mkuu ndio maana nikasema kadanganya kama mtaalam wa uchumi na masoko ya kifedha huwezi kuongea mbele ya chombo cha habari na kusema mgongano wa kifedha umesababishwa na vita ya iraq na kupanda kwa mafuta.....Amesema matatizo ya nishati na vita yamechangia financial crisis, hayo ya mortgage defaults 'wall street finacial analyst' hakuyataja?
sisi wakazi wa kinyerezi hatuna muakilishi online wa kutusemea......- Duh jamaa umemshitukia kuwa ni mtupu? Acha kunivunja Mkulu UM mbavu Bwa! ha! ha! ah! ah! ha!
Respect.
FMES!
sisi wakazi wa kinyerezi hatuna muakilishi online wa kutusemea......
....hapa najua hugusi hamna longo longo zinaongea fact sio za chimwaga
Soma maelezo haya.....
Ukweli ni kwamba Mpasuko wa uchumi umeanzishwa na tatizo mmoja tuu nalo ni subprime meltdown ( Kushindwa kwa watu wenye kipato cha chini kulipa madeni yao ya nyumba).
Mpasuko ulianza kuonekana mwaka 2007 mwezi wa 8 siku ambayo Cit bank walitangaza hasara ya mabilioni ya fedha kwenye mapato yao ya nusu mwaka. Jee swala la suprime linachangia vipi? Habari ni hii; mwisho mwa miaka ya 90, chama cha democratic waliandaa mswada wa sheria ya kupunguza vigezo za kupata mkopo wa nyumba. Mswadwa huo ulipita na kuwa sheria. Mwanzoni mwa 2000 baada ya Bush kuingia madarakani agenda mpya ilikuwa ni kupandisha namba ya wanaomiliki nyumba kwa 5%. Vile vile mwanzoni mwa miaka hiyo ya 2000 wataalamu wa Hisabati wakaja na formula mpya ambayo inaweza kuchanganya riski kutoka kwa wakopaji mbali mbali na kutengeneza mfuko mkubwa wa wadaiwa ambao ukigawanya vipande vipande unaweza kuuzwa kama share (mortgage backed security maarufu kama derivatives).
Mabenki makubwa yakaona faida ya hizi security (yaai hii mifuko ambayo imetengenezwa kwa kuchanganya mikopo ya nyumba ya watu mbali mbali), ili likahamsha ununuzi wa madeni ya wamiliki wa nyumba kutoka kwenye benki ndogogo ndogo kwenda kwenye benki kubwa. Yaani mfano rahisi ni kwamba benki ya nyumba ya Tanzania wanakopesha, kisha wanachanganya mkopo wangu na wa Michuzi na wanawauzia bank kubwa kama CRDB, then CRDB wanakatakata hii mikopo miwili katika vipande vipande na kuviuza kwa wananchi mbali mbali duniani. TATIZO LINAKUJA KWAMBA Benki ya nyumba sababu haikai na hii mikopo hivyo inakuwa haijali nani anakopa sababu CRDB yeye atanunua kwa vyoyote vile. Hivyo matokeo yake ni kwamba mtu asiye na vigezo vya kupewa mkopo akawa anapewa bila tatizo lolote. SASA, SIKU YA SIKU IKAFIKA WATU WAKAABZA KUSHINDWA KULIPA MALIPO YAO YA KILA MWEZI KWENYE HII MIKOPO, HAPO NDIO HILI DHAHAMA LILIPO ANZA KATIKATI YA MWAKA 2007.
Wakopeshwaji walipoanza kushindwa kulipa malipo ya mwezi, maana benki kubwa zikaanza kushindwa kuwalipa wawekezaji walionunua shea, na Insuarence company (AIG) ambazo ziliweka bima kwenye hii mifuko zikaanza kushindwa kulipia na tatizo likaawa linazidi kutanuka.
Kwa nini John Mashaka is wrong? hii ni sababu; Uchumi wa Marekani mpaka mwaka 2008 kwa asilimia zaidi ya 40% ulikuwa ukishikiliwa na Mashirika ya fedha (financial Institutions). 40% Ya Index kubwa kama Standard and Poor 500(s&p 500) ni makampuni ya fedha. Kumbuka ya kwamba makampuni yote ya fedha kwa njia moja au nyingine yameusika kuuza hizi shea hewa kwa jamii. Matokeo yake ni kwamba kadri muda ulipozidi kwenda ndio watu walio kopeshwa nyumba walishindwa kulipa, na mabenki yanajiendesha kwa kukopesha na sio other wise. Sasa kama watu hawalipi madeni yao matokeo yake ni kwamba ukopeshaji unapungua na sheria za kukopa zikaanza kuzidi (ndio unakumbuka neno Credit Crunch lilitawala sana muda fulani). Sasa benki zinapoacha kukopesha maana yake ni kwamba Uwekezaji nazo unapungua, na kama uwekezaji zinapungua maana yake ni kwamba watu wanapunguzwa kazi.
