Wallace Karia amebakia kama mgombea Urais TFF, wagombea wengine wakosa vigezo

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
16,871
Reaction score
39,881
Nafasi ya Urais TFF imebakia 1 nayo ni ya Wallace Karia, wagombea wengine 6 wamekosa sifa kwenye mchujo na usaili wa awali

Tatizo kubwa lililowanyima sifa za kugombea Urais ni kukosa endorsement kila mgombea alitakiwa awe na angalau endorsement 5, ambapo mgombea Wallace Karia amevuna endorsement 46 kati ya 47

Nafasi za ujumbe TFF zimepata wagombea 10 kati ya 17 waliotuma maombi ya kugombea

Wagombea walioenguliwa wana siku 6 za kukata rufaa kama hawajaridhika na maamuzi

Uchaguzi unatarajiwa kufanyika Tanga August 16, 2025

1751629961290.png

Screenshot_20250704-132139.png
 
Unakuta jitu linalalamikia kwamba huku TFF mambo hayaendi sawa inatakiwa Karia aruhusu uchaguzi uwe huru na wa kidemokrasia wakati huo huo hilo hilo jitu linakwambia 2025 tunatiki, mama Samia mitano tena... Sasa ina maana lenyewe linaona kule Ccm demokrasia na uchaguzi huru havihitajiki kabisa. Huu ni unafiki mkubwa....

Ndo maana majitu kama ya akina Profesa Msola na majinga menzake natamani yaendelee kuchezea kichapo cha mjinga mwenzao Karia mpaka akili iwakae sawa...

TUNAPOTAKA REFORMS NI KWA AJILI YA MAISHA KWA UJUMLA SIO KWA AJILI YA SIASA TU.
 
Hahahahahahaha 😂🤣😂🤣😂🤣😂
 
Mwenye uelewa hiyo endorsement ndo IPO aje?
Nilivyofuatilia ni kuwa, endorsement ni uungwaji mkono kutoka mwenyekiti wa vyama vya mpira vya mikoa, ni kama vile wadhamini. Hao wajumbe ni wapiga kura wa uchaguzi wa TFTlF

Sasa TFF walibadilisha sheria kwamba, mjumbe mmoja atamdhamini mgombea mmoja tu tofauti na huko nyuma mjumbe mmoja anawaunga mkono wagombea zaidi ya mmoja. Mgombea mmoja anatakiwa kudhaminiwa na wajumbe kuanzia watano.

Sasa wanavyolalamika wagombea, endorsement zilikuwa ni siri kwa muda mrefu, wamekuja kushtukizwa dakika za lala salama kina Ally Mayay wanarudisha fomu muda wa kutafuta endorsement umeisha sijui.

Kitu kingine, hii kanuni inamsaida yule aliyepo Madarakani anaweza kuzinunua endorsement zote kutoka kwa wajumbe mapema, wewe ukienda unaambia umechelewa mjumbr ameishamuunga mkono mgombea mwingine.
 
Ooh Kwa hiyo pochi nene muhimu hapo.
 
Nafasi ya Urais TFF imebakia 1 nayo ni ya Wallace Karia, wagombea wengine 6 wamekosa sifa kwenye mchujo na usaili wa awali

Tatizo kubwa lililowanyima sifa za kugombea Urais ni kukosa endorsement kila mgombea alitakiwa awe na angalau endorsement 5, ambapo mgombea Wallace Karia amevuna endorsement 46 kati ya 47

Nafasi za ujumbe TFF zimepata wagombea 10 kati ya 17 waliotuma maombi ya kugombea

Wagombea walioenguliwa wana siku 6 za kukata rufaa kama hawajaridhika na maamuzi

Uchaguzi unatarajiwa kufanyika Tanga August 16, 2025View attachment 3393653
Huyu mzee serikali isipoingilia kati, hii taasisi itakuwa mali yake

Kaweka kamfumo kanakotunga sheria na taratibu zinazowafanya wakae pale milele🤣🙌
 
Back
Top Bottom