SI KWELI Wallace Karia Rais wa TFF asema si vyema Yanga kwenda na ndege ya Rais baada ya kupoteza mchezo

SI KWELI Wallace Karia Rais wa TFF asema si vyema Yanga kwenda na ndege ya Rais baada ya kupoteza mchezo

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Salaam ndugu zangu,

Nimekutana na video fupi ikionesha Rais wa TFF Wallace Karia akisema kwamba itakuwa si vizuri kwa Yanga kwenda na ndege ya Rais baada ya kupoteza mchezo.

Je, kuna ukweli wowote wa juu ya hili? Tusaidieni kumhoji

1685472091640.png

Picha1: Sehemu ya Tweet inayomlaumu Rais Karia kwa kauli aliyotoa
1685472433381.png

Picha2: Sehemu ya Ujumbe wa Instagram ukimlaumu Rais Karia kwa kauli aliyotoa

1685473297190.png

Picha3: Sehemu ya ujumbe wa Ali Kamwe akikanusha uvumi unaoenea dhidi ya Rais wa TFF



Video namba 1


Video namba 2


Video namba 3
 
Tunachokijua
Kumeibuka hali ya lawama kutoka kwa Mashabiki wa timu ya Yanga kwenda kwa Rais wa Shirikisho la Mpira nchini Tanzania (TFF) Wallace Karia baada ya kuenea kwa video yenye sekunde 15 (Tazama video namba 1) ikimuonesha kiongozi huyo akiiongea kuhusu Safari ya Yanga na ndege ya Rais. Katika video hii Rais Karia ameonekana akisema.

-"Si vyema timu ya Yanga kusafiri na ndege ya Rais kwa sababu wamepoteza mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika dhidi ya timu ya USM Algers ya nchini Algeria."

Lawama hizi zimeshika kasi na kuenea kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii hasa Twitter na Instagram. Wadau wa soka hasa Mashabiki wa Yanga walioona wanamlaumu Karia kutamka maneno hayo wakiyatafsiriwa kama chuki dhidi ya timu ya yao (Yanga):

Lawama hizo zimejitokeza kwenye kurasa zifuatavyo:
- Katika mtandao wa Twitter Mdau anayeitwa Chriss Litombo Bangala amepost video ya sekunde 15 (Tazama video na picha namba 1) akiambatanisha ujumbe: "Ni Aibu kubwa kwa Kiongozi wa ngazi ya juu kwenye Mpira Tanzania,Anaongea Maneno ya Hovyo kabisa, Tukisema kua kiongozi huyu alituhujumu Yanga dhidi Mwarabu tutakua tunakosea kweli?"
- Kwenye mtandao wa Instagram Mdau anayejiita YangaWhatsapp_MakaoMakuu ameweka Video hiyo yenge sekunde 15 akiambatanisha na ujumbe wa kulaumu kauli ya Rais Karia kwa kusema "Huyu raisi kaaza uchochezi katuona tumenyamaza anatuaza." (Tazama picha namba 2).

Je, upi ni ukweli juu ya kauli na video hii?
JamiiForums imefuatilia vyanzo mbalimbali ili kujua uhalisia wa kauli hizo zinazodaiwa kutolewa na Karia tumebaini yafuatayo:

Kwanza, kupitia mtandao wa Twitter kwenye chapisho la Chriss Litombo Bangala linalomlaumu Rais Karia baadhi ya wadau wamejitokeza kupinga lawama hizo na kudai lawama hizo ni upotoshaji. Mfano, Vennatz1 amepiga hoja ya Chriss Litombo Bangala kwa kuweka video yenye sekunde 31 (Tazama Video namba 2) na kuweka ujumbe "Ni aibu kubwa sana kwako kupotosha umma"

Video hiyo iliyowekwa na Vennatz1 inaonesha kwa urefu zaidi kuhusu kilichokuwa kinazungumzwa na Rais Karia. Katika video hiyo Rais Karia anasema:

- "Wasaidizi wa Mama (Rais Samia) tayari wameshanifuata wameniambia niwatafute Yanga waniambie program yao wanaondoka lini kwenye mchezo wa marudiano. Lakini mimi nasema huo mchezo wa marudiano itakuwa sio vyema kuondoka na ndege ya Mama wakati tumepoteza hapa nyumbani. Tushikamane Watanzania wote (tuhakikishe Yanga anashinda hapa hapa nyumbani)."

Kutokana na video hii ya pili iliyowekwa na Vennatz1 kuna kauli Rais Karia amesikika akisema:

- "(tuhakikishe Yanga anashinda hapa hapa nyumbani)"

Kauli hiyo inaonesha kuwa Rais huyu alitoa kabla ya Yanga kucheza na USM Alger mchezo wa kwanza. Ambapo anahimiza Watanzania kufanya jitihada kuhakikisha Yanga inashinda mchezo wake wa nyumbani.

Naye Msemaji wa Yanga Ali Kamwe kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram amepost video yenye urefu wa sekunde 31 na maelezo yanayokanusha lawama anazopewa Rais wa TFF (Tazama picha namba 3). Kamwe ameandika

-"Hii ndio kauli sahihi ya Rais wa TFF, Wallace Karia.. Ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya waandishi wanaingia kwenye mkumbo wa upotoshaji kwa kuikata kwa Makusudi kauli ya Rais wa TFF na kuipeleka hewani .. Hii Sio sawa."

Zaidi ya hayo, Video hiyo ikiwa na dakika mbili na sekunde 56 yenye maongezi ya Rais Karia kwa kirefu zaidi iliwekwa katika kurasa ukurasa wa Instagram wa Azamsports mnamo tarehe 18 May, 2023 ambayo ni siku 10 kabla ya mchezo huo wa awamu ya kwanza kati ya Yanga dhidi USM Alger kuchezwa (Tazama Video namba 3).

Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo vya taarifa na Video hizo tatu juu na uchambuzi huo, uvumi unaomlaumu Rais wa TFF kutaka Yanga wasipewe ndege ya Rais kwa sababu wamepoteza mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya USM Alger ni uzushi uliotokana na Video ndefu kukatwa sehemu ndogo na kutafsiriwa vibaya.
Back
Top Bottom