Uchumi wa Marekani unaangalia mambo 3, Inflation (mlipuko wa bei), idadi ya watu wasio na kazi (unemployment rate) na ukuaji wa uchumi (economic Growth). Lolote kati ya haya matatu likisumbua ndio utaona seriakali inakimbilia kwenye mambo mawili yaani Fiscal Policy (kama kuwapa watu cheki za bure ili wakatumie) au monetary policy (Banki kuu ya marekani kupunguza kiwango cha riba.) Haya yote yamekwisha fanyika lakini hali bado ni tete. Makampuni makubwa ya fedha bado yanatapa tapa, mengi yamekwisha anguka. Sasa kumbuka kama 40% ya uchumi unategemea makampuni ya fedha haya makampuni yakiyumba kidogo tuu uchumi lazima uterereke.
Vita ya Iraq sio sababu ya kusumbua uchumi wa America, kama unajua uchumi vizuri utakumbuka ya kwamba Marekani ilikwenda kwenye dipression mwaka 1929, baada ya hapo mambo yalikuwa mabaya sana kwenye uchumi wa marekani, mpaka mwaka 1940 ambako America ilikwenda kwenye vita vya dunia. Na baada ya hapo Uchumi ulisimama. Uchumi wa America unategemea kazi na kama kazi zipo basi hakuna tatizo. Sasa sidhani kama vita ya Iraq ndio iwe tatizo, wachumi wengi hapa marekani hawaliweki hilo hata kwenye mabano.
Ongezeko la bei ya mafuta sio tatizo la kusumbua uchumi. Kumbuka ya kwamba Mafuta yamepanda bei kuanzia mwishoni mwa 2006 mpaka mwisho mwa 2008. Na mafuta yashapanda kabla, Ulaya wanalipa mafuta ghali kwa miaka yote mbona chumi zao hazitetereki? Jee kuna uwiano gani kati ya $80 na Economic downturn? I need data na sio kelele kama kasuku.
Bei ya mafuta sio kwamba yaliweza kuathiri mambo 3 Inflation, Unemployment rate and Economic growth na usipo adhiri haya mambo 3 huwezi kuyumbisha uchumi wa marekani.
Lol wakuu mmemuelewa FMES?-Wenzako tunazo share huko labda tukupe darasa tu jinsi mchezo unavyochezwa huko Wall Street mkuu, hatusomi kwenye magazeti tu na online ni Alhamis tu nilikuwa pale 747 7Th Avenue, NYC kwenye ghorofa ya 21 unajua kufuatilia haya mambo mkuu, vipi unajua hiyo address ina jengo la nani? Haya ya wall Street huyawezi mkuu lakini tunaweza kukupa darasa ikibidi! Bwa! ha! ha! ah!
-
FMES
Yo Yo;
Soma maelezo haya.....
Ukweli ni kwamba Mpasuko wa uchumi umeanzishwa na tatizo mmoja tuu nalo ni subprime meltdown ( Kushindwa kwa watu wenye kipato cha chini kulipa madeni yao ya nyumba).
Quote:Yo Yo
Mpasuko ulianza kuonekana mwaka 2007 mwezi wa 8 siku ambayo Cit bank walitangaza hasara ya mabilioni ya fedha kwenye mapato yao ya nusu mwaka
Mijadala mingi imeibuka na si jambo la ulazima uwe na degree ya uchumi ujue couses ya financial crisis duniani.Its a shame kwa msomi na mwanaharakati kama John mashaka kupotosha umma kuwa mtikisiko wa kiuchumi unaondelea sasa hivi umetokana na sababu moja wapo ikiwa vita ya Iraq na ongezeko la bei ya mafuta.
John mashaka kama msomi ni reflection ya wasomi wetu tunaowapa dhamana ya kutoa maamuzi sahihi kwa manufaa ya wananchi na matokeo yake ni kutumbukiza kwenye matatizo.
