Wallah! Kama Simba SC itacheza Mpira Mkubwa iliyocheza Simba Day na TP Mazembe, kuna Mtu tarehe 25 anafungwa Goli 7

Wallah! Kama Simba SC itacheza Mpira Mkubwa iliyocheza Simba Day na TP Mazembe, kuna Mtu tarehe 25 anafungwa Goli 7

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Kuna Timu kwa nia njema tu naionya kwakuwa bado ina Jeraha la Kufungwa mara mbili Dar es Salaam na Port Harcourt isikubali Kucheza Mchezo wake wa Ngao ya Hisani (Jamii) na Simba SC tarehe 25 Septemba, 2021.

Kwa aina ya Mpira mkubwa (mwingi) na wa Kiwango cha Kimataifa iliyoucheza ( nikifurahishwa ) zaidi na Kasi ya Wachezaji, Pumzi, Nguvu na Ari ya Kiushindani waliyonayo naiona hiyo Timu itakayocheza nayo Jumamosi ijayo itafungwa hata Goli ( Bao ) Saba ( 7 ) kwa Sifuri (0).

Kwa Simba SC hii iliyopo sasa (na ambayo imeboreka zaidi) bado sijaona Klabu yoyote ile hapa nchini Tanzania ya Kucheza nayo na hata Kuifunga na kama Simba SC itafungwa na Klabu yoyote ya Tanzania basi itakuwa 95% hiyo Timu imeroga mno na 5% imehonga sana Waamuzi ili Waibebe.

Kwani ukiachilia mbali kuwa Simba SC ni Timu ya Wenye Nchi lakini pia ndiyo Timu pendwa na Mwenyezi Mungu na kwamba ameshaibariki zaidi kwa Mafanikio ya Kimpira.
 
Hivi unaweza kuwa mwenye nchi Bila kuwa mwananchi

Ko kifupi mwenyenchi ni mwananchi yaani kama vile kuwa waziri hadi uwe mbunge

Pale unapojiita mwenyenchi na kusahau ww ni mwananchi pia.

Ni vyema kujifariji mapema maana mpira umechezwa leo kama ndondo
 
vijana wanacheza vizuri, tatizo lililopo simba ya sasa sijaona bado mchezaji mwenye kubadili sura ya mchezo pindi simba inapozidiwa kama alivyokuwepo C.C.C.
 
Lawama zangu zimuendee kocha kwa kupanga kikosi kibovu kwa kuwaweka wachezaji wanyumbulifu nje na kuanza na wachezaji wawili wenye hadhi ya Mbeya City kama ma striker(Kibu na Mugalu).

Utaanzaje na Banda nje we kocha wa hovyo? Sako naye nje? Ukitegemea Mugalu na Kibu ndio wakupe matokeo! Simba tuliyoizoea ni Simba ya pira biriani na siyo mpira wa ki-Yanga Yanga na tukicheza na striker mmoja tu na viungo wengi. Kocha akiendelea kupanga ma striker wawili au watatu kwenye kikosi Simba hii haitofika mbali.

Falsafa ya Simba na huyu kocha kwa mimi naona haviendani kabisa. Sven alikuwa kocha muafaka kwa Simba na huyu Gomes sidhani kama atamaliza msimu huu.
 
Mpira mzuri upi?
Kipindi cha pili chote hakuna hata shuti moja lililolenga lango.

Hapa ni kujifariji tu
 
Aliye haribu leo ni Mugalu.
Kibu kacheza vizuri sana.

Mugalu ni kirusi pale Simba na kocha anampenda sana.
Makosa ya miaka yote bado anayarudia kila kukicha.
Anakosa goli la wazi halafu anatabasamu.

Ningekuwa na maamuzi Simba ningevunja mkataba wa Mugalu leo hii.

Sijawahi kusikia mshambuliaji anasajiriwa ili akabe mabeki, sijawahi kusikia kabisa.
 
