Waliosoma Jitegemee Secondary School hebu ingieni hapa Tusalimiane

Waliosoma Jitegemee Secondary School hebu ingieni hapa Tusalimiane

Nakumbuka tuliifunga Tambaza that day ndo balaa likaanza. Kwa wasiofahamu ni kwamba Vurugu ile ndo ilipelekea Tambaza kubadilisha mchepuo kutoka Olevel to Alevel. Nilikuwepo ktk wanafunzi waliokwenda Tambaza kuwatambua vinara wa vurugu.

Mkuu hivi beef kati ya Tambaza na Jite au Azania na Jite Ipi ilikuwa hatari zaidi?
 
namkumbuka sana marehemu mbonabucha yule mlemavu wa mguu alikua mtaalam sana!wapi kaboka mchizi jina lake halisi limenitoka kidogo yule ticha wa civics

ha ha ha ha ha bila shaka atakuwa ni clavery alikuwa anafundisha civics na b'keeping kwa 4m 1 na 2
 
Duu! Nilikuwa hapo advance...siwezi kusahau siku ambayo Mwl wajadi alinikamata navuta sigara hostel...yaaaani walinichangia maafande tall, short, white na wengine siwakumbuki mpaka discipline office...
 
zile stiki zilikua ni noma zinatoka maporini kule yani siwezi kumsahau wajadi nilikula stiki siku hiyo aliyonikamata getini siku tatu nilikua siwezi kukaa kwenye kitu kigumu!nikamwambia mshua mi ile shule tena basi !washua wetu wakitambo kile siunawaelewa tena akaniambia utasoma hapo hapo vaa uende shule,ila ndiyamukama alikua hatari sana nasikia wale waliitangulia kumaliza walimvunja mguu lakini bado balaa lake tuliliona!1998 na kuendelea

Mkuu zile stiki inasemekana zilikuwa zinatoka Singida.
Kuhusu Wajadi we acha tu nikiwa Hostel alishawahi kutupa adhabu (Tifu) mara tatu na mara zote baada ya kutoka hapo. tulikuwa hatuwezi kukunja miguu wala mikono Nakumbuka nilikuwa nikimaliza adhabu ya Wajadi nikienda Sanga Hall kupata chakula badala ya mkono kufuata mdomo ilikuwa inabidi mdomo uufuate mkono na Hapo kuchuchumaa ilikuwa marufuku
 
Mkuu hivi beef kati ya Tambaza na Jite au Azania na Jite Ipi ilikuwa hatari zaidi?
Ile ya Tambaza nilikuwa njuka. tuliwahi kumalizana nayo mapema sana. Na Tambaza kipindi kile walijenga kuiheshimu JITE kwani walijua kitakachowatokea...

Ila nikiwa Kidato cha Nne kulizuka ugomvi huo wa Azania na Jite. Chanzo kilikuwa ni pale Don Bosco katika mechi ya Mpira wa kikapu. Mechi yenyewe ilikuwa fainali kwa shule za Dar. Timu zote mbili zilikuwa na kiwango cha juu. Haikutabirika nani atashinda.

Balaa lilianzia kwa mashabiki ambapo baadhi ya watemi wa Azania walitaka kulazimisha ushemeji kwa dada zetu wa Jiteute. Wakawa wanawasumbua na kuwalazimisha kukubaliana nao. Baada ya kujaribu kuingilia kati ndo balaa likaanzia hapo na mpira ukavunjika. Jite tulikuwa wachache ila tulifanikiwa kuwatawanya Azania waliokuwepo pale na likaongezeka kundi lao kutoka shule ndo balaa likazidi. Kumbuka ugomvi ulianza saa 12.45 jioni hivyo haikuwa rahisi kusaka suluhu mapema.

