nakumbuka vizuri maisha ya JITE, siwezi kuwasahau Masemele, Madilu mzee wa tai za vitobo, Babu Mafunguo, Mrimi Mnandi, Afande Ismaili, Afande Bruno, Afande Tall, mpiga picha P.DIDI, bila kusahau Mkisi Program
Mkuu tumesoma wote, ila nilikuwa mchepuo wa Sayansi.....Member wa Jitegemee kuanzia 1993 mpaka 1996
Mkisi kaanzia siku nyingi kufundisha civics na misifa yake
Wakati tunasoma pale Bwenge alikuwa na binti yake anasoma palepale
Nakumbuka tuliifunga Tambaza that day ndo balaa likaanza. Kwa wasiofahamu ni kwamba Vurugu ile ndo ilipelekea Tambaza kubadilisha mchepuo kutoka Olevel to Alevel. Nilikuwepo ktk wanafunzi waliokwenda Tambaza kuwatambua vinara wa vurugu.Mkuu kabanga ni kweli mkuu shule sio kabisa siku hizi sio ile ya akina Wajadi naMassawe ambao waliiweka juu sana shule
Wakati wa ugomvi wa Jiteute naTambaza wakati huo Tambaza bado ikiwa na olevel uliopelekea nafikiri ni konda mmoja kufa mitaa ya Keko kweli Jiteute ilikuwa shule enzi hizo.....
Alikuwa Mwalimu wangu wa Darasa. Alikuwa ananimaind sana maana nilikuwa natengua maamuzi yake mengi sana (nilikuwa Kiranja) ya kionevu. Alipenda totoz hivyo wakimzingua darasa zima mnakuwa msambweni.Mrimi ameshatangulia mbele ya haki mkuu. Bruno tumbo mzee wa beetle!! Hahahaa...lafudhi ya huyu jamaa ni vituko aise.
Kuna safari moja tulikwenda Manyara kisha Ngorongoro same trip. Tuliongozana naye na Wajadi kama wakuu wa msafara, kuna dogo mmoja (siku hizi ras maarufu ana kiwanda cha kutengeneza vikoi) alikamatwa na puli kumi za bangi pale Mto wa Mbu. Alizichukua Wajadi kama kidhibiti ila hazikufika Dar, jamaa alizipuliza zote....Mkuu Mrimi Mnandi alitangulia mbele za haki Huyu jamaa alikuwa bingwa wa kuandaa Study Tour
Hahahaha nimecheka hapo kwenye Bold mkuu. Inawezekana tunafahamiana ila bahati mbaya haya masecurity yetu JF hayavunji ukuta wa kujua who is who.Mkuu Paw mbona na mimi nilikuwa mchepuo huo huo wa Science
Kweli mkuu Jiteute ilikuwa enzi za Massawe na akina Bwenge na yule mama wa Skauti nimemsahau jina na vipaji lukuki na nkumbuka matokeo yetu ya Form four 1996 ndo yalikuwa ya mwisho mazuri kwa upande wa Olevel na baada ya hapo na baada ya Massawe kuondoka shule ikaanza kuporomoka kutokana na utozi mwingi
Tufahamiane Mkuu Paw
Hahahaha nimecheka hapo kwenye Bold mkuu. Inawezekana tunafahamiana ila bahati mbaya haya masecurity yetu JF hayavunji ukuta wa kujua who is who.
Yule mama anaitwa Anyitike. Nadhani unamkumbuka, pia nilikuja kupata taarifa kuwa afande Kihimbi alikuja kufariki ghafla baada ya kuanguka akikimbiza denti Smart Area. Kifua kilikuwa amekopesha kampuni ya sigara.
