Walokole sasa wamegawana vituo vya daladala na spika na kufanya mahubiri

Walokole sasa wamegawana vituo vya daladala na spika na kufanya mahubiri

Sasa hivi Walokole wameamua kugawana hadi vituo vya daladala, Wakiwa na spika zinazounguruma, ni mwendo wa mahubiri tu mwanzo mwisho.

Mimi ninachojua kuna taratibu za kuendesha haya mambo ya mahubiri. Kuna ishu ya kelele, pia ambayo ni lazima idhibitiwe kwa mujibu wa sheria ya mazingira. Lakini Serikali imeliacha hili jambo.

Je hakuna utaratibu, kanuni zinazotawala matumizi ya vipaza sauti mitaani?. Kwa nini serikali inaacha watu kwa kutumia mgongo wa dini wanaingilia haki ya wengine kupata utulivu?

Wahubiri hawa wanajihesabia haki, wao wanaamini kuwa kwa kuwa wanatangaza neno la Mungu kwa hiyo wana haki ya kufanya mahubiri popote na kwa kipaza sauti chochote wanachokitaka, na ukiwaambia kuwa huo siyo utaratibu wanakuhesabia dhambi.

Hata hivyo Yesu Mwenyewe amewahi kukemea wanaofanya maombi mitaani na kusema mfanyapo maombi msipayukepayuke, sasa nashangaa hawa walokole wanaohodhi vituo vya daladala na kupayukapayuka bila kujali haki za wengine za kupata utulivu iwezekanavyo.

Andiko linasema hivi:

"Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba". (Mathayo 6:7-8)

Haihishii hapo tu, kuna hawa wa vituo vya daladala, lakini kuna wale wanaopanda daladala na kuanza mahubiri. Aisee.

Ila mwisho wa mahubiri hayo huwa ni KUOMBA SADAKA.
Tuacheni,kwani na nyinyi mwisho wa siku si mnakua mmepata neno la Mungu...
 
Sema hupendi kulisikiliza Neno la Mungu tu.Yaani unakerwa na Neno la Mungu (Injili).Just imagine kama mtu ni mwizi,mzinzi,mwasherati,muongo,mtoa rushwa,msengenyaji,nk atafurahia kulisikia Neno la Mungu au Injili inayokemea hayo?
1Wakorintho6:9-10
Wagalatia5:19-21
Ufunuo21:8
Harafu tofautisha kati ya Kusali na Kuhubiri Neno la Mungu.
Yesu alichosema kwenye andiko hilo ulilonukuu,(Mathayo6:1-6) linahusu pale watu wanapokuwa wanasali siyo kuhubiri Neno la Mungu.
Kupayukapayuka kwa mjibu wa maandiko ni kuomba kwa kurudiarudia maneno yale yale lakini siyo kupiga kelele.
Kuhubiri Neno mahali pa wazi kama barabarani,vituo vya basi,sokoni siyo kosa! Isipokuwa mahali ambapo panahitaji utulivu ndiyo hawaruhusiwi kuhubiri kwa kupaza sauti mf.hospitali,maofisini,nk (pale wataomba ruhusa ya kushuhudia watu Neno la Mungu bali kwa sauti ya kawaida mf.kuzungumza na wagonjwa ili kuwaombea.
Mkuu kwa malalamiko yako vile vile usisahau kuiambia Serikali kuhusu Alfajiri kwenye Misikiti wanavyo tuamsha kwa VIPAZA SAUTI tukiwa tumelala.
Dawa:
Sikiliza Injili ili uokolewe na Hukumu inayokuja juu ya kila atendaye dhambi,(Marko16:16-17),(Warumi3:23)
Na mshahara wa dhambi ni Mauti,(Ufunuo21:8)
Bali aaminiye na Kubatizwa ataokolewa na hukumu.
Mungu akubariki sana.🙏🙏
 
Hao walokole mabarabarani hawahubiri tu bali wanasali pia kwa sauti ya juu kwa kutumia maspika yao huku wakipayukapayuka kinyume cha mafunzo ya Yesu kuwa tusalipo tusipayukepayuke.
 
Kwani adhana ikpiligwa asubuhi wakati tumelala au kengele ya kanisa katoliki mbona tunakaa kimya? Huo ndio uvumilivu na kuvumiliana.
 
Back
Top Bottom