Wallace Karia analeta siasa na ubabe kwenye uongozi wa mpira nchini

Wallace Karia analeta siasa na ubabe kwenye uongozi wa mpira nchini

Mti Dawa

Member
Joined
Aug 10, 2022
Posts
6
Reaction score
20
HIi leo Rais Wa TFF amesikika katika mkutano na viongozi wa CAF na FIFA huko Arusha akiita wanafamilia wa mpira watu wenye mambo ya "kijinga-jinga".

Kauli hii ya kitemi kutoka kwa Rais wa mpira nchini, ni muendelezo wa ubabe na jeuri ambayo anaoionyesha mbele ya jamii ya wanamichezo nchini.

Karia anakosa weledi kwenye masuala ya mpira na uongozi, amejiambatanisha na viongozi wachache wa serikali kwa kutekeleza matakwa yao, na hiyo ndiyo inampa kiburi kisichomithilika.

Karia anatumika na watu wachache nje ya TFF kufanya maamuzi ndani ya TFF, kama hiyo haitoshi Karia anatumia rungu la kanuni kufungia watu kila kukicha, hizi kanuni zinapaswa kuatazamwa upya sababu zinatumika kama fimbo ya kuwaonea wanyonge na wasiwe na pa kukimbilia.
 
Karia ni dikteta..anaharibu futiboli ya nchi yetu iliyoanza kumea vizuri recently
 
Karia ni dikteta..anaharibu futiboli ya nchi yetu iliyoanza kumea vizuri recently
Ni vizuri kutambua kuwa futiboli ya nchi yenu imeanza kumea RECENTYLY chini ya uongozi wake.
 
Back
Top Bottom