Unakumbuka zile bakora zilizokuwa zinaletwa na fuso? Dah ile shule ilitupatia nidhamu za maisha kweli kweli
Yule mwalimu bishoo alikuwa anaitwa Mpeta (nadhani ni chemistry)..... Mama Mnzava ndiye alinifundisha Biology. Nakumbuka Ktk Reproduction nusu ya mabinti walitega shule siku hiyo....Year uko right mkuu ni Mama Anyitike na wanasema yule mama hakuwahi kuwa na mtoto ndo maana alikuwa mkali vibaya sana nanasikia pia Mama Lyimo alishafariki pia mkuu
Unamkumbuka yule mwalimu wa Biology alikuwa akija darasani hashiki chaki kwa ajili ya kuogopa kuchafuka achana na Mama Mnzava aliyekuwa bingwa wa Bios sanapale Jiteute
halafu unakumbuka Form Four moja ya biashara nafikiri ni D1 wakati huo sisi tukiwa Form IV C1 ilikuwa ya matoz wakiingia darasani wana perfume na vitana na brush wakitoka ile mchana huwezi jua ndo wanaingia au wanatoka maana ni wasafi mbaya na walimu walikuwa washajua darasa lile ni la matoz so wakiingia kufundisha waelewe wasielewe hakuna anayejali
Nimekutajia na darasa mkuu unaweza pata picha
Nakuja PM mkuu Paw
Yule mwalimu bishoo alikuwa anaitwa Mpeta (nadhani ni chemistry)..... Mama Mnzava ndiye alinifundisha Biology. Nakumbuka Ktk Reproduction nusu ya mabinti walitega shule siku hiyo....
Kumbuka darasa ambalo lilishawahi kumtoa baruti afande Tall (Form Four)
Yeah namkumbuka yule mama. Alikuwa mnataji sana aisee. Jinale limenitoka maana hakuwahi kutufundisha sisi. Mabada unamkumbuka? Mzee wa Fizikia.Mkuu achana na Mpeta kuna mama pia wa Bios alikuwa bishoo mbaya yaani hashiki chaki na hataki kuchafuka na hamalizi hata muda wake wa kipindi
Sisi tulikuwa tukiingia mchana tukijua siku hiyo kuna Bios tunawahi asubuhi vipindi vya mama Mnzava tunakula shule ya uhakika na huyo mama bishoo akiingia tunasikiliza tuu hakuna hata kuandika lolote
Nimekumbuka sana Mkuu nyie mlikuwa balaa
Ila tumekula sanastick aise za Jiteute dah ile shule ilinifundisha mengi sana
Yeah namkumbuka yule mama. Alikuwa mnataji sana aisee. Jinale limenitoka maana hakuwahi kutufundisha sisi. Mabada unamkumbuka? Mzee wa Fizikia.
Darasa letu tangu january hadi desemba halikuwahi kuwa na wanafunzi wote kufika kwa pamoja, ajabu tulifanya vizuri sana kwenye papers. Namkumbuka JINIAZ Jeremiah alitutesa kwenye sayansi kinoma ila National alipata namba isiyo njema kuitaja hadharani. Nilikutana naye yupo AIRTEL sijui kama bado anapiga kazi pale
Yeah namkumbuka yule mama. Alikuwa mnataji sana aisee. Jinale limenitoka maana hakuwahi kutufundisha sisi. Mabada unamkumbuka? Mzee wa Fizikia.
Darasa letu tangu january hadi desemba halikuwahi kuwa na wanafunzi wote kufika kwa pamoja, ajabu tulifanya vizuri sana kwenye papers. Namkumbuka JINIAZ Jeremiah alitutesa kwenye sayansi kinoma ila National alipata namba isiyo njema kuitaja hadharani. Nilikutana naye yupo AIRTEL sijui kama bado anapiga kazi pale
Mkuu achana na Mpeta kuna mama pia wa Bios alikuwa bishoo mbaya yaani hashiki chaki na hataki kuchafuka na hamalizi hata muda wake wa kipindi
Sisi tulikuwa tukiingia mchana tukijua siku hiyo kuna Bios tunawahi asubuhi vipindi vya mama Mnzava tunakula shule ya uhakika na huyo mama bishoo akiingia tunasikiliza tuu hakuna hata kuandika lolote
Nimekumbuka sana Mkuu nyie mlikuwa balaa
Ila tumekula sanastick aise za Jiteute dah ile shule ilinifundisha mengi sana
Kulya hapana aise zile zilikuwa sio adhabu bali mauajiHahahahaaa....na adhabu kali kali kama push up uwanja wa damu pale...vipi siku hizi, mwanao shule anasoma utakubali atiwe stick kama za Wajadi au Ndyamukama?!