Kuna Timu kwa nia njema tu naionya kwakuwa bado ina Jeraha la Kufungwa mara mbili Dar es Salaam na Port Harcourt isikubali Kucheza Mchezo wake wa Ngao ya Hisani ( Jamii ) na Simba SC tarehe 25 Septemba, 2021...
A hahaha🤣🤣🤣 uwa unajua kuwadanganya mbumbumbu wenzako aisee duh yaani unajitapa kabisa kuwa mmecheza mpira mkubwa na unaenda kumfunga yanga kwa mpira ule 🤣🤣🤣🤣 auna ata chembe ya aibu, mngecheza mafichoni nafikiri mngeficha mambo mengi lakini kwakuwa mmecheza adharani kila mtu ameona labda kipofu
 
vijana wanacheza vizuri, tatizo lililopo simba ya sasa sijaona bado mchezaji mwenye kubadili sura ya mchezo pindi simba inapozidiwa kama alivyokuwepo C.C.C.
Simba uwezo wanaona ,angalia walipofungwa walivyochangamka ,sema walifungwa zimebaki dk chache lakini unaona walivyokimbiza pia ,Sina wasiwasi na Simba tutafika mbali
 
Kuna Timu kwa nia njema tu naionya kwakuwa bado ina Jeraha la Kufungwa mara mbili Dar es Salaam na Port Harcourt isikubali Kucheza Mchezo wake wa Ngao ya Hisani ( Jamii ) na Simba SC tarehe 25 Septemba, 2021...
Yanga inaongoza kuzungumziwa humu jf,that shows how big they are..
 
Lawama zangu zimuendee kocha kwa kupanga kikosi kibovu kwa kuwaweka wachezaji wanyumbulifu nje na kuanza na wachezaji wawili wenye hadhi ya Mbeya City kama ma striker(Kibu na Mugalu)...
Wewe ni fara. Hilo pira birian simba alikuwa analicheza kwa kocha yupi?

Ni kweli jana kocha alizingua kuwaanzisha Kibu na kuwaacha akina Sakho na Banda. Lakini sio kusema eti kocha mbovu.

Si nyie mlikuwa mnapiga kelele kuhusu Sven leo mnasema alikuwa bora??

Acheni ushabiki maandazi
 
Nyie sisi tuna watu 🐒
IMG_20210919_134409.jpg
 
Hivi unaweza kuwa mwenye nchi Bila kuwa mwananchi

Ko kifupi mwenyenchi ni mwananchi yaani kama vile kuwa waziri hadi uwe mbunge

Pale unapojiita mwenyenchi na kusahau ww ni mwananchi pia.

Ni vyema kujifariji mapema maana mpira umechezwa leo kama ndondo
Kuna CCM na wenye CCM yao. Wengine wafuasi wa CCM. Usichoelewa nini hapo?
 
Kuna Timu kwa nia njema tu naionya kwakuwa bado ina Jeraha la Kufungwa mara mbili Dar es Salaam na Port Harcourt isikubali Kucheza Mchezo wake wa Ngao ya Hisani (Jamii) na Simba SC tarehe 25 Septemba, 2021.

Kwa aina ya Mpira mkubwa (mwingi) na wa Kiwango cha Kimataifa iliyoucheza ( nikifurahishwa ) zaidi na Kasi ya Wachezaji, Pumzi, Nguvu na Ari ya Kiushindani waliyonayo naiona hiyo Timu itakayocheza nayo Jumamosi ijayo itafungwa hata Goli ( Bao ) Saba ( 7 ) kwa Sifuri (0).

Kwa Simba SC hii iliyopo sasa (na ambayo imeboreka zaidi) bado sijaona Klabu yoyote ile hapa nchini Tanzania ya Kucheza nayo na hata Kuifunga na kama Simba SC itafungwa na Klabu yoyote ya Tanzania basi itakuwa 95% hiyo Timu imeroga mno na 5% imehonga sana Waamuzi ili Waibebe.

Kwani ukiachilia mbali kuwa Simba SC ni Timu ya Wenye Nchi lakini pia ndiyo Timu pendwa na Mwenyezi Mungu na kwamba ameshaibariki zaidi kwa Mafanikio ya Kimpira.
Poisonous umetisha
 
Nipo hapa Lubumbashi kwa mda nimejaribu kuwaonyesha clips za game ya jana nkawambia hii ndo Simba ya msimu huu mpya. Ki ukweli walichosema ni kuwa kama hii ndo Simba ya msimu huu basi club El Ahly wajiandae kurejesha kombe kwa Simba

Hii ni tafsiri ya kilichosemwa na wakongomani si maneno yangu.Naomba nieleweke hivyo tafadhari
#💪 1.
 
Back
Top Bottom