje?
Ndeha alishanipa bakora tatu takatifu wkt nipo form4 mwl wa darasa mama shalua alinisakizia kwake eti nimeshindikana
 
kadoda11 huoni jamaa anasema Jitegemee ni kwa wale waliofail form four ndo wanaenda pale hajui wengine walifaulu msingi ila wakaona haina haja ya kwenda government school wakaishia Jitegemee
Mimi ni mmojawapo nilichaguliwa government school mzazi akaona miyeyusho akapiga biti utasoma hapo
mkuu hawa ni form six wa mwaka gani?.nimeipenda sana hii picha.naona swala la usafi si jambo la kuhoji.
 
Wadau kwa waliosoma Jitegemee enzi hizo na pia wale waliosoma Dar miaka ya 90 kuna wahenga maarufu sana wafuatao sijui wako wapi miaka hii,
a) Pomp Duu- Huyu alikuwa anapendelea sana muziki,alikuwa rasta kimtindo halafu alikuwa mshiriki mzuri sana wa shughuli nyingi za pale shuleni.
b) Adam Kimanyo- Huyu naye alikuwa maarufu san enzi hizo, siku za mechi na timu za shule nyingine alitumika sana kwenye kamati za ufundi. Ilikuwa ngumu kwenda kwenye mechi bila kumshirikisha.
c) Edd Cocks- Huyu dogo alikuwa maarufu sana na pia machachari kweli.habari zote za mujini alikuwa anazijua.
d)Mwalimu Kidenya- Huyu mwalimu nae alijipatia umaarufu sana kwani alikuwa yupo serious sana.

Karibuni
 
Back
Top Bottom