Wamachinga Simu 2000 wamshukia Albert Chalamila, wasema kauli kuwa machinga wanatakiwa kustaafu miaka mitatu ilhali wanasiasa hawastaafu inashangaza

Rais hawezi kumtuma mkuu wa mkoa akaongee ujinga kama ule.

Acha kumsingizia Rais kwa mambo yanayofanywa na watu wenye mihemko wasiojua nini chakusema.

Kama Rais angekuwa anamtuma kwanini Rais alimwambia Chalamila aache tabia yake ya ujeuri na Chalamila akakiri ameacha?
Nimeipenda hii
 
Na ukaamini?Wanyamwezi wanasema "ulisyentekwa"/ulinunuliwa pipi(mtoto) ili unyamaze kulialia kwa kipondo ulichopewa na mtoto mwenzako michezoni.🤣🤣🤣🤣🙏
 
Kamati ya maboresho ya Soko la Simu 2000 chini ya mwenyekiti wake pamoja na wafanyabiashara na wadau wa stendi wa Simu 2000 wameongea na waandishi wa habari leo Julai 17, 2024 kuhusu yaliyojiri tangu kumaliza kikao chao na mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila.

Mosi, mwenyekiti amesema wafanyabiashara sio wavamizi kwenye eneo hilo bali waliletwa na Serikali. Wamesema kitendo cha Mkuu wa Mkoa kusema pale sio kwa mama zao na baba zao haikuwa kauli ya kiungwa na haikupaswa kutolewa na Kiongozi ambaye amepewa dhamana na Serikali ya kuhudumia wananchi kwa niaba.

Mwenyekiti amesema wao ni watanzania na baba na mama yao ni Tanzania na walipo ni sehemu yao maana wao ni sehemu ya watanzania kwasababu ipo kwenye ardhi ya Tanzania.

Mwenyekiti: Hawa viongozi tumewapa dhamana ya kuongoza na kusimamaia kero na changamoto zetu pamoja na mapungufu kama aliyaona mkuu wa Mkoa hakupaswa kuzungumza kauli kama zile ya kwamba Machinga sasa anatakiwa akae miaka miwili au mitatu awe amestaafu kuwa machinga, atoke sehemu kama hizi aende sehemu zingine.

Unajiuliza, hawa ni viongozi ambao wanaishi kwa kodi zetu, wanakaa miaka mitano mpaka kumi basi kwanini yeye hakuona umuhimu wa kutoa ushauri kwamba sasa wakuu wa mikoa kwasababu mikoa iko michache Tanzania na watanzania ni wengi na wao wanapenda kuwa viongozi, wanufaike na keki ya Taifa, kwanini asiwe wa kwanza kutoa mapendekezo sasa mkuu wa mkoa anatakiwa kukaa miaka miwili/mitatu baada ya hapo amuachie mtu mwingine.

Akaona hawa wamachinga ambao walikuwa wanakaa kwenye jua kwa muda mrefu, wamekuja sokoni kujitafuta anadhani miaka miwili inatosha kuacha umachinga na akatufute fremu, sijajua taaluma ipi ya uchumi inakubaliana na hili jambo.

Anasema mmefinywa na waume zetu mnajiliza hapa unafiki, kweli unamwambia mtu jambo analia machozi unamwambia ni mnafiki! Yale machozi ya wafanyabiashara waliona ni adha wanaenda kupitia kupitia huu mradi ndio maana walianza kupata picha ya nini kinafata kwasababu wameshahangaika muda mrefu. Walikuwa Ubungo wakatolewa, walikuwa wapi wakatolewa, wameshanyang'anywa mizigo sana, wameletwa sokoni wameambiwa sasa kaeni hapa ni sehemu rasmi, tena inakuja kwamba hapa sio sehemu rasmi.

Karakana ni muhimu kuliko wafanyabiashara wadogo wadogo, hii inaweza ikajenga picha sasa viongozi wa nchi yetu hawajali tena mtu wa hali ya chini na kuna wafanyabiashara walinifata wakaniambia kwelie angekuwepo marehemu haya maneno yasingewezwa kuzungumzwa.

Kauli za nitaamuru polisi wapige push up juu ya migongo yenu zilikuwa ni fedheha, ni udhalilishaji na ni kutweza utu wa mtu.

View: https://www.youtube.com/live/naKo4HNboMs

Wapewe flana za kijani na kofia, wasifie mpaka wasahau wake zao!
 
Hawa viongozi wao si walienda kule Dodoma badala waongee kero zao na kutetea wananchi wakarud na msemo wa "Mama tuvushe"

Hawa viongozi njaa ni nyoko sana
 
ha ha ha!
Ushauri kwa CHADEMA, wakae kimya, waache kila mtu asifie, nafasi za kuteuliwa kwa kusifia zitajaa, watakumbuka asali na maziwa ya Nchi ya ahadi.
Ila,sidhani kama nililenga hayo na CHADEMA.Wanapaswa na walipaswa kuyaelewa vema waliyoambiwa leo hadi wamejinunisha miaka ishirini nyuma kabla hawajapazoea hapo hadi kudhania ni nyumba yao waliyoijenga.Too late to lament!
 
