Wamachinga: Tuko tayari kuandamana 2025 Rais aendelee kubaki madarakani

Wamachinga: Tuko tayari kuandamana 2025 Rais aendelee kubaki madarakani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wamachinga wa Dar wamesema wanamshukuru Rais Magufuli kwa kuwajali na kutengeneza mazingira bora ya kufanya kazi.

Wamesema hakuna Rais aliyefanyia wema kama Rais Magufuli hivyo wako tayari kuandamana ili Rais Magufuli abaki madarakani.

Aidha wamachinga wamesema uongozi waliokuwa nao kwa takribani miaka saba ni uongozi wa kiuanaharakati hivyo wanataka kuchagua viongozi kwa kukubaliana.

Matatizo mengine waliyoyataja ni pamoja na kuwa na namna rasmi ya kukopeshana ili kuweza kuongeza mitaji ya biashara.

 
Serikali inataka kupanua wigo wa vyanzo vya mapato, Ili mapato yaongezeke ni lazima wamachinga watolewe barabarani wakalipie leseni, Kodi ya mapato na kodi nyingine zilizopo. Hawa hawana cha kujitetea nacho zaidi ya kuandamana ili Magufuli abaki madarakani?

Halmashauri zitakapoanza kazi ya kuwaondoa hawa machinga barabarani wala Magufuli hataongea lolote kwa sababu mpango wa serikali ni kuongeza wigo wa makusanyo ya fedha. Kama hawaongezi huo wigo wa kuongeza mapato. Hii miradi lukuki aliyoianzisha Magufuli kwa fedha za ndani anaimaliziaje?
 
🤔 🤔wanatoa rai kwa niaba ya wamachinga wote wafanyao biashara nchi nzima!

The rise of Bahima empire in East Africa!

Ilianza kama conspiracy theories, sasa Bashite & co watakuwa kazini underground, wanakamilisha hili!

Everyday is Saturday...............................😎
 
JPM akiamua kuchukua njia hiyo itakua Tanzania haina tofauti tena na Burundi, Uganda, Rwanda, Sudan, Congo hatutakua na lingine la kujivunia, atakua ameturudisha nyuma miaka 50, pamoja na umasikini wetu na elimu mbovu ya CCM na uminyaji wa haki za binadamu bado tulikua na la kujivunia kwamba Rais anakaa miaka 10 tu.
 
Kwa mujibu wa miongozo anaepaswa kupewa kitambulisho ni yule anaeuza chini ya sh 10900 kwa siku lakini Sasa hao machinga wanaoandamana ni watu wanaouza zaidi ya 50,000 mpaka laki 3 kwa siku. Acha waandamane, ni wajanja hao wanaandamania maslahi.
 
Kwa mujibu wa miongozo anaepaswa kupewa kitambulisho ni yule anaeuza chini ya sh 10900 kwa siku lakini Sasa hao machinga wanaoandamana Ni watu wanaouza zaidi ya 50000 mpaka laki 3 kwa siku acha waandamane Ni wajanja hao wanaandamania maslahi
Hahahah hao wa Kariakoo ni kawaida kufunga 30-50K deile.
 
Back
Top Bottom