Waliowahi kuwa wanene au vibonge, tukutane hapa

Waliowahi kuwa wanene au vibonge, tukutane hapa

Niliwahi Kuwa mnene hadi nikawa najikatia tamaa jinsi nilivyo,unene usikie kwa jirani unachosha sana,kilo zangu hazikuwa chini ya kg120.sasa hivi Nina kg70.,kama unapiga gym na wewe ni mnene usinyanyue vyuma we pendelea kukimbia na kuruka kamba au kuendesha baskel Mazoezi haya yanapunguza mwili kwa kasi kuliko ..unapotoa jasho jingi ndivyo na uzito unashuka kwa haraka,Mimi nilifikia kuondoa hadi kilo 1 kwa siku.!
kilo 1 kwa siku??Hukutumia pills kweli??Maana hyo ratio ni kubwa sanaaaa..
ujue kwa mwanaume anahitaji kalori 2640 zitokanazo na chakula ulacho kwa Siku,kwa mwanamke inacheza kwenye 1780 km sijasahau.,Ss hyo ratio yko kidogo inatisha kwakua wakat unapunguza fat percentage iliyopo mwilini still utakua unakula ili shughuli zingine za mwili ziendelee,Mkuu hbu funguka vzr hpo tafadhali
 
Ninafanya mazoez roho inaniuma kweli kuamka alfajir ila ntafanyaje lakin nlipungua kilo mbili nimepumzika wiki mbili et Nina 73 ndo nimeanza tena nataman niwe na 55. Lakin sijui nifanyaje kuitwa binge ni kero
Kilo 73 unaitwa bonge!? Labda kama Wewe ni mfupi!!!
 
Kabla ya ujauzito nilikuwa 55 kg, ile kujifungua nikajikuta nachezea 80kg...minyonyo hiyo, mitako kule, nilikuwa sijipendiiii.
Nilianza kwenda job kwa miguu asubuhi, plus nikawa nafunga. now nimerudi kuwa kamodo kama sijazaa.
 
Dah mi hili tambi linanitesa balaa, sijui nitumie nini liishe.... Nikitembea padogo tu ulimi nje[emoji36][emoji26][emoji36][emoji36]
 
Doh mimi nafanya mazoez mara moja kwa week mbili au mwezi, yaan naamka asubui naruka kamba ata round 100, lakn baada ya apo nakaa tena ata mwezi bila tizi, mvivu kupitiliza
 
Back
Top Bottom