Mwamba alikua kashatupia makoncho yake anawaona machinga kama wanafunzi mikono inawasha awachape viboko kama wale wanafunz wa mbeya
 
Ila,sidhani kama nililenga hayo na CHADEMA.Wanapaswa na walipaswa kuyaelewa vema waliyoambiwa leo hadi wamejinunisha miaka ishirini nyuma kabla hawajapazoea hapo hadi kudhania ni nyumba yao waliyoijenga.Too late to lament!
Well said, na bado itawatafuna.
Wamachinga wamebememndwa, wanafanywa kama yai la kuku lililotagwa kabla ya muda.
 
Chura Kiziwi japo unajifanya kiziwi ila inatosha sasa, mpumzishe huyu Mlevi Chalamila.

Kuna ukomo wa ubumbuwazi, hata kama kila kitu mpaka uambiwe na kushauriwa, hebu hili tumia akili yako mwenyewe hata kama ni ndogo.
 
Well said, na bado itawatafuna.
Wamachinga wamebememndwa, wanafanywa kama yai la kuku lililotagwa kabla ya muda.
Ndiyo ukweli huo.Wasijidekeze na kutaka kubakia kuwa wamachinga maisha yao yote.Kila kitu huanza,hukua,huzeeka na kufa/kupotea hata kwa kutekwa.Kila kazi ina muda wa kustaafu.Kama hadi kaya zenye uchumi duni zilizowekwa kwenye mpango wa kupata ruzuku chini ya mpango wa TASAF huwa wanastaafu,wao ni akina nani hasa hadi hawataki kustaafu?
 
Kamati ya maboresho ya Soko la Simu 2000 chini ya mwenyekiti wake pamoja na wafanyabiashara na wadau wa stendi wa Simu 2000 wameongea na waandishi wa habari leo Julai 17, 2024 kuhusu yaliyojiri tangu kumaliza kikao chao na mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila.

Mosi, mwenyekiti amesema wafanyabiashara sio wavamizi kwenye eneo hilo bali waliletwa na Serikali. Wamesema kitendo cha Mkuu wa Mkoa kusema pale sio kwa mama zao na baba zao haikuwa kauli ya kiungwa na haikupaswa kutolewa na Kiongozi ambaye amepewa dhamana na Serikali ya kuhudumia wananchi kwa niaba.

Mwenyekiti amesema wao ni watanzania na baba na mama yao ni Tanzania na walipo ni sehemu yao maana wao ni sehemu ya watanzania kwasababu ipo kwenye ardhi ya Tanzania.

Mwenyekiti: Hawa viongozi tumewapa dhamana ya kuongoza na kusimamaia kero na changamoto zetu pamoja na mapungufu kama aliyaona mkuu wa Mkoa hakupaswa kuzungumza kauli kama zile ya kwamba Machinga sasa anatakiwa akae miaka miwili au mitatu awe amestaafu kuwa machinga, atoke sehemu kama hizi aende sehemu zingine.

Unajiuliza, hawa ni viongozi ambao wanaishi kwa kodi zetu, wanakaa miaka mitano mpaka kumi basi kwanini yeye hakuona umuhimu wa kutoa ushauri kwamba sasa wakuu wa mikoa kwasababu mikoa iko michache Tanzania na watanzania ni wengi na wao wanapenda kuwa viongozi, wanufaike na keki ya Taifa, kwanini asiwe wa kwanza kutoa mapendekezo sasa mkuu wa mkoa anatakiwa kukaa miaka miwili/mitatu baada ya hapo amuachie mtu mwingine.

Akaona hawa wamachinga ambao walikuwa wanakaa kwenye jua kwa muda mrefu, wamekuja sokoni kujitafuta anadhani miaka miwili inatosha kuacha umachinga na akatufute fremu, sijajua taaluma ipi ya uchumi inakubaliana na hili jambo.

Anasema mmefinywa na waume zetu mnajiliza hapa unafiki, kweli unamwambia mtu jambo analia machozi unamwambia ni mnafiki! Yale machozi ya wafanyabiashara waliona ni adha wanaenda kupitia kupitia huu mradi ndio maana walianza kupata picha ya nini kinafata kwasababu wameshahangaika muda mrefu. Walikuwa Ubungo wakatolewa, walikuwa wapi wakatolewa, wameshanyang'anywa mizigo sana, wameletwa sokoni wameambiwa sasa kaeni hapa ni sehemu rasmi, tena inakuja kwamba hapa sio sehemu rasmi.

Karakana ni muhimu kuliko wafanyabiashara wadogo wadogo, hii inaweza ikajenga picha sasa viongozi wa nchi yetu hawajali tena mtu wa hali ya chini na kuna wafanyabiashara walinifata wakaniambia kwelie angekuwepo marehemu haya maneno yasingewezwa kuzungumzwa.

Kauli za nitaamuru polisi wapige push up juu ya migongo yenu zilikuwa ni fedheha, ni udhalilishaji na ni kutweza utu wa mtu.

Tunaomba kutumia fursa hii kumuomba mkuu wa mkoa kwamba hizi kauli asizitumie tena mahala popote ndani ya nchi yetu kwasababu pia zinaifanya Serikali ipate taswira mbaya kwa wananchi wake na kauli zile zinaweza zikajenga chuki baina ya Serikali na viongozi.

View: https://www.youtube.com/live/naKo4HNboMs

Hivi huyu Chalamila na Nape si huenda biological father wao akawa ni mtu mmoja!
 
Back
Top Bottom