Kwa mshangao kesho yake tunafika shule tunakutana na mabinti ambao wamechanjwa viwembe na kuporwa mabegi na Azania. Kilichotokea hapo ni balaa kwani Jiteute wengi na Azania waliishia kukamatwa na kulazwa vituoni. Massawe alihangaika sana kulimaliza lile. Nilikuwepo kwenye timu ya usuluhishi ambapo tulienda Azania kupeleka ujumbe wa amani na maridhiano, ingawa walijaribu kutufanyia vurugu hatimaye tulifanikiwa kuonana na serikali ya wanafunzi na Waalimu na ugomvi ukaishia pale.

Ila vurugu ile sitaisahau maana ilikuwa ni balaa kuliko ya Tambaza

 
Paw,

Mkuu Paw inaonekana wewe ulikuwa mtata sana
Kuhusu beef za Jite n a Azania nakumbuka nyingine ilikuwa kama sikosei ni 2007 au 2008 ilianza tu kimzaha mzaha ilikuwa ni pale pele Don Bosco kwenye mechi ya Basket ball kabla ya mechi kuanza walipanda jamaa wa kuimba wa kwanza kupanda jukwaani na kuimba alikuwa jamaa wa Azania alianza kuimba na kuwadiss sana washikji wa Jite baada ya jamaaa wa Azania kushuka akapanda jamaa wa Jite naye akawadiss sana Jamaa wa Azania kuona hivyo jamaa wa Azania wakawa wamechukia wakaanzisha fujo wakawa wamempiga jamaa wa Jite wakamvunja meno ya mbele (hayakutoka yote ila tu yalivunjika vipande) baada ya vurugukukua kuna jamaa wa Jite alimchoma dogo mmoja wa Azania na sindano ya kushonea viatu kwenye jicho halafu akazungusha ile sindano jamaa akawa amemtoboa jicho kabisa daah ilikuwa noma sana kesho yake Watoto wa Jite walioonekana Kariakoo walichzea kichapo cha hatari na wale wa Azania walioonekana ande za Tandika nao walichezea kichapo kama kawaida.
 
Last edited by a moderator:
duuh.... huyu mrimi si ndo yule aliyekuwa anatengeneza tuvitabu kama twa Nyambali Nyangwine .. aiseee!
!! sikujua kama alikufa.
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Salama
Ndo huyo huyo ila alisha rest in peace

Mi namkumbuka Masawe.
Alikuwa anapenda kazi yake sana.
Anawahi kazini kiiila siku.

Jumatano tunachagua Queen na King.
yaani wasafi kuliko wote.
kisha anawapa zawadi.
sometimes anawapa ofa ya chai Steers au ofisini.
Inategemea...
Kali zaidi siku ya birthday yake moja iligonga siku ya jumatano...
tulimwimbia hepbasdei tu yuu assemble.
kisha zikashushwa box za mapipi tukagaiwa kuanzia form one mpaka six.
aisee yule jamaa...ni peace sana.
Nayakumbuka mapipi hadi leo. teh teh
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Mtamile,

Nilisoma na mtoto wa Lowassa.
Alikuwa anaitwa Emanuel Lowasa.
HGE ya mwaka 2001.
Tulipiga nae kwata mpaka mwisho.
jamaa sijui yuko wapi nowadays.
 
Nilisoma na mtoto wa Lowassa.
Alikuwa anaitwa Emanuel Lowasa.
HGE ya mwaka 2001.
Tulipiga nae kwata mpaka mwisho.
jamaa sijui yuko wapi nowadays.

cha ajabu hata kama alipata div 0,ukiuliza sasa hivi yuko wapi utaambiwa tayari ana gamba la masters from a certain university in europe or USA na sasa ni mkurugenzi ktk kampuni kubwa au shirika nyeti nchini.usicheze na watoto wa wakubwa the caliber of lowassa.
 
Mmeongea yooote mmesahau mr rite na pale loliondo eti cj iz kuna uwanja wa mpira tulivyoenda jwenye alumni tuliwafunga nadenti waliopo muchezo yote
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Mmeongea yooote mmesahau mr rite na pale loliondo eti cj iz kuna uwanja wa mpira tulivyoenda jwenye alumni tuliwafunga nadenti waliopo muchezo yote
Rite namkumbuka sana.
Komando kutoka Zenji. Jamaa alikuwa mkimya, mpole ila mtata sana akikuta denti ananyanyaswa.

