Waliosoma Jitegemee Secondary School hebu ingieni hapa Tusalimiane

Waliosoma Jitegemee Secondary School hebu ingieni hapa Tusalimiane

Kuna afande babu mbeba mafunguo kila jioni yeye ndo anafunga madarasa yote pia alikuwa sana ofisi ya Head master Mkisi sijui kama bado yupo
 
Wapi MTOKAMBALI, KWEMBE, NDIYAMUKAMA, NYAHONYO, NZIKU, CHAO bila kuwasahau walimu wng wa darasa wa 4m 5 na 6(HGE) 2011-2013 NGAMESHA na KINYERO..
Nyahonyo alikuwa teacher wetu wa darasa baada ya afande Biseko

Kuna pedeshee Mdendemi a.k.k Madilu yeye ni biashara ya vitabu vyake tu
 
Da nimekumbuka mbali sana... mi nilikuwa kilanja enzi za massawe na mang'wela akiwa discipline master nilikuwa mnoko wanafunzi walinichukia sana nilivaa rank nyekundu pamoja na beji hadi nje ya shule.
 
Hahahaha kweli aisee. Mwanae alikuwa na wajihi kama baba yake. Cha kushangaza walikuwa wanaishi wawili tu kwenye ile nyumba pale nyuma ya ofisi ya Massawe.

Mrimi Mnandi alifariki yes, nakumbuka last time nakutana naye alikuwa anaandaa Reunion ya Jitegemee na alinisihi sana nije ila bahati mbaya alinikuta na ticketi mkononi hivyo sikuweza kuhudhuria sherehe ile. Yule Mpare alijua kutengeneza pesa. Mwaka mmoja baadaye ndo akafariki dunia. RIP.

Ila wadau wengi pale wameshatangulia kujibu kwa Mungu. Mungu awarehemu.

mwee. jaman mpare wawatu rip
vipi mama lyimo yupogo?
 
Nakumbuka bwenge alikuwa na sira mbaaya sasa sijui binti yake kama alifata hasara ya sura ile kwa bahat mbaya sikuwah kumwona huyo binti namkumbuku pia mwl Ntibuela alikuwa poa sana, nakumbuka wakati nasoma ilikuwa mwiko mwanafunzi kwenda shule na zaidi ya shilingi elfu tano na tena kuna wakati walimu walikuwa wanatukagua.
Siku moja kuna mwanafunzi tulikuwa tunamwita mdudu nyoka alikamatwa akiwa na shilingi elfu sita akatakiwa amwite mzazi.
Jamaa kufika nyumbani akamwambia mzee wake kuwa ada aliyompa amenyang'anywa na mwalimu mmoja anaaitwa Bwenge, kumbuka wakati huo tulikuwa tunalipa ada shilingi laki moja na elfu ishirini.
Siku ya pili mzazi wa mdudu nyoka yaani mzed nyoka mwenyewe akaja shule akitaka kumwona huyo mwalimu aliyepora ada ya mwanae. Kufika ofisini akakutana na Bwenge basi mzee akaanza kumweleza bwenge kuwa ile hela ilikuwa ni ada hivyo mwanae hana kosa hivyo ampe hiyo hela akalipe hapo ndipo kazi ilianza bwenge katoa elfu sita mzazi akakataa akasema na laki na ishirini wakashindwa kuelewana akaitwa mkuu wa shule afande Massawe.
Kesi ikawa kubwa ikabidi aitwe mdudu nyoka kuulizwa jana bwenge alichukua sbilingi ngapi akasema na laki na ishirini hiyo kauli ilimchanganya mno bwenge na kwa kuwa Massawe hakutaka liende mbali ikaamriwa bwenge arudishe laki na ishirini siku hiyo nilimwona bwenge akitoa machozi unajua wakati huo hiyo hela ilikuwa nyingi sana.
Toka wakati huo ikawa hakuna kupekuana tena na nakumbuka mdudu nyoka alikuwa tajiri kwa mwezi mzima mpaka akamaliza ile ada.
hahHAhaa kwahiyo bwenge hakummaind Huyo Dogo
 
Nilikuwa nimepinda wazazi wakanipeleka hiyo shule hostel wakiamini nitakuwa na nidhamu miezi sita nikapinda zaidi wakaona isiwe taabu nikahamishwa.
 
Jiteute 2004 kuna mwizi tulimnasa Makame Dormitory aisee tukapiga kinyama alikua anatusumbua sana huyu Bwana Kesi ikafika kwa Wajadi akasema tulitakiwa tunapompeleka pale awe amevunjika miguu tyr. Kwata ilikua safi sana Ila binafsi vipindi vya mchana nilikuwa sivipendi kinoma [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] good memories.
 
Mimi ni in-take ya O level 1996-1999 sasa kuna siku tulikuwa tunapiga sana kelele darasani, maafande 4 wakatuvamia darasani. Sasa mimi dawati langu lilikuwa la mwisho kabisa, na mlango wa darasa ulikuwa mmoja nyuma ya darasa yaani, kama milango ya magari ya zamani ya kubeba abiria, Kia. Hivyo, mara nyingi maafande wakituvamia mimi na masela wangu tunachomoka kiurahisi sana kwa kuwa dawati letu lilikuwa nyuma kabisa na karibu na mlango.

Sasa siku hiyo maafande wametuvamia wakaingia darasani 4 na mikwaju ya kutosha, sasa mimi kama kawaida yangu, nikawasubiri hile wamefika kati ya darasa mimi nikawaambia masela wangu jamani tusepe, masela wakaogopa. Basi mimi nikanyata mdogo mdogo nikachomoka class basi hile nageuka tu nakutana uso kwa uso na afande mmoja nje kumbe alikuwa anavuta sigara. Ilikuwa kama movie vile. Jamaa akanidaka akaniongiza ndani, wacha nipewe kichapo. JITE imenifunza mengi sana, I am who I am because of JITE UTE...
 
Hyo shule imenifanya nipende Jeshi na niwe mzalendo wa kweli.. Pili imenifundsha kuwa smart.. Kimavazi na kichwani pia.. Tatu hyo shule imenifunza uvumilivu sana way back 2mekula sana joro! Nimenyuti sana juu ya paa za chooni.. Walimu wengi hawapo.. Wapo wapya wapya tu..

Updates..
Mkungu tree limeshushwa hall kubwa pale.

Kumejengwa uwanja mkubw wa mpira

na mambo mengne mengi.. Last time nilienda mwaka jana.. Nilipita na escort kufanya ukaguzi Mgulani..

Namkumbuka sana kumalija,mkisi..,ndiamkama!,MASEMELE, na wengne wengi.. Almost 6 yrs nilikuw pale.. 2mepiga sana makondakta pale uhasibu..!

Mefanya sana majanga.. Adhabu nisiyoisahau ni kupigwa viboko 100 ,kuchota madumu 60,na kusafisha pale ktk karo almaarufu kama "usikae Hapa"..
 
Back
Top Bottom