Wallace Karia amebakia kama mgombea Urais TFF, wagombea wengine wakosa vigezo

Wallace Karia amebakia kama mgombea Urais TFF, wagombea wengine wakosa vigezo

Atakayekujibu ajibu pia kwann wagombea wengine wote wakose ila yeye tu Karia ndio apate?
Waliokosa wadhamini ni uzembe wao. Hata wakipitishwa hawawezi kupata kura. Hizi sheria zipo lakini wanakaa kimya baadaye wanaanza kulalamika.
 
Kwakweli sijui, kina Mayay ndio wanajua.

Kama walizifahamu mapema basi wamechemka. Mambo mazuri yanahitaji kupambaniwa!

Lakini tujiulize, kwa mfano, unajua unahitaji wadhamini, je utasubiri muda wa uchaguzi au utaanza kampeni mapema? ukianza kampeni mapema ukibainika unatolewa kwenye mchakato.

Ukisubiri muda wa endorsement unakuta ni muda finyu sana kana kwamba mpaka uzunguke mikoani unakuta muda haukutoshi. Pia, muda huo ukipiga simu ya mjumbe hapokei au anapokea anakwambia tayari nimeishamdhamini mgombea mwingine.

Sehemu yoyote yenye ridhiki kwa Afrika hasa kusini mwa jangwa la sahara ina utata sana. Kumbe reforms ni kila sehemu zinahitajika.
Kampeni unaanza mapema kwa kuongea na wadhamini ana kwa ana. Hiyo iko hivyo hata kwenye siasa.Mtu kama Ali Mayay anakosaje watu watano tu wa wakumdhamini?
 
Iki kitu kipo muda mrefu kuanzia uchaguzi uliopita hii sawa na wale wajumbe wa ccm lazima uanze kula nao na kuwekeza kwao miaka 4 kabla ya uchaguzi ili waweze kukuchagua.
Sasa huyu msomali sio mchoyo kiujumla anakula nao Ally Mayai ni mabahili uchaguzi uliopita alikosa sifa kwa kukosa wadhamini nilitegemea awamu hii atajipanga lakini napo kakosa , wanachama wote wa yanga waligombea kwa mihemuko wakati wakijua fika hicho kipengele cha mdhamini ni kigumu sana kukitimiza.Karia sio mchoyo mgao wa fifa lazima uwafikie wajumbe wote ili nao waweze kuinjoi.
 
Ile pingamizi ya wale lastborn imeishia wapi kwani,si walimuwekea pingamizi aondolewe?
Kuwekewa pingamizi na kushinda haina maana kuwa unasifa jifunze zaidi kujenga hoja. Pingamizi ni mambo ya kisheria siyo kubet
 
Kuwekewa pingamizi na kushinda haina maana kuwa unasifa jifunze zaidi kujenga hoja. Pingamizi ni mambo ya kisheria siyo kubet
Basi wewe mwenye hoja Karia kaondolewa asigombee,ukiwa Yanga akili nadhani huwa zinahama hata kama ulisoma,🤣🤣🤣
 
Mwenyekiti wa uchaguzi TFF hatoshi hana uwezo wa kutasfsiri sera za michezo Tanzania
 
Kwa mataifa ya mpira huyu karia wala hata asingethubutu kuchukua form ya kugombea tena, maana kwa mambo ya ovyo ovyo yanayoendelea kwenye soka letu yalitosha kumfanya ajiuzulu.
Mambo ksma yapi ayo yangemfanya ajiuzuru??
 
Mambo ksma yapi ayo yangemfanya ajiuzuru??
Kushindwa kwake kuhandle siasa za simba na yanga ambazo zinaleta kichefu chefu kwenye soka letu na kuchafua taswira nzima ya mchezo huo, na hata suala la Yanga kutokulipwa zawadi ya mshindi ya michuano ya msimu uliopita kiasi cha kuharibu reputation ya mdhamini... hapo bado sijaongelea vilio vya waamuzi wanaoendekeza rushwa.. kwa ufupi yapo mengi sana yanayo mdisqualify kuendelea kukalia hicho kiti.

Kwa wenzetu ambao wako serious na mpira mtu kama Karia hawezi kabisa kuwa hata kiongozi wa soka ngazi ya mkoa, ila kwa huku Mavumbini anaonekana ni Mungu mtu kisa tu kawapeleka Afcon mara kadhaa.
 
Back
Top Bottom