Walokole sasa wamegawana vituo vya daladala na spika na kufanya mahubiri

Tuacheni,kwani na nyinyi mwisho wa siku si mnakua mmepata neno la Mungu...
 
Sema hupendi kulisikiliza Neno la Mungu tu.Yaani unakerwa na Neno la Mungu (Injili).Just imagine kama mtu ni mwizi,mzinzi,mwasherati,muongo,mtoa rushwa,msengenyaji,nk atafurahia kulisikia Neno la Mungu au Injili inayokemea hayo?
1Wakorintho6:9-10
Wagalatia5:19-21
Ufunuo21:8
Harafu tofautisha kati ya Kusali na Kuhubiri Neno la Mungu.
Yesu alichosema kwenye andiko hilo ulilonukuu,(Mathayo6:1-6) linahusu pale watu wanapokuwa wanasali siyo kuhubiri Neno la Mungu.
Kupayukapayuka kwa mjibu wa maandiko ni kuomba kwa kurudiarudia maneno yale yale lakini siyo kupiga kelele.
Kuhubiri Neno mahali pa wazi kama barabarani,vituo vya basi,sokoni siyo kosa! Isipokuwa mahali ambapo panahitaji utulivu ndiyo hawaruhusiwi kuhubiri kwa kupaza sauti mf.hospitali,maofisini,nk (pale wataomba ruhusa ya kushuhudia watu Neno la Mungu bali kwa sauti ya kawaida mf.kuzungumza na wagonjwa ili kuwaombea.
Mkuu kwa malalamiko yako vile vile usisahau kuiambia Serikali kuhusu Alfajiri kwenye Misikiti wanavyo tuamsha kwa VIPAZA SAUTI tukiwa tumelala.
Dawa:
Sikiliza Injili ili uokolewe na Hukumu inayokuja juu ya kila atendaye dhambi,(Marko16:16-17),(Warumi3:23)
Na mshahara wa dhambi ni Mauti,(Ufunuo21:8)
Bali aaminiye na Kubatizwa ataokolewa na hukumu.
Mungu akubariki sana.πŸ™πŸ™
 

Hao walokole mabarabarani hawahubiri tu bali wanasali pia kwa sauti ya juu kwa kutumia maspika yao huku wakipayukapayuka kinyume cha mafunzo ya Yesu kuwa tusalipo tusipayukepayuke.
 
Kwani adhana ikpiligwa asubuhi wakati tumelala au kengele ya kanisa katoliki mbona tunakaa kimya? Huo ndio uvumilivu na kuvumiliana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…