Walokole sasa wamegawana vituo vya daladala na spika na kufanya mahubiri

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
17,047
Reaction score
63,206
Sasa hivi Walokole wameamua kugawana hadi vituo vya daladala, Wakiwa na spika zinazounguruma, ni mwendo wa mahubiri tu mwanzo mwisho.

Mimi ninachojua kuna taratibu za kuendesha haya mambo ya mahubiri. Kuna ishu ya kelele, pia ambayo ni lazima idhibitiwe kwa mujibu wa sheria ya mazingira. Lakini Serikali imeliacha hili jambo.

Je hakuna utaratibu, kanuni zinazotawala matumizi ya vipaza sauti mitaani?. Kwa nini serikali inaacha watu kwa kutumia mgongo wa dini wanaingilia haki ya wengine kupata utulivu?

Wahubiri hawa wanajihesabia haki, wao wanaamini kuwa kwa kuwa wanatangaza neno la Mungu kwa hiyo wana haki ya kufanya mahubiri popote na kwa kipaza sauti chochote wanachokitaka, na ukiwaambia kuwa huo siyo utaratibu wanakuhesabia dhambi.

Hata hivyo Yesu Mwenyewe amewahi kukemea wanaofanya maombi mitaani na kusema mfanyapo maombi msipayukepayuke, sasa nashangaa hawa walokole wanaohodhi vituo vya daladala na kupayukapayuka bila kujali haki za wengine za kupata utulivu iwezekanavyo.

Andiko linasema hivi:

"Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba". (Mathayo 6:7-8)

Haihishii hapo tu, kuna hawa wa vituo vya daladala, lakini kuna wale wanaopanda daladala na kuanza mahubiri. Aisee.

Ila mwisho wa mahubiri hayo huwa ni KUOMBA SADAKA.
 
hilo Andiko ulilotaja hapo linazungumzia kusali. Kuna tofauti ya kusali na kuhubiri. Kuhubiri ni kupiga panda. Ni kuwasikilizisha wote ujumbe wa Mungu. Atakayeusikia na kuufuata itakuwa heri yake, asiyetaka atajua mwenyewe! Injili lazima ihubiriwe kwa kila kiumbe.

“Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
”
— Marko 16:15 (Biblia Takatifu)
 
hilo Andiko ulilotaja hapo linazungumzia kusali. Kuna tofauti ya kusali na kuhubiri. Kuhubiri ni kupiga panda. Ni kuwasikilizisha wote ujumbe wa Mungu. Atakayeusikia na kuufuata atakuwa hei yake, asiyetaka atajua mwenyewe! Injili lazima ihubiriwe kwa kila kumbe.

Hata kusali husali kwa makelele pia
 
Sasa hivi Walokole wameamua kugawana hadi vituo vya daladala, Wakiwa na spika zinazounguruma, ni mwendo wa mahubiri tu mwanzo mwisho.

Mimi ninachojua kuna taratibu za kuendesha haya mambo ya mahubiri. Kuna ishu ya kelele, pia ambayo ni lazima idhibitiwe kwa mujibu wa sheria ya mazingira. Lakini Serikali imeliacha hili jambo.

Je hakuna utaratibu, kanuni zinazotawala matumizi ya vipaza sauti mitaani?. Kwa nini serikali inaacha watu kwa kutumia mgongo wa dini wanaingilia haki ya wengine kupata utulivu?

Wahubiri hawa wanajihesabia haki, wao wanaamini kuwa kwa kuwa wanatangaza neno la Mungu kwa hiyo wana haki ya kufanya mahubiri popote na kwa kipaza sauti chochote wanachokitaka, na ukiwaambia kuwa huo siyo utaratibu wanakuhesabia dhambi.

Hata hivyo Yesu Mwenyewe amewahi kukemea wanaofanya maombi mitaani na kusema mfanyapo maombi msipayukepayuke, sasa nashangaa hawa walokole wanaohodhi vituo vya daladala na kupayukapayuka bila kujali haki za wengine za kupata utulivu iwezekanavyo.

Andiko linasema hivi:

"Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba". (Mathayo 6:7-8)

Haihishii hapo tu, kuna hawa wa vituo vya daladala, lakini kuna wale wanaopanda daladala na kuanza mahubiri. Aisee.

Ila mwisho wa mahubiri hayo huwa ni KUOMBA SADAKA.
Msiwadhihaki Maana tupo ktk nyakati ngumu za mwisho. Nawe okoka uingie mbinguni
 
Back
Top Bottom