Waliouza madafu kwenye futari ya Ikulu wahojiwa, mmoja ni mwanafunzi wa Chuo cha NIT. Ni wauza madafu kweli?

Ninavyojua Mimi,

Kila Mwanaume ni askari,

Ukraine kiliponuka, Eti wanaume nao wakajaribu kukimbia, wakakumbushwa WAJIBU wao.
 
Yaani kwa elimu hii ya vyuo vya Tanzania usome huku unauza madafu ambayo hujui mnunuzi atakuja kununua muda gani? Huko chuo NIT anakwenda saa ngapi?
 
Hivi vyuo vya kibongo unapata wapi muda wa kukariri madesa,course work na kwenda kufanya biashara ya kuuza madafu ambayo hujui mnunuzi atakuja kununua muda gani? Au wakiyafikisha hapo A-Z yananunuliwa yote kila siku?
 
Kwa nini unakuwa na uhakika hivyo au wewe ndio upo idarani na hujawaona? Nikuhakikishie hata idarani siyo wote wanajuana
Inategemea na Idara.. Idara ya TISS na M-IT inaweza ikawa na scenario kama yako.. same as Special units ktk baadhi ya idara kama PCCB na DCEA.. pia CID hawa wote wakikutana ktk harakati mbalimbali za Maisha wanaweza wasijuane.. but MAIN purpose ni same.
 
Samahani Mkuu hii Pettu issues yako kama Ulivyoandika hapa ni Kiswahili, Kijerumani, Kiingereza au Kizanaki?
 
Mkuu,

Hata mimi nimejiuliza sana, tunahakikishaje kuwa hawa si wauza madafu wa kawaida tu walioalikwa Ikulu kuuza madafu na rais wao mpenda madafu akaona vizuri kupiga nao picha?
Kama ni mtaalam wa Behavior Detection utagundua si wana IDARA.. simply.

Pia muda ni mwalimu mzuri.. hao wamepewa fedha kiasi kikubwa.. tutegemee kutoweka hapo (Wamepata mtaji).

Ikiwa wataendelea kubaki hapo basi Jibu linaweza kuwa ni kweli wana wa IDARA.. but wait.....

Ukirefer maelezo yao ni kwamba kuna mmoja hapo ana MWAKA mzima anauza madafu... sidhan kama hiyo sehem ikawa na Information harvester wa kutumia mwaka mzima akiharvet taarifa.. never. Hivyo tunarud na conclusion kwamba ni mwananchi wa kawaida..
 
Tanzania kila raia ni askari ..ila kuna walio ajiriwa na wasio ajiriwq..hata wewe mleta mada ni sehemu moja wapo ya hao..
 
Idara ina watu wa kila aina..ila kama usemavyo
 
Mbona unajieleza sana.
 
Jidanganye. Kuna wanaokaa miaka 15 sehemu na bado wanaendelea na kazi. Lakini kama wapo kazini si ndio vizuri kuwa nchi ni salama? Au mlitakaje? Wasiwepo watu kufuatilia usalama wa nchi?
 
Jidanganye. Kuna wanaokaa miaka 15 sehemu na bado wanaendelea na kazi. Lakini kama wapo kazini si ndio vizuri kuwa nchi ni salama? Au mlitakaje? Wasiwepo watu kufuatilia usalama wa nchi?
Story za vijiweni raha sana..

Ni kweli upo sahihi.
 
Hivi vyuo vya kibongo unapata wapi muda wa kukariri madesa,course work na kwenda kufanya biashara ya kuuza madafu ambayo hujui mnunuzi atakuja kununua muda gani? Au wakiyafikisha hapo A-Z yananunuliwa yote kila siku?
Ndio issue za waandishi wangetakiwa wamtafute wajadiliane nae. Pia walimu wake wangehojiwa kuonyesha maendeleo yake chuoni. Lakini sababu viongozi waliopita waliacha kuendeleza kada ya habari basi ngoja tuendelee kumpongeza mama Samia kwa juhudi anazofanya kuboresha taaluma ya habari
 
TISS ndio huwa Wahandisi wakuu wa kutunga Maigizo ya namna hii. Ndio kazi pekee wanayoiweza.
 
Siwezi kushangaa wakiwa wauza madafu wa kawaida.

Wabongo wengi wanapenda stories za kuungaunga na conspitacy theories.
 
Machizi wote unawaona mtaani ni wana usalama wako kazini.
kuna chizi mmoja yeye alikuwa anatembelea vijiwe vya bodaboda/bajaji, kahawa na vijiwe vya magazeti. Akifika tu anaanza kufanya sarakasi na kujikunjakunja kama nyoka. Ni mtu wa mazoezi anaoneka alivyojaziajazia mwili wake. Uchafu wake unaonekana ni wa kujipaka. Akishamaliza misheni yake hutoweka eneo hilo na hatimae kutoweka mji huo
 
hata hawa wanaouza bidhaa mikononi wakitembeza kwenye mabaa, migahani, mahotelini na kwenye magesti ni wa kutiliwa shaka kwani miili yao imeshiba ni wakakamavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…