Nimemsikiliza kwenye interview yake na daily news nikasitika….is this the man called financial analyst? Muoneni muongo mkubwa wa wall street
Daily News | The leading Online news edition in Tanzania
- Ona sasa ni nani aliyekwambia kwamba huyu kijana anafanya kazi Wall Street? Huyu kijana anafanya kazi kwenye bank system moja kule North Carolina sio Wall Street.
Respect.
FMES.
1. Mkulu hebu nipe shule kwa lugha nyepesi, Serikali ya Nchi zinazoendelea zifanye nini ili kukabiliana na hili tatizo?
2. Thailand nadhani serikali inagawia wananchi wa kipato cha chini mshiko! I am ignorant na hii kitu TBH
3. Pili kwa kama mwanachi wa kule Mwanalumango nayetegemea kuuza embe anatakiwa afanye nini?
Natanguliza shukrani
Mwananchi wa Mwanalumango, anatakiwa tu ajiepushe na tamaa ya mambo makubwa na kuridhika na maisha madogo aliyonayo ya kujinyima nyima, kwa sababu uwezekano wake wa ku-progress ni mdogo sana katika kipindi hiki kibaya cha uchumi.
Wow!!! Jamani, instead of doubting his position at the Wall Street, lets debate his arguments. By the way he did mention about subprime meltdown as another factor of the current crisis. I also think he brought up energy as another factor. Anyways, I sometimes worry that our arguments become too personal and this just does not lead us anywhere. As far as I am concerned, there are so many Tanzania who have achieved so much and we should try to encourage them. I think Mashaka has become quite popular because he has a spotlight. Instead of discouraging him, we should rally behind his efforts. He is not always right, but he deserves constructive criticism.
Ciao
Wow!!! Jamani, instead of doubting his position at the Wall Street, lets debate his arguments. ..... Instead of discouraging him, we should rally behind his efforts. He is not always right, but he deserves constructive criticism.
Hatuwezi ku-ignore kwamba jamaa sio mkweli kuhusu career yake. Mtu anaeongea kwa kuji introduce kama mtalaam wa Wall Street maana yake kile anachokisema ana mamlaka nacho na na ujuzi nacho kwa msingi wa uzoefu/kazi yake. Sasa kama anaongopa kuhusu hilo hilo hatuwezi kuli ignore.
Abaki huko huko kumdanganya Michuzi na wasomaji wa blog ya Michuzi, sio hapa. Hakuna Wall Street North Carolina.
Jamani Mbona hilo la Mtaalamu wa Wall street sijalisikia au maskio yangu ndio mabovu? Nimeskikia akitambulishwa kama mtaalamu wa masuala ya kifedha anayefanya kazi katika masoko ya kifedha huko marekani. Je masoko ya kifedha wanamaanisha kuwa ni Wall street? Soko la kifedha ni wall street peke yake au kuna masoko mengine huko marekani?
Bado hajaacha hako ka uongo ka Wall Street ya North Carolina, akaondoe hako. Au amdanganye Michuzi na wasomaji wa Michuzi.
Ufisadi unaanzia hapo....yeye kama anavyojiita mtaalam wa fedha wa wall street hawezi kutudanganya sisi tusiojua a wala b ya uchumi.....hawa wsomi ndio waliotufikisha hapa na mitatizo kibao.......Nakubaliana nawe. Pia sababu ya kuanguka kwa uchumi inaweza kusababishwa na combination of factors. Wamarekani wanaweza kutopenda kuzitaja hizo sababu nyingine (mfano vita vya Irak na kupanda kwa bei ya mafuta) kwa sababu wanazozijua wao au haziwapendezeshi watawala. Lakini mtu mwingine kulingana na upeo wake wa kuangalia mambo anaweza kuunganisha matukio mbalimbali ili kujua kwa kina tatizo la kuporomoka kwa uchumi. Ndugu mashaka alijitahidi kuelezea sababu zaidi ya ile ambayo tunalazimishwa kuiclaim kuwa ndio sababu pekee.
hajajiita mtaalamu wa wall street bali mtaalamu wa masuala ya fedha anayefanya kazi katika masoko ya fedha. Hebu silikiliza vizuri mahojiano kupitia http://www.dailynews.co.tzanavyojiita mtaalam wa fedha wa wall street hawezi kutudanganya sisi tusiojua a wala b ya uchumi.....hawa wsomi ndio waliotufikisha hapa na mitatizo kibao.......
BTW chech this
YouTube - Keith Olbermann: The best explanation of the causes of the financial crisis you'll ever see