Aliwahi kumpigisha magoti Bwenge mbele ya macho yangu.

Alikuwa akitembea amekakamaa all the way

 
Rite namkumbuka sana.
Komando kutoka Zenji. Jamaa alikuwa mkimya, mpole ila mtata sana akikuta denti ananyanyaswa.

Aliwahi kumpigisha magoti Bwenge mbele ya macho yangu.

Alikuwa akitembea amekakamaa all the way


Paw mtoto wake nae alikuwa amekakamaa kama baba yake natulikuwa nae class
Sijui yule mwalimu yuko wapi kwa sasa namtoto wake
Hivi Mrimi asharest in peace dah namkumbuka sana aise maana alikuwa anauza sana vitabu vyake
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Paw
jitegemee ya sasa kimiundombinu ipo vizuri zaidi kuliko miaka ile.i keep wondering why its current academic parformances dont reflect to the good environment it has.hakika naamnini shule sio uzuri tu wa majengo yake.
 
Paw mtoto wake nae alikuwa amekakamaa kama baba yake natulikuwa nae class
Sijui yule mwalimu yuko wapi kwa sasa namtoto wake
Hivi Mrimi asharest in peace dah namkumbuka sana aise maana alikuwa anauza sana vitabu vyake
Hahahaha kweli aisee. Mwanae alikuwa na wajihi kama baba yake. Cha kushangaza walikuwa wanaishi wawili tu kwenye ile nyumba pale nyuma ya ofisi ya Massawe.

Mrimi Mnandi alifariki yes, nakumbuka last time nakutana naye alikuwa anaandaa Reunion ya Jitegemee na alinisihi sana nije ila bahati mbaya alinikuta na ticketi mkononi hivyo sikuweza kuhudhuria sherehe ile. Yule Mpare alijua kutengeneza pesa. Mwaka mmoja baadaye ndo akafariki dunia. RIP.

Ila wadau wengi pale wameshatangulia kujibu kwa Mungu. Mungu awarehemu.

 
Mkuu Paw inaonekana wewe ulikuwa mtata sana ....
Hahahaha hapana bwana.
Nilikuwa tu jasiri maana sijawahi kuanzisha ugomvi wala kujeruhi mtu shekhe.

Nilikuwa siku zile nahudhuria mafunzo ya martial arts hivyo sikupaswa asilani kupigana na mtu. Ndo maana nilikuwa jasiri kwenda frontline bila kudhurika.

 
Kweli mkuu Paw maana nasikia mpaka Mama Lyimo kasharest in peace
Kuna mwalimu mmoja wa Geography alimuwa mzuri sananafikiri mama Mruma sijui yuko wapi kwa sasa kadoda11 sijui ni kwa nini kwa kweli maanamazingira ya wakati wetu library ilijengwa wakati tuko pale namazingira hayakuwa mazuri kimajengo wala kwa nje ila matokeo yalikuwa mazuri sana ila kwa sasa kila kitu kipo matokeo ya Jiteute ni balaa
 
Last edited by a moderator:
....mazingira ya wakati wetu library ilijengwa wakati tuko pale namazingira hayakuwa mazuri kimajengo wala kwa nje ila matokeo yalikuwa mazuri sana ila kwa sasa kila kitu kipo matokeo ya Jiteute ni balaa
Niliangalia matokeo ya mwaka jana
S0496 JITEGEMEE SECONDARY SCHOOL

DIV-I = 1 DIV-II = 2 DIV-III = 26 DIV-IV = 210 FLD = 443

Nilitamani kulia. Nilikutana wakati huo na mwanafunzi mmoja wa kidato cha tatu ambapo aliniambia kwamba sasa ili kuvuka darasa inabidi mwanafunzi asiwe below 20 wastani wa alama zake.

Mnakumbuka below 50?

 
Back
Top Bottom