ebana jamaa sijui wako wapi tuliishi nao sana kota pale za bandari!kuna day moja mzee nimeona mizinguo na uswahilini nna gem ya soka,nikapiga hesabu nijikatae,nikaenda kuzuga pale zilipokua zinawekwa barua za wanafunzi karibu na geti,kuchek huku na kule kweupe nikatoka nduki ya hatari ile kufika getini uso kwa uso na wajadi na alikua katoka kula vitu vyake!kilichofuatua sikilizia usibanduke ni noma!
hapana martin mkisi hayupo jitegemee kwa sasa... amepanda cheo na kuwa luten kanali na sasa ni mkuu wa kambi ya Ruvu Jkt. Mkuu wa sasa hapo jite bado sijamfaham
kumbe unawakumbuka wale madogo.....halafu ktk kundi lao kulikuwa na dogo mwingine mtukukutu sana kwa jina la abuu,alikuwa anaishi kinondoni.kuna siku moja 2001 nilipiga feni home na kwenda kuliuza kkoo pale round about kwa wauza redio na vifaa vya umeme vilivyo tumika.lengo hasa ilikuwa ni kusaka mshiko wa kuingia ktk show ya manduli mobb kule ktk ukumbi wa jkt unaotumika kufanyia sherehe mbalimbali za kijamii.na ktk show hiyo walitangaza uwepo wa juma nature na duly sykes.basi nikaawachia wale jamaa wa kkoo ile feni yangu kwa ahadi kwamba after two days nipite kuchukua changu kama elfu 30 hivi.kila nikitoka shule jioni napita kkoo kuulizia mshiko wangu,jamaa wakawa wananizungusha tuu.baada ya wiki moja nikakata shauri.nikampa mchongo mzima abuu.abuu akaniambia mbona hiyo issue ndogo tuu.aka-organize watukutu wenzie kama watano hivi ili tukafanye ambush kkoo.ile jioni tunatoka tu jite,tukajikusanya na kudandia daladala hao kkoo kufata haki yangu.kilicho tokea dont miss part II.
Dah mmenikumbusha kitambo nyie raia. Kuna afande mmoja alikua anaitwa Bruno jamaa alinitupiaga stick ya kichwa kisa Mwalimu Mleli kamuambia anishughulikie, nikaona hapa jamaa ataniua nikatoka nduki mbaya smart Area pale nilikipia speed ya hatari kama Hussein Bolt. Ticha Mleli akaanza kupiga kelele kama za mwizi vile maafande wote wakaniungia na stick kama mia nane ivi mikononi.
Nilitoka nduki kufika mbele wakamshtua Kamanda wao wa Mbio anaaitwa Afande Kiimbi (RIP), ebana jamaa anatoka nduki yule sijawahi ona...dakika sifuri niko mikononi mwa maafande...Kilichotokea............Tega sikio Part II. Tehe tehe
Jitegemee Sec.(JIte-Wute )Member 1996-1999
Mwaka 2007 nikiwa ukingoni kumaliza A level, nakumbuka kipindi nikizurura nje wakati wenzangu wakiwa ktk mkisi program, nilikutana na Major Mkisi, kipindi hicho mwenyewe akijiita major msomi, major handsome, alinikamata na kunipa adhabu ya kijeshi. Lakini sasa hivi Mkisi kwisha habari yake. Major Kessy ndio mkuu wa sasa hivi pale Jiteute!