Waliosoma Jitegemee Secondary School hebu ingieni hapa Tusalimiane

Kuna afande babu mbeba mafunguo kila jioni yeye ndo anafunga madarasa yote pia alikuwa sana ofisi ya Head master Mkisi sijui kama bado yupo
 
Wapi MTOKAMBALI, KWEMBE, NDIYAMUKAMA, NYAHONYO, NZIKU, CHAO bila kuwasahau walimu wng wa darasa wa 4m 5 na 6(HGE) 2011-2013 NGAMESHA na KINYERO..
Nyahonyo alikuwa teacher wetu wa darasa baada ya afande Biseko

Kuna pedeshee Mdendemi a.k.k Madilu yeye ni biashara ya vitabu vyake tu
 
Da nimekumbuka mbali sana... mi nilikuwa kilanja enzi za massawe na mang'wela akiwa discipline master nilikuwa mnoko wanafunzi walinichukia sana nilivaa rank nyekundu pamoja na beji hadi nje ya shule.
 
mwee. jaman mpare wawatu rip
vipi mama lyimo yupogo?
 
hahHAhaa kwahiyo bwenge hakummaind Huyo Dogo
 
Nilikuwa nimepinda wazazi wakanipeleka hiyo shule hostel wakiamini nitakuwa na nidhamu miezi sita nikapinda zaidi wakaona isiwe taabu nikahamishwa.
 
Jiteute 2004 kuna mwizi tulimnasa Makame Dormitory aisee tukapiga kinyama alikua anatusumbua sana huyu Bwana Kesi ikafika kwa Wajadi akasema tulitakiwa tunapompeleka pale awe amevunjika miguu tyr. Kwata ilikua safi sana Ila binafsi vipindi vya mchana nilikuwa sivipendi kinoma [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] good memories.
 
Mimi ni in-take ya O level 1996-1999 sasa kuna siku tulikuwa tunapiga sana kelele darasani, maafande 4 wakatuvamia darasani. Sasa mimi dawati langu lilikuwa la mwisho kabisa, na mlango wa darasa ulikuwa mmoja nyuma ya darasa yaani, kama milango ya magari ya zamani ya kubeba abiria, Kia. Hivyo, mara nyingi maafande wakituvamia mimi na masela wangu tunachomoka kiurahisi sana kwa kuwa dawati letu lilikuwa nyuma kabisa na karibu na mlango.

Sasa siku hiyo maafande wametuvamia wakaingia darasani 4 na mikwaju ya kutosha, sasa mimi kama kawaida yangu, nikawasubiri hile wamefika kati ya darasa mimi nikawaambia masela wangu jamani tusepe, masela wakaogopa. Basi mimi nikanyata mdogo mdogo nikachomoka class basi hile nageuka tu nakutana uso kwa uso na afande mmoja nje kumbe alikuwa anavuta sigara. Ilikuwa kama movie vile. Jamaa akanidaka akaniongiza ndani, wacha nipewe kichapo. JITE imenifunza mengi sana, I am who I am because of JITE UTE...
 
Hyo shule imenifanya nipende Jeshi na niwe mzalendo wa kweli.. Pili imenifundsha kuwa smart.. Kimavazi na kichwani pia.. Tatu hyo shule imenifunza uvumilivu sana way back 2mekula sana joro! Nimenyuti sana juu ya paa za chooni.. Walimu wengi hawapo.. Wapo wapya wapya tu..

Updates..
Mkungu tree limeshushwa hall kubwa pale.

Kumejengwa uwanja mkubw wa mpira

na mambo mengne mengi.. Last time nilienda mwaka jana.. Nilipita na escort kufanya ukaguzi Mgulani..

Namkumbuka sana kumalija,mkisi..,ndiamkama!,MASEMELE, na wengne wengi.. Almost 6 yrs nilikuw pale.. 2mepiga sana makondakta pale uhasibu..!

Mefanya sana majanga.. Adhabu nisiyoisahau ni kupigwa viboko 100 ,kuchota madumu 60,na kusafisha pale ktk karo almaarufu kama "usikae Hapa"..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…